Mwigulu Nchemba: Tumefuta baadhi ya tozo, nyingine tumepunguza kwa asilimia 10-50
Screenshot_20220920-104557.jpg
 
Akizungumza leo bungeni, Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba amesema uongezwaji wa wigo wa kukusanya mapato kupitia tozo uliibua malalamiko kwenye jamii, hivyo Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi iliagiza upitiwaji upya wa tozo hizi na kuzingatia maoni ya wananchi.

Marekebisho yafuatayo yamefikiwa-
  • Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu kwa pande zote.​
  • Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja na kutoka benki moja kwenda benki nyingine.​
  • Kutowahusisha wafanya biashara wadogo (merchants) kama ilivyokuwa kweye kanuni ya sasa.​
  • Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki yaani ATM kwenye miamala yenye thamani ya chini ya tsh 30,000/=​
  • Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10-50 kutokana na makundi ya miamala​

Marekebiosho haya yataanza kufanya kazi Octoba 1, 2022. Aidha Serikali itafuta kodi ya zuio ya pango, hivyo kwa sasa itapaswa kulipwa na mmiliki wa nyumba na siyo mpangaji.

Kwa kuwa pesa hizi zitaipunguzia mapato serikali, Waziri ameelekeza Serikali ianze kubana matumizi yake mfano kwenye vikao, mafunzo ya semina, warsha, kukagua miradi n.k

Wataalamu wa wizara ya fedha na mipango ndiyo wamefanya mapitio haya wakiwa ofisini kwa kuwa ni sehemu ya majukumu yao. Taarifa za kuwa kuna tume iliundwa kutoka nje ya wizara ni uzushi.

Muulizeni wakati anaziweka alikuwa hajui kuwa zingetuumiza ( zingewaumiza ) Watanzania hadi Kutudharau na Kutudhihaki kwa kututaka kama tunaona Tanzania ni mbaya tukaishi ( tuhamie ) nchini Burundi?

Na hivi Mama jana kapanda Dala Dala la London huku akiwahi Dirishani na upepo kumtandika vilivyo Hasira zake zote akirejea anazimalizia Kwake kwa Kumtumbua hivyo aanze kujiandaa Kisaikolojia kwa hilo.

PhD imetua kwa Mtu wa hovyo mno.
 
Mama Samia kama unasikiliza tunaokutakia mema, hebu muondowe huyo muhuni Savimbi hapo treasure muweke Dr Kimei arekebishe mambo yakae sawa.

Haiwezekani mambo yanaharibika na Mtaalam wa fedha yupo back bench mnaendekeza makundi yenu tu na kuacha Mtaalam kama Dr Kimei kutokutumika, wengi tunaujuwa uwezo wa Dr Kimei na wengi tulidhani ndio angeteuliwa kuwa Gavana wa BOT badala ya Luoga.

Au marehemu kakurithisha bifu lake na wachaga?
 
Wafutee zoteee sio kujidai ametusaidia kumbee upuuzi tu anafanyaa..
 
Akizungumza leo bungeni, Waziri wa Fedha na Mipango Mwigulu Nchemba amesema uongezwaji wa wigo wa kukusanya mapato kupitia tozo uliibua malalamiko kwenye jamii, hivyo Kamati kuu ya Chama cha Mapinduzi iliagiza upitiwaji upya wa tozo hizi na kuzingatia maoni ya wananchi.

Marekebisho yafuatayo yamefikiwa-
  • Kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu kwa pande zote.​
  • Kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja na kutoka benki moja kwenda benki nyingine.​
  • Kutowahusisha wafanya biashara wadogo (merchants) kama ilivyokuwa kweye kanuni ya sasa.​
  • Kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki yaani ATM kwenye miamala yenye thamani ya chini ya tsh 30,000/=​
  • Kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10-50 kutokana na makundi ya miamala​

Marekebisho haya yataanza kufanya kazi Octoba 1, 2022. Aidha Serikali itafuta utaratibu wa kodi ya zuio ya pango inayotaka kukusanywa na mpangaji, hivyo kwa sasa itapaswa kulipwa na mmiliki wa nyumba na siyo mpangaji.

Kwa kuwa pesa hizi zitaipunguzia mapato serikali, Waziri ameelekeza Serikali ianze kubana matumizi yake mfano kwenye vikao, mafunzo ya semina, warsha, safai za ndani na nje, misafara, kukagua miradi n.k

Wataalamu wa wizara ya fedha na mipango ndiyo wamefanya mapitio haya wakiwa ofisini kwa kuwa ni sehemu ya majukumu yao. Taarifa za kuwa kuna tume iliundwa kutoka nje ya wizara ni uzushi.

Bado kabisa hoja yetu ni kwamba wafanyakazi tunapolipwa mishahara kupitia benki tayari tunakuwa tumelipa kodi.

Kwanini tulipishwe tena tozo, kusema umesamehe tozo kiwango kuanzia elfu 30 kushuka chini hii ni danganya toto hakuna mtu ataenda benki kutoa kiasi cha elfu 30. usitufanye sisi hatuna akili.
 
Kipengele cha kubana matumizi kimekaa vizuri..ila kuna maeneo hajayagusia kama kununua magari ya serikali ya bei nafuu na kupunguza posho za viongozi, mf. Wabunge.
 
Back
Top Bottom