Orodha ya vitu kadhaa ambavyo Wewe Mwanaume Mkeo hapaswi kujua kabisa kuhusu Wewe

Naunga mkono hoja
Napingana na hoja, labda side hustles ndio unaeeza kumficha.
Hii inafanana na namba mbili. Side hustles ndizo mke hapazwi kujua
Napinga hoja. Kabla ya kuoana kila mmoja aweke wazi kama ana mtoto/watoto. Na kuoa/kuolewa halafu kuzaa nje huo ni upumbavu
5. Idadi ya Assets ulizonazo.
Umejenga Assets ngapi, nyumba, maduka, na Assets zingine mashamba and so on, kuwe na mipaka ya Assets anazozijua baadhi Mkeo hapaswi kujua fanya mwenyewe sio kila kitu unamwambia Mkeo, Mkeo hapaswi kujua. Nimekusanua.
Naunga mkono hoja na katika hili ni muhimu kuwe na mtu wako wa karibu anaezijua hizo assets, in case of suddenly death mzigo usipotee. Asset anayotakiwa kuijua mke ni nyumba mnaylishi tu
Naunga mkono hoja. Mkeo anatakiwa kujua tu una maex lakini hatakiwi kujua ni wa kina nani
 
Sasa wewe maskini Una kitu gani cha maana Sana cha kumficha mkeo, kwenye mshahara hapo sawa lakini hayo mengine ni ujinga na utoto. Assets zenyewe ndo hizi hizi nyumba na viwanja vyenye hatua 15x20 vilivyo nje ya mji au kuna vingine kibongo bongo!!!?πŸ˜€
 
mwanaume ni mtawala kwenye ndoa hakuna 50-50...Kama mtawala nina haki ya kujua hali ya yule ninayemtawala ila yeye hawezi kuwa na uwezo wa kunichunguza.

Mwanaume ni mchungaji wa mkewe na wanawe
Mambo ya utawala ndio yana anzishaga vita. Ukishaanza kumficha mkeo details zako. Fahamu kwamba umefungua mlango wa yeye kukuficha details zake.

Na hapo muda si mrefu, ugomvi utaanza na mnaweza kuachana.
 
Msimshambulie mtoa mada, ana reasoning logic. Kuna wanawake washenzi waliingia ndoani kwa matamanio ya fedha na mali. Ukimuambia siri zote utavuruga ndoa, let say umemuonesha salary slip akajua mshahara unaopokea, siku ukileta mshahara pungufu nyumbani atahoji hela zingine zimeenda wapi, varangati litaanza. Ukimuambia una mtoto/watoto nje ya ndoa ataona unajali sana watoto wa nje kuliko wa ndani utanuniwa na kuambiwa nenda kwa hao wanawake wa nje. Kwenye mali nako ukimuambia halafu ndoa ikaja kuvunjika atataka hizo mali mgawane paso kwa paso hata kama zingine alizikuta
 
Once unataka kuoa ni bora kuelezana hali zenu za mahusiano kabla hamja engage katika kuunda ndoa. Kama kuna watoto msifichane, sema tu nina mtoto/watoto ili isije kuleta utata ndoani. Kuna wanaume hubeba wanawake wakifichwa kuwa hawana watoto kumbe watoto wapo kwa bibi, jamaa anabeba anaenda kuzaa naye watoto wapya, inakuja kutokea mwanamke ana watoto wengine wako kwao kwa bibi yao. We baba utaishije na huyo mwanamke mwenye watoto debe? Je utawabagua watoto wa mke wako watakapokuja kutaka mahijaji kwa mama yao? Mind kuwa kwa bibi ni choka mbaya itabidi wahamie kwa mama yao kuliko na maisha mazuri milo mitatu kama dozi kwa siku. Unasomesha watoto wako shule ghali za magari ya njano, je watoto wa mke wako watasoma kayumba hapo kwako?
 
Kuna mtu kashukiwa na kitu kizito huko ndio maana nawapa angalizo mtakao niona mimi ni km fala fulani hivi ila kwa alienielewa amenielewa, usithubutu kumwambia mkeo kwamba una basha wako hua anakutatua Malinda na Ndoa imeishia hapo
Hiki ndio ulochotaka kumalizia au kuna kinginee??
 
