Polisi: Tunamshikilia Mtu mmoja kutokana na tukio la Padri Kitima kushambuliwa

Wewe huoni uzito wa tukio? Unaona Katibu wa TEC ni sawa na hayo matukio mengine? Uliambiwa baada ya kufanya tukio hilo mtuhumiwa alikimbia? Hujaona swala la kinywaji hapo? Shirikisha vidole na ubongo wako.
Mnaona mkitaja kinywaji ndio mtapata kichaka cha kijifichia? Huyo aliyekamatwa alipaswa kutajwa kwa majina matatu na namba yake ya NIDA? Askofu Pisa ametoa taarifa maeneo hayo hayana bar. Huu mchezo wa kutoa taarifa za uongo huwa mnazitumia sana kwa cdm, lakini sasa utafika mwisho.
 
Acha wivu. Ulitaka atumie pesa zako
Padre Kitima Anatumia pesa za sadaka kulewea unaona sawa? Waumini wanabanwa kwenye jumuiya hatari kuwa wachangie hadi maskini wasipochangia mapadre wanagoma kuwapa huduma kama ndoa,mazishi nk kisa hatoi sadaka jumuiya kumbe wanachangia chapombe akina Padre Kitima nk

Hiyo sio sawa
 
Wewe ulitaka anywe togwa!?
 
muliro yuko vizuri kichwani tatizo amri anazopewa usijekuta ndo za hovyo
Asingekubaliana nazo. Lkn kwakuwa ubongo wake kisayansi ulishachoka anajiona ni kijana mwenye nguvu na uwezo wa kuyatekeleza maagizo ya hovyo.
 
Mnaona mkitaja kinywaji ndio mtapata kichaka cha kijifichia? Huyo aliyekamatwa alipaswa kutajwa kwa majina matatu na namba yake ya NIDA? Askofu Pisa ametoa taarifa maeneo hayo hayana bar. Huu mchezo wa kutoa taarifa za uongo huwa mnazitumia sana kwa cdm, lakini sasa utafika mwisho.
Soma tena taarifa ametajwa kwa majina matatu. Kwani wamesema bar au canteen? Acheni kukurupuka someni taarifa vizuri.
 
MMOJA ASHIKILIWA KWA KUHUSISHWA NA TUHUMA ZA KUJERUHIWA KWA PADRI KITIMA

Tarehe 30 April 2025 majira ya saa nne usiku maeneo ya Baraza la Maaskofu Tanzania Kurasini Temeke Dar es salaam ilipokelewa taarifa ya kujeruhiwa kwa Padri Charles Kitima ambaye ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania.

Padri huyo Inadaiwa tangu saa tatu asubuhi walikuwa na kikao na viongozi wa dini mbalimbali na baada ya kikao kuisha saa 1 jioni alikwenda kwenye kantini yao ambapo aliendelea kupata kinywaji hadi saa nne na robo alipokwenda maliwatoni pembeni ya kantini hiyo ndipo alidai kushambuliwa kichwani na kitu butu na watu wawili.

Alipelekwa Hospitali ya Agakhan na anaendelea vizuri na matibabu. Mtu mmoja Rauli Mahabi Haraja mkazi wa Kurasini anashikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo. Uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua kali na za haraka zichulikuliwe kwa wahusika.

Imetolewa na

Kamanda Kanda Maalum ya Polisi

Dar es Salaam.

Pia soma
  1. Padri Kitima adaiwa kushambuliwa usiku huu. Inadaiwa hali yake ni mbaya
  2. Rais wa TEC, Askofu Pisa apingana na polisi, asema taarifa yao kuwa Padri Kitima alikuwa anapata kinywaji wakati anashambuliwa ni Upotoshaji
Waalifu wote picha zao mnaonesha….. huyu alieshikiliwa imekuaje?
 
Asingekubaliana nazo. Lkn kwakuwa ubongo wake kisayansi ulishachoka anajiona ni kijana mwenye nguvu na uwezo wa kuyatekeleza maagizo ya hovyo.
akikataa utamlisha wewe
 
Soma tena taarifa ametajwa kwa majina matatu. Kwani wamesema bar au canteen? Acheni kukurupuka someni taarifa vizuri.
Peleka uduwanzi mbali, taarifa gani ya kusoma vizuri hapo we boya @ ni jina la mtanzania gani?
 
