Profesa Assad: Hakuna bandari inayouzwa, ni uelewa mdogo wa watu

Kusaini mkataba huu wazanzibar tanganyika ni suala la muungano
Japo maandishi yako hayajakaa sawa nimekuelewa ni hivi wamesaini kwa niaba ya Tanzania sio Tanganyika hiyo Tanganyika mulishafuta tokea 19 6 4
 
Kwani wewe umeongelea wasomi wa kiislamu au waislamu kwa ujumla?
Kama unawajua waislamu wa Tanzania vizuri, basi utajua kuwa, wao waathirika wakubwa na wa mwanzo kabisa wa sera za hovyo za hii awamu ya 6. Katika watu ambao hawataki kabisa kusikia upuuzi wa hii awamu ya 6 ni waislamu.
Kuingiza dini katika masuala ya kitaifa na hususan hili la bandari ni dalili ya ujinga mkubwa wa kifikra. Kwasababu ni sawa na kutumika ku-antagonize watu katika kisingida ya kidini ili kuvuruga mjadala. Mwenyewe unadhani unajenga lakini kiukweli una bomoa.
Mim ninachojua hao waislm wengi unaosema wana kiongozi wao sasa ndo uniambie ata kiongozi wao mmoja anaeunga mkono akina mwabukusi kupinga hao waraabu wa dp world, masheikh wote maarufu hapa mjini wapo na dp, mpaka sheikh wangu yule Rusaganya mwana wa kigoma kazma dp mzima mzima
 
Points Muhimu kwenye mahojiano ya Profesa Assad pale Channel Ten kwenye kipindi cha Dira ya Uchumi

[emoji1485] Hakuna Bandari Inayouzwa, ni uelewa mbaya tu wa watu. (Sikiliza zaidi)

[emoji1485] Ukomo hauwekwi kwenye IGA, bali kwenye mikataba ya chini (Projects Agreements). (Sikiliza Zaidi)

Profesa Assad ametoa majibu mazuri kabisa, na huyu ndio Profesa wa kweli sasa, sio wale wengine akina Tibaijuka na Shivji, wachumia tumbo tu, Sikilizeni nondo kutoka kwa Prof.

View attachment 2712096
View attachment 2712097
View attachment 2712098
View attachment 2712099

Prof. Assad: Kuongeza kodi hakusaidii pato la Nchi
Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema Nchi zilizofanikiwa sio ambazo zilifanikiwa kuongeza kodi.

Akizungumza katika mahojiano na Channel Ten, Profesa Assad amesema “Kwa mfano kiwango cha Kodi ya Kampuni Nchini ni 30%, hicho ni kiwango kikubwa sana, Taifa kama Ireland ni moja ya Nchi zilizovutia wawekezaji wengi Ulaya, kiwango chao cha Kodi ni 18%.”

Ameongeza kuwa haungi mkono kupanda kwa kodi kwa kuwa ikishushwa makusanyo yake yatapanda na kusaidia Nchi.

Prof. Assad: Mamlaka zishiriki kukuza wafanyabiashara wadogo sio kusubiri mpaka wakue
“Tuwafundishe watu umuhimu wa uwekaji wa hesabu za fedha, si kwa sababu ya kukusanya kodi, akiweka hesabu zake vizuri miaka mitano sita atahitaji mkopo wa benki, baada ya hapo atakata leseni na tutatoa kodi kidogokidogo,” - Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (#CAG), Profesa Mussa Assad.

PROF. ASSAD: MKATABA WA BANDARI UNAHUSU HAKI ZA ARDHI SIO UMILIKI
Akitoa maoni kuhusu uwekezaji wa DP World katika Bandari, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (#CAG), Profesa Mussa Assad amesema tatizo ni dhana ambazo si nzuri kufikiri kuwa wawekezaji watafanya vitu ambavyo havifai pamoja na watu ambao sio wataalam husika kulisemea jambo hilo.

