Uchaguzi 2020 NEC yamuita Tundu Lissu kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Taifa

Uchaguzi 2020 NEC yamuita Tundu Lissu kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Taifa

..siyo kweli.

..mfumo wetu wa uchaguzi, pamoja na tume, ni taabu tupu.

..wagombea wengi wa vyama vya siasa wameenguliwa kwasababu za hovyo-hovyo.

..kuna jimbo kama Misugwi mgombea ubunge, na wagombea udiwani wote wa cdm, wameenguliwa.

..tusijenge mazingira wananchi wakakosa imani na demokrasia yetu.

..vyama vya upinzani vinajitahidi.
Niambie usio ukweli kuhusu sacos ya ukoo wa Mbowe. 50 million imepotea kimazingaobwe wacheni hizo.
 
Utopolo wenu hawezi kujibu hayo madai kwani!? Awaambie wananchi huyo mayanga ni nani na alipata vipi tenda ya ujenzi. Au pesa za kodi kazigeuza kuwa zake!? Au ndio ule mwendelezo wa upigaji kama walivyowagawia mahawara nyumba za serikali! Bado haijasahaulika hiyo.
Hahaha nadhani hoja zimeanza kupunguza tehteh....awamu ya pili ya kampeni za CCMinayoanza kesho itakuwa mbaya Sana kwa Chadema...stay tuned
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imemuandikia barua mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ya kumuita katika kikao cha kamati ya maadili ya Taifa.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Charles Mahera amesema hilo leo jijini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa mgombea huyo atafika mbele ya kamati Septemba 29 mwaka huu.

Akizungumzia uratibu na usimamizi wa kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 mwaka huu amesema tume imekumbana na changamoto kwa baadhi ya wagombea wa kiti cha Rais kutoheshimu sheria, taratibu na maadili ya uchaguzi.

Ameongeza kuwa baadhi ya wagombea wamekuwa wakitumia maneno ya kukashifu wagombea wenzao, tume, pamoja na kutoa taarifa zisizo za kweli zenye lengo la kuleta taharuki na uzushi miongoni mwa Watanzania.

Chanzo: TBC Online
duu hapa kuna jambo!
 
Huyu Mkurugenzi Charles Mahera tunajuwa namna alivyopata hii nafasi ya Ukurugenzi wa NEC kwa upendeleo ili aje atumike kumptisha Magufuli akishindwa au atengeneze mazingira ya Magufuli kushinda.

Haiingii akilini kwa kutomuandikia Magufuli kwa vitendo vya wazi wazi anavyovifanya kwenye mikutano ya Kampeni hasa anapotoa maagizo kwa TANROADS kujenga mababara.

Nitoe onyo tu, Mahera akumbuke ana familia inayomtegemea, akimfumbia macho Magufuli na kukubali maagizo anayompa itamgharimu yeye na kizazi chake. Mwaka huu CHADEMA hatuibiwi!!!
Acha vitisho dogo.
 
  • Thanks
Reactions: Ole
Usidanganye watu JF, Hivi posta na huyo huyo mwanamama ndio Tume ya Uchaguzi ya Marekani ?? Unapakazia kama uko maskani ya ;Lumumba ukiwakaranga makada wako ??

Mkuu, hivi wakisikiliza unachoongea?

Sasa hawa wote si wanashirikiana na tume ya uchaguzi?

Tume ya uchaguzi si itawasiliana na posta.

Na kama kuna "disputes" si jaji atataka taarifa kutoka tume ya uchaguzi?
 
Ukweli tuuseme tu , katika pita pita zangu chadema inakubalika, nimehudhuria mkutano wa lissu mmoja kweli sio matusi wala nini yaani automatically wananchi wameumizwa na CCM, malalamiko ni mengi mno yanayo husu unyanyasaji wa serikali ya ccm kwa raia, lissu wala hatukani kwenye mikutano yake anakubalika tu , labda cha kuishauri NEC iachane na mambo ambayo hayana tija , iache mpambano uendelee.

Kwa lissu, ajaribu kuwaambia Hao watu wasibweteke waende kupiga kura siku yenyewe, ajitahidi kuwaambia wawahi na wawe wavumilivu kushinda kwenye mstari bila kuchoka ili wapige kura , ni kweli watu ni wengi sana katika mikutano yake.

Kwa ccm , acheni fujo, shindaneni kwa hoja sio kujificha kwenye mgonga wa matusi na NEC.
 
Ukweli tuuseme tu , katika pita pita zangu chadema inakubalika, nimehudhuria mkutano wa lissu mmoja kweli sio mature wala nini yaani automatically wananchi wameumizwa na CCM, malalamiko ni mengi mno yanayo husu unyanyasaji wa serikali ya ccm kwa raia, lissu wala hatukani kwenye mikutano yake anakubalika tu , labda cha kuishauri NEC iachane na mambo ambayo hayana tija , iache mpambano uendelee.

Kwa lissu, ajaribu kuwaambia Hao watu wasibweteke waende kupiga kura siku yenyewe, ajitahidi kuwaambia wawahi na wawe wavumilivu kushinda kwenye mstari bila kuchoka ili wapige kura , ni kweli watu ni wengi sana katika mikutano yake.

Kwa ccm , acheni fujo, shindaneni kwa hoja sio kujificha kwenye mgonga wa matusi na NEC.
Lazima akijieleze mnapoteza muda bure!
 
Dadeki. The fall of Ccm is now so obvious!

Kweli hakuna marefu yasiyo na ncha. Kuanguka kwa Ccm kumeshafika.Hatimaye NEC wanaongeza zaidi kura za Lissu 😂😂😂

Sasa kichwa Tundu Antiphas Lissu kinaenda kutoa hoja hadi NEC wanapoteana.

Na wajaribu kumkata waone. TukoTayari kugawana majengo ya serikali mwaka huu!!
 
Back
Top Bottom