Mwigulu: Tumesikia malalamiko ya Watanzania kuhusu tozo za miamala na Rais ametoa maelekezo ya kuzitazama upya
Rais hakosei 😂😂😂😂 alishamwaga wino kumbe alikuwa ANADEMKA! 🤣🤣🤣🤣🤣

Sifa Kuu za wakutanao kwa Kikao cha utatuzi wa 'Tozo Umiza na Komoa' ni kwamba wa Kwanza ni Muongo sana na ana Dhambi Kubwa ya Kudanganya Kaongea na Maiti na Kumjibu ni mzima, wa Pili anachokivaa Shingoni Kinamzidishia Upuuzi mno Kichwani mwake na wa Tatu ni kama vile Wizara anayoingoza imemsababishia Utaahira kwani yupo yupo tu na haeleweki wakati hiyo Wizara inahitaji Mtendaji mwenye Akili nyingi ambazo kwa bahati mbaya hana.
 
 
🤔🤔🤔🤔🤔

IMG-20210718-WA0139.jpg
 
Eti Rais, makamo wa Rais na waziri wake wote wasomi wa uchumi!!

Nafikiri ni uchumi wa maganda ya korosho.

Huku mtaani nawapa tu taarifa mpesa zishaanza kufungwa.

Failed state!
Upo sahihi mkuu. Kuna mmoja tu ndiye ambaye alinishawishi kutoa kahela kangu baada ya kutaka kutoa nikakutana na kiwango kikubwa sana cha kukatwa.

Njia yake yeye unakua kama unalipia bidhaa kwa kutumia LIPA namba ya vodacom
 
FAILED STATE kwa hiyo tusingelalamika ingekuwaje?
Feelings aside,mkuu hivi ushawahi hata kutafuta maana ya FAILED STATE?
Kwenye failed state hata haya maoni huwezi kuyatoa,a failed state ni zaidi ya neno lenyewe failed,jaribu kusoma zaidi ili siku ingine usiseme mbele za watu kuwa Tanzania is a failed state!
No offence though,,
 
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba, amesema jambo hilo tayari limefika kwa viongozi wakuu wa nchi na tayari Majaliwa ameitisha kikao na wizara ya fedha na Ile ya mawasiliano kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi.

Dk. Nchemba amesema kikao hicho kitafanyika kesho na hivyo ameowaomba Watanzania kuendelea kuwa watulivu na kuisikiliza serikali yao na siyo kusikiliza maneno ya watu ambao wamekua wakifanya upotoshaji mitandaoni.

"Niwaombe Watanzania muwe watulivu, jambo hili limeshafika kwa viongozi wetu wakuu na Rais wetu Samia Suluhu Hassan ameguswa nalo na amesikia maoni ya Watanzania, hivyo tayari ameshatoa maelekezo kwetu ya kufanyia kazi hoja zote zinazotolewa na wananchi," amesema.

"Tunaamini kupitia kikao na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kesho tutatoka tukiwa na muelekeo wa pamoja, kwa hatua ya Sasa niwasihi Watanzania kuendelea kuwa na imani na serikali yao na kumuunga mkono Rais Samia katika utekelezaji wa majukumu ya kuijenga Nchi yetu," amesema Dk. Nchemba.

Ametoa rai kwa wale wote wenye nia ovu kuacha kufanya upotoshaji kwa wananchi na badala yake amewaomba Watanzania kusikiliza maelekezo yote yanayotolewa na viongozi na kuahidi kuyatolea ufafanuzi na maelekezo mambo yote ya kikanuni.
"Rais Samia ana nia njema ya kuijenga Nchi yetu, ni jukumu letu kama wananchi kuendelea kumuunga mkono na siyo kusikiliza wababaishaji wanaofanya upotoshaji," amesema.

Waziri wa Habari na Mawasiliano, Dk. Faustine Ndugulile, amesema wizara yake itaendelea kushirikiana na wizara ya fedha katika kutolea ufafanuzi sheria hiyo, huku akiwaondoa hofu wananchi na kuwahakikishia kuwa serikali yao ni sikivu na inajali wananchi.
Serikali kamwe isijaribu kurudi nyuma, irekebishe tu viwango viwe reasonable.
 
Mnadhani ni ukweli kabisa ya kwamba Majaliwa kassimu Majaliwa alikuwa na taarifa za kifo wa Chuma JPM,

alafu akamua tuu yeye kusema JPM yuko mzima. Doest it make clear sense in your head ?

Mpaka leo !?
it didnt click to me!!
i couldnt buy that shtt!
it didnt feel right to me!
 
Mnadhani ni ukweli kabisa ya kwamba Majaliwa kassimu Majaliwa alikuwa na taarifa za kifo wa Chuma JPM,

alafu akamua tuu yeye kusema JPM yuko mzima. Doest it make clear sense in your head ?

Mpaka leo !?
Swali lako litajibiwa na hiyo "avatar" yako.
 
Ukitaka kupata umaarufu wa kisiasa inabidi utengeneze tatizo Kisha ulitatue. Tegemea kupigiwa makofi na kupongezwa sana
 
Nn shida Kati yenu?
Hakuna chochote zaidi ya vituko vya JF.

Kuna siku mdau akiamka vibaya analipuka na comments kama hizi.

Ukishamjua unacheka tu badala ya kukasirika au kujibu matusi.
 
Back
Top Bottom