Profesa Assad: Hakuna bandari inayouzwa, ni uelewa mdogo wa watu

Profesa Assad: Hakuna bandari inayouzwa, ni uelewa mdogo wa watu

Mambo ya afya tuwaachie madaktari, mambo ya uchumi tuwaachie wachumi, mambo ya fedha tuwaachie wanamahesabu, mambo ya sheria waachie wanasheria.

Renowned lawyers like Professor shivji walishaongea, wewe ni nani katika sheria?
Shivji nu human right (ardhi) lawyer kwa hiyo kwenye IGA ni mweupe kabisa
 
Tatizo hili sakata la Bandari limepoteza professionalism arguments na badala yake limekuwa la Udini, Uzanzibari na Utanganyika. Huwezi kumsikia Muislam au Mzanzibar akiuponda huo mkataba bali atamtetea Samia kwa sababu ya Uislam na Uzanzibar wake
Mkuu haya hilo la uislam na uzanzibar tumelichukua; turudi kwenye IGA kutumia na kumiliki ardhi ni maneno yenye maana moja?
 
Prof Shivji alishindwa kuiona tofauti ya BIT na IGA, aliuingia mtego ule ule uliowanasa watanzania wengi wa kudhani kuwa mkataba uliokwenda bungeni ndio huo huo utakaotumika kibiashara wakati ukweli ni kwamba kibiashara itabidi iandikwe mikataba mingine kutokana na mawanda ya uwekezaji mzima wa DP World.

Profesa Assad hajaongea kama mjamaa, wakati Profesa Shivji aliongea kama mwanafunzi wa zamani wa Mwalimu Nyerere aliyeamini na kuzama kwenye fikra za kijamaa.
Acha upotoshaji,Shivji hakusema eti IGA ndio itatumika kibiashara.Alichosema ni kuwa hizo HGA ndo zitatumika kibiashara lakini zitakuwa ni Siri na hazitaweza ku- cure mapungufu yaliyomo kwenye IGA,Kwani IGA ndo mkataba mkubwa
 
Halina yes lakini kuna baadhi ya watu kama assad,zito na wengine wanaweka udini lakini mtu kama Shivji kajadili kitaalamu bila kuweka mambo ya dini tofauti ndio iko hapo
Mkuu Shivji with due respect ni human right (ardhi) lawyer, kwenye IGA uelewa wake ni mdogo sana ni kama wangu na wewe. Mkuu nakuomba sana usije ukaugulia na mtoto aukamkimbiza kwa Dr. Msukuma kisa anaitwa DR.
 
With due respect Prof atulie!...Angle hii sio yake!
Shivji kashaongea..
Mkuu in the same spirit, Prof. Shivji ni human right (land issue)lawyer, kwenye IGA is not an authority
 
Ni kweli kabisa hakuna palipoandikwa inauzwa lakini pia hakuna palipoandikwa inakodishwa wala kupangishwa hivyo basi.

Kama haiuzwi
Kama haikodishwi
Kama haipangishwi

Maana yake ni moja tu inatolewa bure...

Zaidi Assad naye anataka kugeuka mchumia tumbo.

Maana yeye anazungumzia bandari moja tu wakati IGA inasema bandari zote Tanzania na miundombinu yake.

Mwambie kachelewa kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiyasema haya kwenye kijiwe cha kahawa utapewa maua yako ila siyo humu
 
Acha upotoshaji,Shivji hakusema eti IGA ndio itatumika kibiashara.Alichosema ni kuwa hizo HGA ndo zitatumika kibiashara lakini zitakuwa ni Siri na hazitaweza ku- cure mapungufu yaliyomo kwenye IGA,Kwani IGA ndo mkataba mkubwa
Aliongelea wajibu na haki kuwa sawa, kitu ambacho hakiwezekani kwenye uwekezaji huu wa DP World.

Hii ni biashara inayokuja kutoka Dubai kuwekezwa hapa Tanzania, Prof Shivji aliongea katika mazingira ya uwepo wa usawa kibiashara kitu ambacho hakipo katika hii biashara.
 
Kwa hiyo akina Mbowe pia wakae kimya?
Assad amesoma Accounts and Finance, ambapo ni lazima wasome business law
Huyu aungane na wale mawakili 10 wa Kiislamu wawe upande wa dini. Hili suala la DP World kulitetea ni kujishushia hadhi tu, Assad heshima yake itashuka muda si mrefu.
 
Aliongelea wajibu na haki kuwa sawa, kitu ambacho hakiwezekani kwenye uwekezaji huu wa DP World.

Hii ni biashara inayokuja kutoka Dubai kuwekezwa hapa Tanzania, Prof Shivji aliongea katika mazingira ya uwepo wa usawa kibiashara kitu ambacho hakipo katika hii biashara.
Suala hata la longevity ya Mkataba Mkubwa(IGA) na issue ya Ownership ya Land,unategemea kwenda kui- cure vipi kwenye mikataba midogo if the other party ata- turn hostile na kung' angana na huo mkubwa? Hiyo si ndo maana jamaa wa opposition wana-justify kwamba mpaka hapo bahari itakapokauka ndo shughuli za DP World zitakoma.
 
Umesema vema mkuu, Je linapokuja suala la sheria azungumze mtaalamu wa uchumi au sheria?
Kwa masuala ya kisheria mazito wazungumze wanasheria wenye ueledi mkubwa wa kisheria lakini kama swali lako linahusiana na hili suala la uwekezaji wa bandari basi sio suala zito sana la kisheria ndio maana limechambuliwa na Mbowe ambaye hana taaluma ya kisheria na Kuna wengine waliona uchambuzi wa Mbowe ni Zaidi ya hata wa Prof.Shivji
 
Hawa ndio wamesoma wakaelimika, wale wengine husoma na kufaulishwa so hawaelimiki
 
Profesa Assad husimama kwenye ukweli sio mtu wa kuyumbishwa. Shivji na wenzake hawajawahi kuiunga mkono serikali yoyote ya CCM. Kinachonisikitisha ni nyumbu kuanza kumrushia maneno ya hovyo Profesa Assad.
Kumbe unatafuta wanaounga mkono CCM?
 
Amelewa sifa, alisifiwa sana sasa anajiona yeye ndio mjuvi wa kila kitu.
 
Back
Top Bottom