Mnaona mkitaja kinywaji ndio mtapata kichaka cha kijifichia? Huyo aliyekamatwa alipaswa kutajwa kwa majina matatu na namba yake ya NIDA? Askofu Pisa ametoa taarifa maeneo hayo hayana bar. Huu mchezo wa kutoa taarifa za uongo huwa mnazitumia sana kwa cdm, lakini sasa utafika mwisho.
Hakika kabisa, Ccm na polisiuvccm wao waongo, hawana utu na hawatumii vizuri akili zao,
Waweke na kitambulisho chake kikamilifu, ni mkaazi wa mitaa ipi, anafanya shughuli zipi.
 
MMOJA ASHIKILIWA KWA KUHUSISHWA NA TUHUMA ZA KUJERUHIWA KWA PADRI KITIMA

Tarehe 30 April 2025 majira ya saa nne usiku maeneo ya Baraza la Maaskofu Tanzania Kurasini Temeke Dar es salaam ilipokelewa taarifa ya kujeruhiwa kwa Padri Charles Kitima ambaye ni Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania.

Padri huyo Inadaiwa tangu saa tatu asubuhi walikuwa na kikao na viongozi wa dini mbalimbali na baada ya kikao kuisha saa 1 jioni alikwenda kwenye kantini yao ambapo aliendelea kupata kinywaji hadi saa nne na robo alipokwenda maliwatoni pembeni ya kantini hiyo ndipo alidai kushambuliwa kichwani na kitu butu na watu wawili.

Alipelekwa Hospitali ya Agakhan na anaendelea vizuri na matibabu. Mtu mmoja Rauli Mahabi Haraja mkazi wa Kurasini anashikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo. Uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua kali na za haraka zichulikuliwe kwa wahusika.

Imetolewa na

Kamanda Kanda Maalum ya Polisi

Dar es Salaam.

Pia soma
  1. Padri Kitima adaiwa kushambuliwa usiku huu. Inadaiwa hali yake ni mbaya
  2. Rais wa TEC, Askofu Pisa apingana na polisi, asema taarifa yao kuwa Padri Kitima alikuwa anapata kinywaji wakati anashambuliwa ni Upotoshaji
Polisi wasiwe wanaonea watu.Huyo mtu alishikwa amsshikiliwa kimakosa.Haya yanayotendeka leo ni maagizo kutoka juu.Wale wote wanaoshambulia na kukosoa serikali ya Samiah watakiona cha mtema kuni bila kujali hadhi zao na majukumu yao kwa jamii.
 
Hakika kabisa, Ccm na polisiuvccm wao waongo, hawana utu na hawatumii vizuri akili zao,
Waweke na kitambulisho chake kikamilifu, ni mkaazi wa mitaa ipi, anafanya shughuli zipi.
Rais wa Baraza la Maaskofu nchini, Askofu Wolfgang Pisa O.F.M. Cap, amekanusha vikali taarifa iliyotolewa na jeshi la Polisi kwamba Katibu Mkuu wa Baraza hilo Fr.Dr.Charles Kitima (PhD) alikua anapata kinywaji kabla ya kushambuliwa.

"Hakuna baa katika eneo aliloshambuliwa Fr.Kitima na hivyo hakuwa anapata kinywaji kama inavyoelezwa. Pale ni mgahawani. Kusema mtu alikua anakunywa saa zote hizo si kweli. Tunaandaa taarifa kamili, tutaitia itakapokua tayari" Amesema Askofu Pisa.

#MyTake:
Ikiwa haya aliyoyasema Baba Askofu Pisa ni ya kweli, ina maana Polisi wamedanganya. Sasa je wamedanganya kwa faida ya nani? Na kwa lengo gani? Hivi Muliro anaijua Novena Mtakatifu Ritha wa Kashi kweli?
 
Utawala huu ukianguka, upo umuhimu jeshi la polisi na usalama kufumuliwa upya
 
Back
Top Bottom