Habari za jumamosi wakuu! Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, mimi nimekuwa mhanga wa tatizo hili na limekuwa la muda mrefu sana toka 2015 mpaka hivi leo nimekuwa nikikutana na tatizo hili na mara ya mwisho kunitokea ni kama week mbili zilizopita hapo nyuma.
Wengi husema ukilala chali ndio hutokea hivyo lakini kwangu sasa imekuwa sivyo tena bali hata nikilala kawaida kwa style yoyote ile, jambo hilo linaweza kunitokea. Nakumbuka kuna kipindi fulani hii hali ilizidi kwa siku ilinitokea kama mara 4 yaani usiku, asubuhi mapema majira ya sa12 ikanitokea na mchana pia nilivyolala ikanitokea, na usiku wa hiyo hiyo siku kwa kuwa nyumbani walifahamu hiyo siku tatizo lililonikuta basi usiku tulisali sana na nikabadilishiwa chumba cha kulala lakini usiku hali iliendelea vilevile.
Siku iliyofuata tulienda kwa mchungaji kwaajili ya kufanyiwa maombi lakini baada ya kufika kwa mchungaji kuna maneno alikuwa akiniambia na akiongea ambayo baadaye yalinifanya nijiulize sana maswali. Na pia kabla ya nyumbani kuchukua maamuzi ya kunipeleka kwa mchungaji, mama yangu alisema aliwahi kwenda kwa mchungaji huyo huyo kufanya maombi yake ya kawaida kama siku zote na alisema kuna siku mchungaji yule aliwahi kumwambia kuwa "una mtoto wako ambaye husumbuliwa na ndoto za ajabu wakati wa usiku...."
Hayo maombi nilifanyiwa zamani ni miaka sasa imepita ila hali hii hujirudia mara chache sana sasa nashindwa kuelewa labda huwa ina maana gani? Kwa kuwa humu JF kuna watu wengi wenye uelewa wa mambo mengi tofauti tofauti basi na uhakika naweza elewa kitu.
Asanteni! Mkawe na Sabato Njema!