Akizungumza katika mahojiano na Channel Ten, amesema “Kuna wataalam wa uwekezaji wakiwemo Wanasheria wa Uwekezaji japo ni wachache lakini sisi tunawasikiliza Wanasheria wa Kodi, Wanasheria za Familia, Wanasheria wa mambo ya kampuni ambao ndio wameingia katika maeneo ambayo hayana tija na kusababisha dhana mbaya.”

Ameongeza “Watu wengi si wataalam wa uwekezaji, kipengele kinachozungumziwa katika mkataba ni Haki za Ardhi, sio umiliki, wanachomaanisha ni haki ya utumiaji lakini mmiliki ataendelea kubaki Shirika la Bandari, kuhusu suala la ukomo wanaweza kuweka hata miaka 25 au 30 basi ili watu wakafurahi.”

Mimi Nina amini Hapa pro. Asad ameamua kuitumia akili na elimu yake vibaya tu Tena kwa makusudi Ili aendane na matakwa ya tumbo
 
Tuna nchi ya ajabu sana na wasomi wetu ni wa ajabu

Kwa nini wasomi wetu hawaheshimiani?

Mtu aliyesoma uchumj, badala azungumzie uchumi, unakuta ndio kwaanza ametoka na misuri ya shingo anaongelea mambo ya kisheria, kitu ambacho si sawa

Unamkuta mtu aliyesomea Sheria, anekalia kuzungumzia mambo ya uchumi akiwaaminisha wananchi kwamba, wamsikilize? Stupid!

Na ndiyo maana hata kwenye kuandaa mawaziri mbalimbali, kinachokuwa kinazingatiwa, ni Professional zao na siyo blablaa!

Tunakwama wapi kuheshimu fani za wengine?

Hi la juzi kwa Msomi nguli wa uchumi Prf Hasadi kuhitimisha eti wanasheria wamepotoka, mandate hiyo aliitoa wapi?

Yeye ni nani katika fani ya sheria?
 
Tuache wataalamu wa uchumi na uwekezaji watuelemishe faida za kiuchumi na uwekezaji kutokana na uwekezaji wa bandari. Tukiacha Kila mtu akawa mchambuzi wa uchumi itakuwa haina maana kuwa na wachumi.
 
Umesema vema mkuu, Je linapokuja suala la sheria azungumze mtaalamu wa uchumi au sheria?
 
Tuna nchi ya ajabu sana na wasomi wetu ni wa ajabu

Kwa nini wasomi wetu hawaheshimiani?

Mtu aliyesoma uchumj, badala azungumzie uchumi, unakuta ndio kwaanza ametoka na misuri ya shingo anaongelea sheria, kitu ambacho si sawa

Unamkuta mtu aliyesomea Sheria, anekalia kuzungumzia mambo ya uchumi akiwaaminisha wananchi kwamba, wamsikilize? Stupid!

Na ndiyo maana hata kwenye kuandaa mawaziri mbalimbali, kinachokuwa kinazingatiwa, ni Professional zao na siyo blablaa!

Tunakwama wapi kuheshimu fani za wengine?

Hi la juzi kwa Msomi nguli wa uchumi Prf Hasadi kuhitimisha eti wanasheria wamepotoka, mandate hiyo aliitoa wapi?

Yeye ni nani katika fani ya sheria?

  • Lissu
  • Mwabukusi
  • 1,354,900

Wote hawa 1,354,900 wamesoma sheria na hawataki DP World.

Ukimtafuta Mama Ntilie mzuri mwenye ujuzi wa kulipa pango la meza yake na kulipa kodi, anaweza kabisa kuona matatizo ya huu mkataba.

Ukimchukua kijana wangu wa form 3 ukampa ausome anaweza kabisa kukwambia mbona kama hapa pana uonevu!

Asad is tooo very senior ku doubt uwezo wake kwenye mkataba wa DP world, ana uwezo kabisa wa kuelewa na kukosoa.

