Hukumu aliyohukumiwa na jamii kuwa ni mnajisi inatosha.

Hapo alipo haonekani hadharani hovyo na akionekana anavaa miwani nyeusi
 
Bila shaka mleta uzi ni mamluki!
 
Kwamba DPP anafanya kazi kwa kuwakomoa cdm na sio Sheria zinataka Nini. Unakwama wapi we 🌈?
 
Kama hii ni kweli basi kuna double standard kubwa sana nchi hii.

Ukiwa chama fulan hugusiki, hii si poa kabisa
Mkuu ndiyo unajua leo? Na sijui kwa nini umesema ''kama ni kweli''! Hii wengine tulishasema adhabu yake ilikuwa ni kuondolewa uwaziri tu. Hapa ndipo tulipofikia. Hakuna njia ya mkato. Bila wananchi kuamka na kukiwasha ni bure. Hii inatakiwa mara waliposema kesi imeondolewa na DDP nchi nzima ingeweka moto! Hiyo ndiyo lugha watawala wanaielewa.
 
Nawaonea huruma vijana waliongiziwa chupa aisee. Cjui ningefanyaje kama ni mwanangu. Ningemuonyesha Mimi ni mkibosho jombaa.
 
Tatizo la CDM ni kutaka kusaka sifa kila pahali na kutaka kuingiza politics kila pahala. Saa nyingine huu ujuaji unawaharibia au kuwapotezea watu haki zao. Punguzeni kiheleni heleni.
Kitu kingine ni matumizi ya matusi Kwa kila anayeonekana kutovutiwa na siasa na misimamo ya cdm.

Binafsi sidhani kama unaweza kuongeza ushawishi Kwa matumizi ya lugha zisizo na staha lakini pia Kwa kuwa na kimbelembele Kwa kila kitu.
Na Siyo kila anayeongea tofauti na cdm haipendi cdm na kwamba hawezi kuipa kura. Mfano Mimi binafsi kwenye kupiga kura Huwa sipigii chama, trend yangu ni ifuatavyo:-
1995: Lyatonga Mrema, na baada ya marudio DSM nilipiga Kwa Lipumba
2000: Lyatonga Mrema
2005: Freeman Mbowe
2010: Dr. Slaa
2015: Dr. Magufuli
2020: Dr. Magufuli
2025: Inshallah, tukijaaliwa na kukawekwa. Mtu atakayenishawishi nitampia bila kujali Chama.
 
Good point
 
Kwa hiyo baada ya Chadema kuleta siasa kwenye jambo hilo ikawa ni kikwazo kwa muathirika kupata haki yake ama unamaanisha kuwa mtuhumiwa alitumwa na Chadema ambao wako juu ya sheria mpaka kuwafanya police wasifanye kazi yao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…