Papa Francis: Mapenzi ya Jinsia Moja siyo Kosa, siyo Uhalifu, lakini ni Dhambi
Papa amesema ushoga sio dhambi kwa maana kubwa amehalalisha

Waroma woyooooo
Bora KKKT yangu migogoro ila ushoga noo
 
Nitumie nafasi kuwakaribosha waroma kanisa kwetu KKKT

Sisi kwetu ushoga ni dhambi.

Na inayokana na msingi wa kibiblia kabisa

Njoo Lutheran ujifunze neno la Mungu na tuishi humu
 
Kama sio kosa, uhalifu, lakini ni dhambi, sasa kosa na uhalifu sio ni aina ya dhambi? Sasa yeye kazi yake sio kuwaelekeza hao mbinguni? Je, anachukua hatua gani dhidi ya dhambi hiyo? Hivi Yesu wa Nazareti wakati akiwa duniani alilishughulikia suala ili kivipi?

Hivi ile ya Sodoma na Gomola (kama ni kweli) kulikuwa hakuna serikali au serikali kama ilikuwepo ilihalalisha suala hilo?

Nature inaonesha vitendo hivyo sio sahihi. Halafu kuna sayansi inachochea mambo hayo, badala ya kuwa na sayansi ya kuzuia mambo hayo.
 
Vuta picha kama kiongozi yoyote wa kiislam kutoka sehemu yoyote Duniani kama angetoa Tamko hili waislam wangechukua hatua gani mpaka muda huu,
Kuna tofauti kubwa kati ya dini za watu na dini ya Mungu

Huyo ni kiongozi wa kiislamu pia ila wewe HUWEZI kujua

ASOMAYE na AFAHAMU.
 
HILI NI KANISA LA SHETANI LIMEANDIKWA KWENYE UFUNUO 17
ASOMAYE NA AFAHAMU.

Hawa Hawa ndio waliomuingiza mtume chka na KUSHUSHA kitabu Chao.

Wanashare.
Ubani.
Hudi.
KOFIA.
ROZALI.
.

Mwanamke (yule Babeli) wa Ufunuo 17 anaelezwa kuwa

“alikuwa amevikwa nguo ya rangi ya zambarau, na nyekundu, amepambwa kwa dhahabu, na kito cha thamani, na lulu, naye alikuwa na kikombe cha dhahabu mkononi mwake, kilichojawa na machukizo, na machafu ya uasherati wake. Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, Siri [2 The. 2:7], Babeli Mkuu, Mama wa Makahaba” [Ufu. 17:5, KJV
 
Papa yuko sasa, kuna uhalifu na dhambi. Uhalifu mara nyingi ni pale unapoenda kinyume na sheria za kidunia. Ingawa uhalifu pia yaweza kuwa dhambi lakini utahukumiwa na sheria za kidunia. Dhambi ni pale unapovunja sheria za Mungu/ Dini. Ukitenda dhambi hauhukumiwi kwa sheria za dunia bali hukumi yako itafanywa na Mungu mwenyewe.

Kanisa halihukumu wenye dhambi, ila lina kemea dhambi. Kanisa haliwabagui wenye dhambi ila linakemea na kuonya wenye dhambi.

Ndo maana tuna watu makanisani ni wazinzi, tuna watu makanisani wanatembea na wake za watu n.k. Tunasali nao na hatukuwa kuwapiga mawe.

Nadhani kwenye hili swala inabidi tushushe mihemuko, tuliangalie kwa namna nyingine.

Kama nchi nadhani inatosha kuwa na sheria inayo ruhusu faragha bila kujali watu wanafanya nini huko faraghani. Na kanisa kazi yake iendelee kuhubiri injili na kukemea dhambi bila kubagua wenye dhambi.
 
Yuko sahihi,! Ushoga ni choice hakuna mtu anakushikia bunduki uwe shoga ni kwa ujinga wako mwenyewe kuwalaumu viongozi wa dini au wamarekani ni mwendelezo wa utamaduni wa malalamishi ambao waafrica tunao.

Be the Gadem MAN stop blaming other people on your life choices.
 
Unamtukana papa na ukatolic lkn maajabu unatumia kalenda waliyoandaa wao, unasali siku waliyoandaa wao, unatumia biblia waliyoandaa wao, na vile vile unampinga papa wakati anahusika na dini zote adi ya yule mtume feki wa kushushiwa kitabu tokea mbingu za kusadikika.

Ukimkataa papa ukatae ukristo hata uislam pia maana huyo ndiye nguzo za dini zote kwa mgongo wa kificho.

Rudini ktk asili zenu kamwe hamtoteseka na uvuguvugu wa hao matapeli wenu mnaowaita viongoz wa dini.

Umenena vyema sana mkuu. Nafurahi KUONA jf Ina Great thinkers.

