Mwalimu P,
Tumsifu Yesu Kristo!
Milele Amina,
kwanza nakushukuru kwa kuunga mkono yale yaliyokupendeza,
lakini pia niwie sana radhi kwa yale ambayo binafsi naamini ni ya kweli ila yamekukwaza au kukukera wewe na pengine wadau wengine wa jf, kwa namna moja ama nyingine, ingawa najua wazi sababu ya pekee ya kwanini umekereka.
Asante, ni kweli nimekereka, lakini kwa jinsi ulivyojibu kwa heshima na unyenyekevu, moyo wangu umesajishika, kimebaki kitu kimoja tuu cha mwisho ni kukupiga darasa na wewe, kuwa Kanisa Katoliki, linaongozwa na watu ambao ni binadamu, sasa hawa viongozi wakitenda ndivyo sivyo, wabebeshe misalaba yao, tusichafue kanisa Katoliki kwa makosa ya Padri fulani, Paroko fulani au Askofu fulani!
Tatu na mwisho nakushukuru sana kwa ushauri mjurabu sana wa jumla dhidi yangu binafsi, na pengine wadau wote wa jf, wenye maoni au mtazamo kama wangu dhidi ya mchango wa kanisa Katoliki katika kuchochea aina ya siasa zinazoendelea Tanzania.
Naomba tusiite kuchochea, bali Kanisa Katoliki ni kanisa la ukweli linasimama na kweli, likiona mambo ya hovyo yanayofanywa na utawala, haliwezi kunyamaza, lazima lisimame na likemee.
Mwalimu P,
Naomaba kuuliza swali,
hivi ni nani aliwakutanisha Tundu Lisu na Freema Mbowe ndani ya majengo ya kanisa katoliki wakati ule wa vuguvugu la kuelekea uchaguzi wa ndani ya chadema, haswa joto lilipopanda kwenye nafasi ya mwenyekiti wa chadema taifa?
Naomba kukiri, hili sikuwahi kulijua.
Kwanini kiongozi huyo wa TEC kwa niaba ya kanisa Katoliki aliingila kati masuala ya siasa tena za Chadema na asithubutu kabisa kuchukua hatua kama hiyo na kuingilia kati masuala ya kisiasa ndani ya vyama vingine vya siasa nchini, ikiwa hakua na nia au dhamira ya kuitumia Chadema kujaribu kumuhadaa kiongozi mojawapo wa Chadema na kumsaidia aliemkusudia ili hatiamae amtumie katika kupitisha agenda zake za siri na pengine agenda za kanisa katoliki, kwasababu mazungumzo yao yalifanyika ndani ya majengo ya kanisa Katoliki?
Kanisa katoliki halijihusishi na siasa za vyama wala halina agenda zozote za siri
Tukisema,
huyo kiongozi wa kanisa katoliki alikua anakusudia kumuhujumu yule kiongozi wa Chadema ambae hakutaka awe mwenyekiti wa Chadema taifa, na in fact alifanikiwa kumuangusha,
na sasa anafanya tu muendelezo wa kupitisha agenda alizokusudia kuzitekeleza kwa naiba ya kanisa Katoliki kupitia mgongo wa Chadema tutakua tunamuonea au tunamsingizia kiongozi huyo wa kanisa Katoliki?
Not necessarily , kama nilivyosema, japo ni kanisa la Mungu, linaongozwa na viongozi ambao ni binadamu, pia ni kweli kuna wakati wanakuwa ni ma exremist, hata sisi walei wengine, tukiona its too much, tuna kemea,
Mpeni Mungu yaliyo ya Kimungu na Kaisari yaliyo ya Kaisari! Hiki kinachofanywa na Baraza la Maaskofu Katoliki, sio kuchanganya dini na siasa?
Je,
tabia hii ya kiongozi huyo wa kanisa katoliki haikua miongoni mwa mambo yaliyowakasirisha baadhi ya walei wa kanisa katoliki na kuwachochea wakafanya maandamano ya kumkataa hadi ubalozi wa vatikani?
Wale Wakatoliki wa vijora, achana nao, ile ilikuwa movie, ikakosa cast sahihi hivyo ika flop!.
Je,
Ni mtaalamu gani wa sayansi ya siasa asie jua kwamba ziara ya kichungaji iliyokwamia nje ya gereza ya Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida Muhashamu Edward Mapunda katika Gereza la Ukonga ni script ya kiongozi huyo wa TEC kwa niaba ya kanisaKatoliki?
Askofu wa Jimbo, Paroko, Padri au waumini, wana wajibu wa kuwatembelea waumini wao majumbani, mahospitali na magereza, si vema kuwazuia. Natamani watokee wenye busara wamashauri Mama, asifanye mzaha kabisa na Kanisa Katoliki!, hivi tuu kile alichofanywiwa yule muumini wetu, kingewaka, lakini kwa vile aliyemfuatia pia ni Mkatoliki, hiyo ndio salama yake, vinginevyo...!
Nadhani kuhusika kwa kanisa Katoliki Tanzania miongoni mwa mambo ya kisiasa yanyoendelea, kupo wazi sana na sidhani kunahitajika hata uthibitisho kwasababu hakujifichi.
kwa maoni yangu,
chemistry ya kimtazamo, ukabila, udini na urika wa kiongozi mkuu wa Chadema taifa na kiongozi yule wa TEC kwa niaba ya kanisa Katoliki una vinasaba vya yaliyotokea oct.2029, lakini pia yanayoendelea hivi sasa politically speaking.
Not necessarily, japo kwa vile yule ni Msingida, na Msingida ndipo uzushi wa ukabila unaletwa. Mimi nimefanya nae mahojiano na hilo la kuchanganya dini na siasa, nililiuliza
View: https://youtu.be/_iDRrF9NqwA?si=Xd7tQHkL1UhWRJE8
Mwalimu P,
kwa heshima, adabu na utii wangu kwako kama mwalimu,muandishi, mzazi, baba, kaka na pengine mjomba wa wadau wengi sana humu jukwaani, tafadhali niwie radhi.
Sikustahili kureply comment yako, ila kwasababu za mshawasha wa juu sana wa kisiasa nilio nao kwasasa, nimeona nisikae kimya, nijieleze walau kwa swali nililouliza hapo juu, but nadhani utakapo reply maelezo haya, kwa heshima ya kiwango kilekile ninachokuheshimu, nitagwaya kukujibu tena, but nitaendelea kudeal na hawa wavamizi na vibwengo wa siasa swiftly and softly bila kuchoka, kuogopa wala kukata tamaa, kwasababu wengi ni saizi yangu halafu nawamudu vizuri tu.
I'm sorry for saying all that Mwalimu P.
Mungu Ibariki Tanzania
Ubarikiwe.
P