Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 30,742
- 56,070
Uzoefu wako wa kisiasa not equivalent to matokeo.Uzoefu wa siasa niliona ni mkubwa, miaka 30 nipo kwenye haya masuala ninayajua vilivyo.
Hizi harshtags zisikudanganye, unapokuja uchaguzi halisia hutamuona hata mmoja katika haws wanaoshinda wakiandika hizi slogans.
Waarabu wa tahrir square na watanzania ni watu wa aina mbili tofauti.Uzoefu wako wa kisiasa not equivalent to matokeo.
Mambo yamebadilika na vizazi vinabadilika, waliozaliwa 1960s mpaka 90s ndio ulikuwa mtaji mkubwa wa ccm, kwa hizi enzi za digitali mambo ni tofauti
2011, misri,tahrir square kulitokea mapinduz makubwa
Player mkubwa behind the scene ni social media, imekuwaje? Je lingewezekana kwa vizaz vya zamani? Sidhan
Now sisemi hashtag zitapeta kura, ila ni moja ya vyombo vinavyoweza ku mobilize kizaz cha sasa ni social media
Naona umehamia kwenye udini, punguza hisia, hakuna mahali nimetaja uislam. Or kushambulia diniWaarabu wa tahrir square na watanzania ni watu wa aina mbili tofauti.
Mnaongozwa na chuki za kijinga dhidi ya uislam wa Samia lakini bahati nzuri mpo wachache sana na mwanzo pamoja na mwisho wenu ni humu humu mitandaoni.
Mnaopiga makelele licha ya kutumia nguvu ya chuki ya dini ya mheshimiwa, mpo wachache sana hamzidi watu milioni mbili.Naona umehamia kwenye udini, punguza hisia, hakuna mahali nimetaja uislam. Or kushambulia dini
Wala hii mada si ya dini, ni mada inayozungumzia yanaondelea
Tunazungumzia facts hapa
Yes waarabu ni tofauti na watanzania, nitakupa pia mfano mwingine, bangladesh, social media ilitumika sana ku mobilize vijana hatimae wakapindua na serikal yenyewe
Yes kila jamii ni tofauti lakini, vyote huwa viko related by common interest , unequal treatment na serikal zao.
Huwa haiji siku moja, ni progressive, baada ina reach peak.
Kwa hiyo umetoka kwenye facts na hoja umeanza kunijumuisha kwenye makundi? 😂Mnaopiga makelele licha ya kutumia nguvu ya chuki ya dini ya mheshimiwa, mpo wachache sana hamzidi watu milioni mbili.
CCM wanao wanachama milioni 13.5 kwa takwimu za 2020 sijaongelea takwimu za muda huu. Pia kumbukeni kuwa daftari la wapiga kura limeshaboreshwa tangu mwezi March mwaka huu, mnapoteza muda.
Tatizo la ujana wenu ni kushindwa kuwa na busara za kupanga mipango yenye kutazama mbali.
October 2025 kapigeni kura hii mihemko haiwezi kupatiwa utatuzi kwa hizi slogans za JF na instagram.Kwa hiyo umetoka kwenye facts na hoja umeanza kunijumuisha kwenye makundi? 😂
Na ngonjera za vyama juu?
Kaka you are better than that
Dont go low like that
Waandikie wahusika kaka, sipo kwenye hayo makundiOctober 2025 kapigeni kura hii mihemko haiwezi kupatiwa utatuzi kwa hizi slogans za JF na instagram.
Utarudiarudia haya mara ngapi. Kumbuka, kamba inazidi kukaza!Laana mnayo nyinyi wanaharakati mnaoibuka mwaka wa uchaguzi na kuongea vitu ambavyo hamna uhakika navyo.
Kila mradi alioucha JPM muda huu kama haumaliziki upo katika hatua za mwishoni, Nyinyi ni mashujaa wa nyuma ya keyboard bendera hufuata upepo.
Mapambano yenu yanaanza na kuishia kwenye laptop na simu zenu.
Hiyo kura unayohimiza wewe; hata kwenye mazingira ovu yaliyopo, nayo imeanza kuwa tete kwenu. Samia hata kwenye hali hii, bila ya marekebisho ya taratibu; kuiba kura na kulazimisha kubaki madarakani sasa kunaanza kufifia.October 2025 kapigeni kura hii mihemko haiwezi kupatiwa utatuzi kwa hizi slogans za JF na instagram.
Unarudia yale yale, toka uingie JF!Utekaji upo kabla hata Samia hajaingia ikulu, upo tangu awamu ya Nyerere na Mkapa. Ni suala linalotisha lakini halina uhusiano wa moja kwa moja na siasa za nchi, zipo sababu nyingi za watu kuuana na kutekana.
Huna ushahidi wa rasilimali za nchi kugawiwa kwa watu wachache, msingi wa maneno hayo ni chuki dhidi ya uislam na jinsia ya Samia, hakuna ukweli wowote kwenye huo upuuzi.
Hakuna mtu anayegawa rasilimali bure, makampuni makubwa yanashinda tender kwa uwezo wa ufanisi yanayokuwa nayo sio kwa vigezo vya kipuuzi vya asili yao.
DP World alishinda tender bandarini kwa ukubwa wa kampuni yao na kwa maslahi mapana ya kibiashara ya ukanda huu mzima, haya kuyaelewa mpaka uwe na upeo mpana na usiwe mmoja wa wale wanaochagua upande wa chuki za kijinga za mitandaoni.
