Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa

Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa

MMOJA ASHIKILIWA KWA KUHUSISHWA NA TUHUMA ZA KUJERUHIWA KWA PADRI KITIMA

Tarehe 30 April 2025 majira ya saa nne usiku maeneo ya Baraza la Maaskofu Tanzania Kurasini Temeke Dar es salaam ilipokelewa taarifa ya kujeruhiwa kwa Padri Charles Kitima ambaye ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania.

Padri huyo Inadaiwa tangu saa tatu asubuhi walikuwa na kikao na viongozi wa dini mbalimbali na baada ya kikao kuisha saa 1 jioni alikwenda kwenye kantini yao ambapo aliendelea kupata kinywaji hadi saa nne na robo alipokwenda maliwatoni pembeni ya kantini hiyo ndipo alidai kushambuliwa kichwani na kitu butu na watu wawili.

Alipelekwa Hospitali ya Agakhan na anaendelea vizuri na matibabu. Mtu mmoja Rauli Mahabi Haraja mkazi wa Kurasini anashikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo. Uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua kali na za haraka zichulikuliwe kwa wahusika.

Imetolewa na

Kamanda Kanda Maalum ya Polisi

Dar es Salaam.

Pia soma
  1. Padri Kitima adaiwa kushambuliwa usiku huu. Inadaiwa hali yake ni mbaya
  2. Rais wa TEC, Askofu Pisa apingana na polisi, asema taarifa yao kuwa Padri Kitima alikuwa anapata kinywaji wakati anashambuliwa ni Upotoshaji
Walitakiwa waweke majina yake matatu na namba yake ya NIDA, namba yake ya simu ikibidi, lengo ni kujiridhisha na wasemacho polisi.
 
Vibaka wa kibibi Samia hawa. Hata ukiwa mjinga namna gani utajua hawa wametumwa kwa sababu kanisa limesema ukweli. Samia amesikika mara nyingi akitishia viongozi wa dini wanaosema ukweli.
Hiki ki ajuza naona urais unakitoa akili.
 
Polisi wa nchi hii wakamate mtuhumiwa usiku huohuo wa tukio kama hili.

Unaamini kakamatwa mtuhumiwa kweli au mtaletewa kanyaboya tu kusafisha hali ya hewa!
Uzuri ni kwamba raia hawahitaji taarifa,majibu tayari tunayo
 
Muliro hana tofauti na Wasira. Uwezo wao wa kufikiri uko chini sana. Hayo yote yametokana na uzee.
muliro yuko vizuri kichwani tatizo amri anazopewa usijekuta ndo za hovyo
 
Yaani Padre Kitima aliendelea kutandika pombe kuanzia saa moja hadi saa nne.na robo usiku

Sadaka za wakatoliki zinabomolewa hasa.
Hongereni wakatoliki watoa sadaka
Acha wivu. Ulitaka atumie pesa zako
 
Bro tumia akili muda mwingine uchawa wako utatufikisha pabaya.
Daaa! Yaan asee anaonekana anapenda sana umafia au atakuwa sio mtz, wala hizo sio sifa za wanCCM au atakuwa mchawi ashazoea kula nyama za watu.
 
Issue ni kunywa au issue ni kushambuliwa akiwa eneo la makaazi yao?
Hivi aliyetoa ile statement ana weredi?
na wapi hasa aliposhambuliwa, murilo anasema alishambuliwa chooni, tec alishambuliwa kwenye uchochoro akielekea nyumbani,
 
1746094191314.png
 
Back
Top Bottom