Ni wimbo gani unaoutafuta sana bila mafanikio?
Wakuu kuna nyimbo 1 ya jamaa wa kenya anaitwa Lenny km sjakosea, chorus yake ni "sasa bebigal, sio kamdigida nataka nikutach, nimekutafuta kwa shidaa sio kamdigida nataka nikutach"

Nna miaka zaid ya 5 nausaka huu wimbo bila mafanikio

Cc KIOO
Mku KIOO tusaidie bas kaka,
Baby Gal wa King Lenny
 
Jaribu kusikiliza huu kama ni wenyewe.
Cc @Mwamba028
Ndio wenyewe aisee Mkuu, ubarikiwe sana.

Yaan kama King Lenny alivyomtafuta kwa shida mwana Mombasa Anisa akaja kumpata baadae ndio nami nilivuoutafuta sana kwa shida huu wimbo na sasa nimeupata.

Ahsante sana ubarikiwe, pamoja na mleta uzi.

NB
Mitandao mingi sijui ni ya Gen-Z? Manake walikua wakiniletea Baby Gal ya Mad Ice
 
Mkuu Idimi unaokoa sana jahazi,

Kuna Wimbo wa kitambo sana, unaimba WAHAYA NA WAKURYA NI WATANI WA JADI,
WANAPOKUTANA NI MINGURUMO YA RADI, nimesahau muimbaji ila anatumia lafudhi ya Kihaya au Kisukuma hivi
 
Wakuu saidieni pia wimbo wa Inspector Harun wa MAISHA UTATA, kwenye Chorus kasimama Nature Kiroboto
 
Wakuu saidieni pia wimbo wa Inspector Harun wa MAISHA UTATA, kwenye Chorus kasimama Nature Kiroboto
Au unamaanisha maisha ya uswazi? Maana sijawahi kusikia jina la huo wimbo!
 
Poleni wana jamii forum

Binafsi natafuta wimbo sina uhakika na jina lakini nahisi unaitwa Bukoba Rap au Wahaya rap.

Unaanza jamaa kwenye intro anaongea then anasema Anko T

Kisha kwenye baadhi ya mistari anaelezea alivyotoka bukoba kuja Dar na ndugu zake kumpokea anasema "everybody say nyegera" hustle za kuishi Dar uku akiwa ajui kiswahili anawataja baadhi ya waliompokea Dar mfano Muganyizi na somebody Rumanyika waliokuwa maeneo mbalimbali Dar

Mbele anaendelea kueleza alivyopitia magum mpaka kuja kuimba Rap

Baadae mwishoni anasema "huwezi amin now na present Fani"

Ameimba kuchanganya kiswahili na kihaya pia kingereza kama ilivyo hulka ya Wahaya.

Nilikuwa mimi nimeisave Bukoba Rap nilikuwa nao kwenye external yangu ilianguka ikaharibuka toka hapo sijawahi kuusikia tena
 
Natafuta rap moja imeimbwa kinyaturu sijui mwimbaji ni nani. Ni ya zamani
 
Wakuu natafuta nyimbo za bendi ya Mapacha Classic ya Jose Mara. (Baada ya kujiondoa Mapacha Watatu)
 
Natafuta wimbo,msanii wa kike anayetokea tht anaimba kwa lafudhi ya kisukuma wa zamani chorus "ae ae ae ae".
 
Back
Top Bottom