KRISTO YESU NDIYE MKOMBOZI WA ULIMWENGU.
JIWE KUU LA PEMBENI.
 
Someni sana Biblia SOMENI BIBLIA NDIO KITABU CHA KWELI.
SHETANI NA ROMA WANAIHARIBU LAKINI HAWATAWEZA.

UNABII UNAZIDI KUTIMIZWA.


Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

Ufunuo wa Yohana 17:5
 
Hello Wadau.

Papa Francis wa RC ya Vatican ameupiga mwingi kwa kuunga mkono ushoga na kusema mashoga siyo wahaliifu, na kwamba ni wana wa Mungu pia.[emoji849][emoji849]

Haijaeleweka mara moja ikiwa huu ndiyo msimamo wa Kanisa Katoliki au ni maoni binafsi ya Papa Francis.

Commets ziwe fupi fupi tafadhali.

------
Papa Francis amekosoa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja kuwa "sio haki", akisema Mungu anawapenda watoto wake wote jinsi walivyo na kuwataka maaskofu wa Kikatoliki wanaounga mkono sheria hizo kuwakaribisha watu wa LGBTQ kanisani.

"Kuwa mpenzi wa jinsia moja si kosa," Francis alisema wakati wa mahojiano Jumanne na The Associated Press.

Francis alikiri kwamba maaskofu wa Kikatoliki katika baadhi ya sehemu za dunia wanaunga mkono sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja au kubagua jamii ya LGBTQ, na yeye mwenyewe alitaja suala hilo kwa maneno ya "dhambi".

Lakini alihusisha mitazamo hiyo na asili ya kitamaduni na kusema maaskofu hasa wanahitaji kupitia mchakato wa mabadiliko ili kutambua utu wa kila mtu.

"Maaskofu hawa wanapaswa kuwa na mchakato wa uongofu," alisema, akiongeza kwamba wanapaswa kutumia "huruma, upole, kama Mungu ana kwa kila mmoja wetu".

Baadhi ya nchi 67 au mamlaka duniani kote zinaharamisha shughuli za ngono za watu wa jinsia moja zilizokubaliwa, 11 kati ya hizo zinaweza au kutoa hukumu ya kifo, kulingana na Human Dignity Trust, ambayo inafanya kazi kukomesha sheria hizo. Wataalamu wanasema kwamba hata pale ambapo sheria hazitekelezwi, zinachangia unyanyasaji, unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu wa LGBTQ.

Nchini Marekani, zaidi ya majimbo kumi na mbili bado yana sheria za kupinga mapenzi ya jinsia moja kwenye vitabu, licha ya uamuzi wa Mahakama ya Juu wa 2003 kutangaza kuwa ni kinyume cha katiba.

Umoja wa Mataifa mara kwa mara umekuwa ukitoa wito wa kukomeshwa kwa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja , ukisema zinakiuka haki za faragha na uhuru wa kutobaguliwa na ni ukiukaji wa majukumu ya nchi chini ya sheria za kimataifa kulinda haki za binadamu za watu wote, bila kujali mwelekeo wao wa kijinsia au utambulisho wa kijinsia.

Akitangaza sheria kama hizo "sio za haki", Francis alisema Kanisa Katoliki linaweza na linapaswa kufanya kazi ili kukomesha. "Lazima ifanye hivi. Ni lazima ifanye hivi,” alisema.

Francis alinukuu Katekisimu ya Kanisa Katoliki kwa kusema wapenzi wa jinsia moja lazima wapokewe na kuheshimiwa, na hawapaswi kutengwa au kubaguliwa.

"Sisi sote ni watoto wa Mungu, na Mungu anatupenda jinsi tulivyo na kwa nguvu ambayo kila mmoja wetu anapigania utu wetu," Francis alisema, akizungumza na AP katika hoteli ya Vatican anakoishi.

Sheria hizo ni za kawaida barani Afrika na Mashariki ya Kati na ni za wakati wa ukoloni wa Waingereza au zimeongozwa na sheria za Kiislamu.

Baadhi ya Maaskofu wa Kikatoliki wameziunga mkono kwa nguvu kwamba zinaendana na mafundisho ya Vatikani ambayo yanachukulia vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kuwa "vina machafuko ya asili", huku wengine wakitaka zibatilishwe kama ukiukwaji wa utu msingi wa binadamu.

Mnamo mwaka wa 2019, Francis alitarajiwa kutoa tamko la kupinga kuharamishwa kwa mapenzi ya jinsia moja wakati wa mkutano na vikundi vya haki za binadamu ambavyo vilifanya utafiti juu ya athari za sheria kama hizo na kile kinachoitwa "matibabu ya ubadilishaji".

