Watanzania tuna mambo,eti tunaridhia na kumuomba MTU aliyopo madarakani ndio arekebishe Katiba na aturuhusu kufanya mikutano ya kisiasa.
Kwa kweli sisi ni matahira wa mwisho Duniani.
Tunataka uhuru wetu na Taifa letu pia. Tatizo letu ni mahakama ya Tanzania imejaza watu wasio huru. Hili jambo lingemalizwa na mahakama lakini yenyewe huwa inajifanya haijui ifanye nini.
 
Kuna kitanzi kinataka kuning'ing'izwa hapo ili jamaa waende na maji.😁.

"Msajili wa vyama aandae muongozo wa chaguzi za ndani za vyama vya siasa".
 
Kauli za rais zinavunja moyo.
Kikosi kazi kimefanya kazi nzuri sana
 
Kama walikaa karibu mwaka mzima kujadili hizi hoja 18 ambazo hazina mashiko siyo jipya zaidi ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
 
Watanzania tumepigwa na kitu kizito kisigoni hatujui ni kipi kitatokea

Hakuna jipya hapo yote ni blaah blaah zakusogeza siku Ili 2024&2025 zifike na wanaojiona wanahati miliki ya nchi wachukue vyao

Kuna ugumu gani Kwa mh rais kuhuisha rasimu ya warioba ? Gharama za tume hii busara tu wangenyofoa kipengele Cha aina ya muungano mengine yote wakayaacha kama yalivyo na inakuwa katiba

Inatia hasira nchi hii kweli eti ,jambo dogo linachukua miezi kumi ?

Na hao mnajiita mpo kwenye maridhiano tayari mmekwisha kupoteza tayari. Jiulize swala ambalo lipo kisheria tayari nalenyewe kamati inashauri ifunguliwe kipindi hicho sheria inaitambua .

CHADEMA kazi kwenu kuendelea na maridhiano ambayo nayo yatachukua miezi kumi au mjitoe
 
CHADEMA kazi kwenu kuendelea na maridhiano ambayo nayo yatachukua miezi kumi au mjitoe
Mara nyingi CHADEMA inakuwa kama iko juu kileleni na inataka kuangukia ama kwenye mwamba au kwenye ardhi ngumu. Maridhiano ni muhimu, lakini CHADEDMA inapata nini na inapoteza nini, ndiyo jambo la kujadili.
 
Mfumo mzuri wa uaandaji.. tusibir serikali ifanye maamuzi yake...
Ila kama mama akikubali hili na kabadili katiba.. bas atawekwa kwenye kumbukumbu kubwa ya tz hii
 
Je, Hawa sio wateule wa rais?(ambaye ni m/kiti wa ccm/chama Cha siasa). Hii haitakuwa sawa na kutwanga maji kwny kinu?
 
Dominated power ya tawala hata iundwe mahakama chini ya mwamba bado mgombea wa tawala atapita tu!

Kitu kimoja ninachojifunza, hasa nikiangalia haya yanayoendelea na akili za oppositions wetu, tawala wapo smart sana sana! Huku kwenye porojo tunawapopoa lakini ndani wamejipanga in a very complicated system.

Kama hujanielewa angalia game ya Al hilal vs Yanga! Yanga walitawala mchezo lakini hawakucheza kufuzu, Al Hilal hawakutawala lakini walicheza kufuzu! Ndicho wanachofanya tawala.

Sometimes wanaacha mpige kelele hadi mhisi mnabeba nchi saa mbili asubuhi lakini wanajua mwisho wa utawala wenu ni kwenye kelele huku wao wanashinda na kuwaacha muendelee kupiga kelele! Mnapewa viti vya uwakilishi huko dom kuwapoza, viongozi wa upinzani na wawakilishi wa dom wanapewa vi safari na viposho posho wana enjoy life huku wakiunda vikundi vya kupiga kelele mitandaoni kulinda nafasi zao!

Mfumo wa sihasa uko very corrupted! Tunadanganyana majukwaani tu!
 

Tatizo la Rais wetu Hana kauli ya moja kwa moja. Anaongea kwa katikati Yani hatoi suluhisho.
 
Mara nyingi CHADEMA inakuwa kama iko juu kileleni na inataka kuangukia ama kwenye mwamba au kwenye ardhi ngumu. Maridhiano ni muhimu, lakini CHADEDMA inapata nini na inapoteza nini, ndiyo jambo la kujadili.
Hayana umuhimu wowote zaidi yanaisadia CCM kuendelea kujimilikisha nchi kama mali yao

Hujaone jinsi walivyopendekeza kuhusu msajili wa vyama na chaguzi za ndani ya vyama ?

Nilifikili nyundo waliokuwa wanapewa space walizifanyia kazi , kumbe na wao ni sawa tu na serikali na mambo yake
 


Ndio maana CHADEMA wanalilia Katiba Mpya ili kuondoa hicho unachokisema.
 
Vyama visipewe ruzuku.
Chama tawala kisitumie rasilimali za serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…