Uchaguzi 2020 NEC yamuita Tundu Lissu kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Taifa

Uchaguzi 2020 NEC yamuita Tundu Lissu kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Taifa

Sasa ulitaka wajitowe mpate kupeta kirahisi ???? Hamtaki Tume huru , tumeamua kumchinja kondoo atavyoelekea . Mwaka huu tutagawana mbao au muondoke tu
Tume huru ni ya watu kutoka wapi🤔? Emb tow suggestion yako, juu ya upatikanaji wa tume huru.
 
Hahahaha, inakuwa kama ile issue ya professor Asad (siku hizi anahudumu MUM), yaani waswahili tabu sana, wanakupamba ila siku mambo yakiwa mabaya huoni hata mmoja wa kuja kukusaidia. Lisu naweza sema uwezo wake wa kufikiri umeathirika sana, yaani anaishi kwenye buble, yaani Tanzania haijui na bado watanzania hawajui, hakuna hata mtu mmoja aliyenaye bega kwa bega, ila ni ushabiki tu wa kumsukuma mbele ili wapate pa kutokea wale wenye nia ovu, na mwisho wa siku ngoma anaicheza peke yake. Probably ataenguliwa kugombea na kushitakiwa

Hivi nyie hamchoki kuzungumza ujinga? Hivi Hivi mlisema hatarudi, mara hatateuliwa kugombea Urais.. maneno meeengi ya kichawi. Aibu yenu.

Jiandaeni kwa Tundu Lissu kuwa Rais wa nchi hii mapema sana tarehe 29 October 2020.
 
zile ndo sheria sister, ndo maaana wanasema fanyeni kampeni za kistarabu, ukifanya kampeni unatakiwa uwe na adabu pia! tumia lugha nzuri kunadi sera zako na pia jitahidi kushawishi wananchi kwa uwezo wako wote ukitumia staha

sasa jamaa ana mdomo mchafu alafu anajiona kama ndo anajua sheria peke yake nchi nzima, ona yanayomkuta sasa, aende kujibu nec, akimaliza akikosa uraisi kuna kesi znamsubiri, kule wananchi wanataka kumpiga mawe uku kwingine wasiojulikana wanamweka target
Kila wanachofanya NEC NA CCM WANAMPA MAILAGE Myampaa kwani amesema nn cha uongo au m
 
Ni balaa wewe ukiona Mkurugenzi wa Nec anasema anataka mgombea anayenadi kuboresha afya.. barabara n.k ujue hakuna kitu hapo
 
Amezidisha uongo acha aitwe na mnaotetea uongo sawa kwa kuwa ndo manufaa yenu Ila haiwezekan umma uhadaiwe
 
Lissu kwenye hicho kikao, watanzania tunakuomba utusemee kwa NEC, wapiga kura tunataka Mdahalo wa wagombea wote wa Urais. Uitishwe na tume.
 
Tundu hawajui watanzania, wafuasi wake ni zaidi ya wajumbe maana heri wajumbe wanapiga kura hao wa Tundu wanakaa nyuma ya keyboard kumjaza, wachache wanaenda kumtazama na wakati huohuo asilimia kubwa hawana hata vikatio
2810
Mapambio ya kanga hayo lissu anawapiga kura wengi 18 hadi 35 magufuli kakanwa na wazee vijana na rika la kaTi kabaki na wanafunzi wa msingi na sekondari ndio maana yeye na mkurugenzi wa. Uchaguzi wamepanic wanapumulia ju juu
 
Hahahaha, inakuwa kama ile issue ya professor Asad (siku hizi anahudumu MUM), yaani waswahili tabu sana, wanakupamba ila siku mambo yakiwa mabaya huoni hata mmoja wa kuja kukusaidia...
Magufuli kajithibitishia alikuwa anapambwa kama ntukufu ndani ya mwezi tu watanzania wanamwona zimwi hawataki hata kumsikia analazimisha wanafunzi. Watoto. Professor Assad taifa kubwa yule
 
Mabibi na mabwana ni muhimu Tume ikakumbuka kuwa wagombea ni wa wananchi si wa Tume.

Mengi yamevumiliwa lakini hayatavumiliwa yote.

Tumesikia wito usiothibitishwa kuwa mgombea mmoja kujieleza kwenu.

Maneno mawili kwenu, "tunakoelekea siko."

Tumecheza ngoma za chama kimoja muda wote. Kanuni na vizingiti vipya kila wakati vinachipuka kama uyoga.

Acheni kutumika.

Lissu mkimtaka Dodoma tutakuja naye kwa mamilioni.

Andaeni ofisi ya kutupokea wote.

Wanaoongea kikabila, wanaoita wenzao majina, wanaochochea fujo dhidi ya wagombea nk hamuwaoni?

Hivi unapo mhukumu mtu jukwaani kuwa ni kibaraka wa mabeberu hakumuweki mtu huyu hatarini vilivyo?

Tume mjue tumrchoka kweli kweli.

Haki yetu na uhuru wetu viko wapi?

Waacheni wagombea. Wagombea si wenu. Hawa ni wetu. Tuacheni tuwachambue sisi kwani wapiga kura ni sisi.
 
Tume huru ni ya watu kutoka wapi🤔? Emb tow suggestion yako, juu ya upatikanaji wa tume huru.


Kumbe hata huru hujui maana yake ??? Muulize Jecha aliyechukua fomu za kugombea uraisi kupitia CCM , atakuambia

Ni kama mnacheza mechi , Yanga na Simba halafu Simba itoe mchezaji wake ndio awe Referee wa mechi , umeona wapi mambo hayo ???
 
Back
Top Bottom