Hatimaye, papa hakukutana na makundi, ambayo badala yake yalikutana na mtu Nambari 2 Vatikani, ambaye alithibitisha tena "hadhi ya kila mtu na dhidi ya kila aina ya vurugu".

Siku ya Jumanne, Francis alisema kuna haja ya kuwa na tofauti kati ya uhalifu na dhambi kuhusiana na mapenzi ya jinsia moja.

"mapenzi ya jinsia moja si kosa," alisema. "Sio uhalifu. Ndio, lakini ni dhambi. Sawa, lakini kwanza tutofautishe kati ya dhambi na uhalifu.”

"Pia ni dhambi kukosa hisani," aliongeza.

Mafundisho ya Kikatoliki yanashikilia kwamba ingawa wapenzi wa jinsia moja lazima waheshimiwe, vitendo vyao "vina machafuko ya asili". Francis hajabadilisha mafundisho hayo, lakini amefanya kufikia jumuiya ya LGBTQ kuwa alama mahususi ya upapa wake.

Kuanzia na tamko lake maarufu la 2013: "Mimi ni nani kuhukumu?" alipoulizwa kuhusu kasisi aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa jinsia moja , Francis ameendelea kuhudumu mara kwa mara na hadharani kwa jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia .

Akiwa askofu mkuu wa Buenos Aires, alipendelea kutoa ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja kama njia mbadala ya kuidhinisha ndoa zao, jambo ambalo mafundisho ya Kikatoliki yanakataza.

Licha ya mawasiliano hayo, Francis alikosolewa na jumuiya ya Wakatoliki wa LGBTQ kwa amri ya 2021 kutoka ofisi ya mafundisho ya Vatikani kwamba kanisa haliwezi kubariki muungano wa watu wa jinsia moja "kwa sababu Mungu hawezi kubariki dhambi".

Vatikani mwaka wa 2008 ilikataa kutia saini tamko la Umoja wa Mataifa lililotaka kukomeshwa kwa mapenzi ya jinsia moja, ikilalamika kuwa maandishi hayo yalikwenda nje ya upeo wa awali na pia yalijumuisha lugha kuhusu "mwelekeo wa kijinsia" na "utambulisho wa kijinsia" .

Katika taarifa yake wakati huo, Vatikani ilizitaka nchi kuepuka "ubaguzi usio wa haki" dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kukomesha adhabu dhidi yao.

Chanzo: BBC Swahili
Mmmh hii dunia ngumu? Bora kusali mwenyewe tu.
 
Kama sio fake news naomba nitoe maandiko yanayozuhia ushoga. Maana yapo ktk Biblia takatifu yenye Vitabu 69.
Kama kweli yawezekana waandishi walimnukuu vibaya.
 
Ushoga ni dhambi na ni uhalifu!
Huyu Papa anaweza pia kuwa ni S........!
Kwanini watu wanaopaswa kusema bodly kwamba ushoga haukubaliki wanaremba remba maneno!
Ukimsoma Papa unaona kabisa anaunga mkono Ushoga!
Kwani Majambazi na Wauaji siyo watoto wa Mungu!
Wanakubali Ushoga ili kumpinga Mungu! Period
Je, uzinzi ni UHALIFU?
 
Shetani na katoliki ni kitu kimoja.

NIMESOMA NA KUFUATILIA HILI JAMBO ILA KUNA VITU HAWA JAMAA WA UPINDE WAMEVIONGEZEA KWA PAPA.

YANI WAMEMLISHA MANENO PAPA.
ILA NAE YUPO KARIBU SANA NA MASHOGA.

SOMENI BIBLIA UNABII UNATIMIA.

Na katika kipaji cha uso wake alikuwa na jina limeandikwa, la siri, BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA NCHI.

Ufunuo wa Yohana 17:5
 
Wapi aliposema haki za mashoga? Amezungumzia kuwa ni dhambi, ila sio uhalifu, na ni kweli kabisa. Wewe ukifumaniwa na mke wa mtu leo, hakuna sheria inayokupa adhabu, lakini ni dhambi.

Acha justfication papa kakosea sana kukubali nchi zikubali mapenzi ya jinsia moja ni kukubali ushoga kwenye jamii, ni kukubali dhambi nilitegemea yeye ndiyo akataze nchi za ulaya kupitisha sheria za aina izoo ila yeye ndyo kahalalisha wakubaliwe hakuna mtu asiyetenda dhambi na wote ni watoto wa Muumba lkini waje kanisa kutubu na kuacha siyo waje ndani ya kanisa kma watu wa jamii izoo na kanisa halitakiwi kutambua mapenzi au ndoa za namna iyoo
 
Kumbe ndio maana maaskofu na mapadri wa katoliki wanawalawiti sana watoto makanisani hasa huko Ulaya na Amerika!
 
Back
Top Bottom