Hali ya ndoa itakuwa mbaya zaidi ikiwa vice versa. Mwanamke naye akificha mambo yake hiyo ndoa itakuwa ni kituko na itakumbwa na mlipuko mkubwa wa kuvunjika na kusambaratika kama mwanaume atakuwa na akili timamu na ana uwezo. Mwanaume mburula/zoba anaweza kuishi na mwanamke mshenzi anayeficha mali zake/anajenga kwao kwa siri, ana biashara zake kwao, hujui anapokea mshahara kiasi, ana mkopo benki kiasi gani. Ndoa za kishenzi huwa hazidumu mpaka mwisho wa uhai
 
Mbona uko nje ya mada kabisaa. Lol
 
5.

Nyie ndio mnaokufa halafu mmeacha magofu yenu hakuna anayejua kuwa zilikuwa mali zenu...matokeo yake wanarithi watu baki... Utasikia hii nyumba mwenyewe hajaonekana mwaka wa 20 sasa...kumbe ulishakufa miaka 18 iliyopita
Hili nimeshalitolea ufafanuzi kwa umakini mkubwa huko juu nimeulizwa sana nikalitolea ufafanuzi soma vizuri mkuu,
 
Hapana sio kweli, nitakuuliza swali anaemuoa mwenzie ni nani ni weww au ni mkeo au mnaoana? Nipe jibu nikupe swali lingine, halafu nataka twende taratibu katika hili ili tufike sehemu tuelewane vizuri, maana tukienda haraka hatuwezi kuelewana
 
Kazi zingine zinafahamika na huwezi zificha mfano mwalimu πŸ˜€πŸ˜†
 
Hii story inataka kufanana na mtu fulani, ila yeye hakuwahi kuwa nje ya nchi, na huo mwaka 2009 alikua hapa hapa Bongo.

Duuuh poleee sana aiseeee.
 
Hakuna MTU wa karibu zaidi ya MTU uliooana naye Kwa hizi Siri zako haziendani na misingi ya ndoa
Upo sahihi kabisa mkuu,

Nimesema hivi hapaswi kujua km unakataa basi wewe mjulishe, mjulishe password zako zote unazozitumia, mjulishe kila kitu kuhusu wewe mjulishe mjulishe mjulishe kuna sehemu utafika utagundua kwanini nilikwambia usimjulishe na hapaswi kujua au hakupaswa kujua sababu ya protection yako na yake unamlinda, unajilinda na una linda ndoa yako, kwa maana mlinzi namba moja ndani ya nyumba yako ni wewe na sio Mkeo, hajakuoa wewe ndie umemuoa, umemlipia mahari ukamtoa kwao ukaenda kuishi nae kwenye mji wako, yeye anakuangalia wewe km Mume, elewa ninaposema km Mumewe namaanisha nini hapa kuna la kujifunza Mume ni nani na Mwanamume ni nani, yeye hajafanya hivyo kwako hajakuoa umemuoa hajakulipia mahari umemlipia mahari awe Mkeo wa ndoa, hukumuoa ili umwambie kila kitu kinachokuhusu wewe la hasha sio hivyo, hajakutoa kwenu na kwenda kuishi na wewe ila wewe ndie ulieamua hivyo kwamba huyu namuoa awe mke tujenge familia sio awe mtu wa kumwelezea kila kitu kinachonihusu na ukamtoa kwao na kwenda kuishi nae unapopataka wewe sio anapopataka yeye, grow up bro ukikua utanielewa nilikua namaanisha nini
 
Kazi zingine zinafahamika na huwezi zificha mfano mwalimu πŸ˜€πŸ˜†
Sawa sijakataa ila sikumaanisha hivyo ungenielewa usingefika huko, sio Mwalimu tu kuna kua Msanii anaejulikana hio ipo open sababu unajulikana kabisa wewe kazi yako ni hii, ila haina maana kua Msanii basi anafanya kazi ya sanaa tu peke yake, no sio hivyo nyuma ya sanaa zipo kazi zingine anazozifanya nje ya sanaa, sasa hizo ndio zipo kapuni, did you get me?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…