Aje mwarabu kufanya biashara kwenye eneo ambalo sisi hatuna utaalam nalo au tuendelee kubakia na umaskini ule ule?.
Samia asingetafuta uwekezaji bado sisi wapiga kelele tungeendelea kulalamika kwamba hajafanya lolote, wenye upeo mdogo kama nyinyi mnasomwa mitandaoni na mnapuuzwa tu.
Watu wa Mitandaoni wanaishi wapi?Wanasemaga kura haziko mitandaoni
NRNENguvu ya jambo lolote katika kuamua, ni uwingi wa waamuzi wenyewe
Na ndiyo maana, kura nyingi, humpa mtu nguvu ya kuwa mshindi na kutawazwa kuwa kiongozi
Tunaona, hata miswaada mingi kwenye mabunge, huamriwa na nguvu ya hoja na kuungwa mkono na watu wengi ndipo inapita, na ikishindikana hivo, huitishwa kura za ki CCM za ndiyo au hapana, na pale sauti ya wengi itakaposikika, jambo hilo huamriwa kwa nguvu ya sauti hiyo
Tukirudi sasa kwa mambo yanayoendelea nchini na yale yaliyoko katika uso wa Tanzania na Watanzania
Tunaelekea kipindi mhimu sana kama nchi, ni mhimu kwa sababu ya tukio lenyewe
Uchaguzi kupata viongozi wazuri, na watakaoipeleka nchi yetu mbele
Wakati tukielekea kipindi hiko, Kama Taifa huru, linavyo vyama vinavyotegemea kuingia kwenye hatua hii mhimu ya uchaguzi
Hata hivyo, yapo mambo ambayo ni madai mhimu sana kwa vyama hususani Chadema chama kikuu cha upinzani
Madai haya na jinsi yanavyoungwa mkono kwa mamilioni ya Watanzania, ndiyo yanawapa watafiti kuangalia uhalisia sasa wa madai yao na kwamba, Chadema kimekuwa kikidai mara zote kuwa, CCM wamekuwa wakiiba kura ili wao kuendelea kukaa madarakani
Na kwa sababu hiyo, Chadema kimeadhimia, hakitaingia kwenye uchaguzi bila ya madai yake kufanyiwa marekebisho (REFORMS)
Kwa nguvu iliyopo mitandaon, kinaipa nguvu Chadema na kuwaamisha Watanzania kwa ujumla kwamba, ni kweli CCM hutumia janja janja kwenye chaguzi zote nchini
Kwa nguvu na uwingi wa wanaounga mkono hoja ya no reforms no election, ni kiashiria cha kweli kabisa, ccm huiba kura
Watanzania tuamke, Tanzania inaamriwa na Watanzania na siyo CCM
Kataa kwa nguvu zote mateso ya CCM
No reforms no election!
Asingekuwa na uwezo asingeweza kumalizia miradi karibu yote aliyoachiwa na JPM.Unarudia yale yale, toka uingie JF!
Hilo halitamsalimisha Samia Suluhu Hassan, mtawala ambaye hana uwezo wa uongozi wa nchi.
Alichoweza kufanya ni kuruhusu GENGE lenu kukiteka chama cha CCM na kukitumia kufanya kila aina ya uchafu ndani ya nchi hii.
Sasa waTanzania wanasema, INATOSHA.
Aibe kura kwa sababu zipi wakati kaweza kutimiza kilichoandikwa kwenye ilani ya 2020?.Hiyo kura unayohimiza wewe; hata kwenye mazingira ovu yaliyopo, nayo imeanza kuwa tete kwenu. Samia hata kwenye hali hii, bila ya marekebisho ya taratibu; kuiba kura na kulazimisha kubaki madarakani sasa kunaanza kufifia.
Kamba inawakazia nyinyi wapiga kelele wa mitandaoni.Utarudiarudia haya mara ngapi. Kumbuka, kamba inazidi kukaza!
Kilichobaki kwa Samia kuwashangaza waTanzania, ni kung'ang'ania kubaki madarakani baada ya waTanzania kumkataa!Aibe kura kwa sababu zipi wakati kaweza kutimiza kilichoandikwa kwenye ilani ya 2020?.
Samia atawashangaza mashujaa wa nyuma ya keyboard kina Kalamu, ikifika October 2025.
Acha tuwe wapiga kelele; kwani tunajuwa kelele zinawasumbua sana toka mlipoingia kwenye utawala.Kamba inawakazia nyinyi wapiga kelele wa mitandaoni.
Hakuna mwananchi anayetumia SGR muda huu anaweza kumkataa Samia.Kilichobaki kwa Samia kuwashangaza waTanzania, ni kung'ang'ania kubaki madarakani baada ya waTanzania kumkataa!
Hili litamsababishia matatizo makubwa kama yaliyompata yule mama wa Bangladesh miezi kadhaa ilyopita.
Samia anajiandalia njia ileile iliyomkumba mama Sheikh.
Utaumia sana mkuu Kalamu Samia akiendelea kuwa Rais wa TZ baada ya 2025, pole nakupa mapema kabisa.Acha tuwe wapiga kelele; kwani tunajuwa kelele zinawasumbua sana toka mlipoingia kwenye utawala.
Kelele hizo hizo zimewafikisha hapa mlipofikia sasa, licha ya kufanya ulaghai mwingi na kuonyesha kila aina ya hadaa.
Sasa saa yenu imewadia. Hakuna njia tena ya kujinusuru.