Asad wa watu kakukosea nini?

Rubbish.
 
Points Muhimu kwenye mahojiano ya Profesa Assad pale Channel Ten kwenye kipindi cha Dira ya Uchumi

[emoji1485] Hakuna Bandari Inayouzwa, ni uelewa mbaya tu wa watu. (Sikiliza zaidi)

[emoji1485] Ukomo hauwekwi kwenye IGA, bali kwenye mikataba ya chini (Projects Agreements). (Sikiliza Zaidi)

Profesa Assad ametoa majibu mazuri kabisa, na huyu ndio Profesa wa kweli sasa, sio wale wengine akina Tibaijuka na Shivji, wachumia tumbo tu, Sikilizeni nondo kutoka kwa Prof.

View attachment 2712096
View attachment 2712097
View attachment 2712098
View attachment 2712099

Prof. Assad: Kuongeza kodi hakusaidii pato la Nchi
Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad amesema Nchi zilizofanikiwa sio ambazo zilifanikiwa kuongeza kodi.

Akizungumza katika mahojiano na Channel Ten, Profesa Assad amesema “Kwa mfano kiwango cha Kodi ya Kampuni Nchini ni 30%, hicho ni kiwango kikubwa sana, Taifa kama Ireland ni moja ya Nchi zilizovutia wawekezaji wengi Ulaya, kiwango chao cha Kodi ni 18%.”

Ameongeza kuwa haungi mkono kupanda kwa kodi kwa kuwa ikishushwa makusanyo yake yatapanda na kusaidia Nchi.

Prof. Assad: Mamlaka zishiriki kukuza wafanyabiashara wadogo sio kusubiri mpaka wakue
“Tuwafundishe watu umuhimu wa uwekaji wa hesabu za fedha, si kwa sababu ya kukusanya kodi, akiweka hesabu zake vizuri miaka mitano sita atahitaji mkopo wa benki, baada ya hapo atakata leseni na tutatoa kodi kidogokidogo,” - Aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (#CAG), Profesa Mussa Assad.

PROF. ASSAD: MKATABA WA BANDARI UNAHUSU HAKI ZA ARDHI SIO UMILIKI
Akitoa maoni kuhusu uwekezaji wa DP World katika Bandari, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (#CAG), Profesa Mussa Assad amesema tatizo ni dhana ambazo si nzuri kufikiri kuwa wawekezaji watafanya vitu ambavyo havifai pamoja na watu ambao sio wataalam husika kulisemea jambo hilo.

Akizungumza katika mahojiano na Channel Ten, amesema “Kuna wataalam wa uwekezaji wakiwemo Wanasheria wa Uwekezaji japo ni wachache lakini sisi tunawasikiliza Wanasheria wa Kodi, Wanasheria za Familia, Wanasheria wa mambo ya kampuni ambao ndio wameingia katika maeneo ambayo hayana tija na kusababisha dhana mbaya.”

Ameongeza “Watu wengi si wataalam wa uwekezaji, kipengele kinachozungumziwa katika mkataba ni Haki za Ardhi, sio umiliki, wanachomaanisha ni haki ya utumiaji lakini mmiliki ataendelea kubaki Shirika la Bandari, kuhusu suala la ukomo wanaweza kuweka hata miaka 25 au 30 basi ili watu wakafurahi.”

Tatizo hili sakata la Bandari limepoteza professionalism arguments na badala yake limekuwa la Udini, Uzanzibari na Utanganyika. Huwezi kumsikia Muislam au Mzanzibar akiuponda huo mkataba bali atamtetea Samia kwa sababu ya Uislam na Uzanzibar wake
 
Mkuu si mmesema swala la bandari halina udini ?
Halina yes lakini kuna baadhi ya watu kama assad,zito na wengine wanaweka udini lakini mtu kama Shivji kajadili kitaalamu bila kuweka mambo ya dini tofauti ndio iko hapo
 
Back
Top Bottom