Si tuliambiwa isra huwahawajadiliani na magaidiIsrael imehtukizwa na kupewa kichapo cha 5-1 ndani ya masaa 24. Inshort intelijensia yao haikungamua uwepo wa mashambulizi haya. Hata mataifa makubwa awakutegemea kusikia kilichotokea.
Kwa kichapo kilichotokea maana yake Dunia haipo salama dhidi ya mashambulizi ya kulipiza kisasa. Ni ishara kwamba dola zote duniani zinapaswa kuanza kutathimini hali za amani kwenye maeneo yao.
Ugaidi siyo jambo linalotumia miaka kufanyika ila utumia sekunde kuvuruga nchi. Israel imevamiwa, ofcos watalipa kisasi kwa kuwaua raia lakini lazima wapo watu watawajibishwa kwa kutotimiza wajibu wao.
Kibaya zaidi ni kwamba wanajeshi na Raia wa Israel wamechukuliwa mateka. Kuchukua Raia na wanajeshi mateka kunaihakikishia Palestina ushindi kwani wanaweza kutumia mateka kumfanya Israel arudishe mashambulizi nyuma.
Suala ili lina muunganiko na imani hasa huku Afrika na Tanzania. Je ndani ya Imani unaamini kati ya Israel na Palestina nani achapwe? Katika tafakuri ya wazi unaamini nani mchokozi kati ya mataifa haya mawili?
Mwisho; Tanzania tukawatoe watu wetu kwenye mataifa haya mapema.l