Tafuta popote nilipowahi kusema wastaafu wamesusa. Nilitarajia ungeniambia tija ya hao wazee kuwepo kwenye hizo hafla, mfano Melecela na umri alio nao na hali yake kiafya. Ni kweli JK alikuwa anafuja fedha za umma kwa safari zisizo na tija huko ng'ambo, je hiki kinachoendelea sasa chini ya awamu ya tano ukiacha style ya ufujaji, tofauti ya ufujaji iko wapi?
Hivi safari za JK hazikuwa na Tija kwa taifa.
Hapo ndipo tunapomkosea sana Mzee wetu Kikwete.
Safari zake ziliingiza mabilioni ya fedha.
Hivi MTU akitumia mfano milioni Mia moja kwa safari kisha akapata marafiki nchi ikaingiza bil. 20 hiyo sio tija.
Wakaja watalii maarufu wakaingiza mabiliona ya fedha na mahoteli yetu yakaingiza fedha n.k. Hiyo siyo tija kwa nchi?
Kuna wakati mmoja walikua maraisi wastaafu wa Marekani na Obama akiwa madaraka ni unategemea ugeni wao uliingizia taifa na wafanyabiashara Sh .ngapi?
Unafikiri mzunguko wa fedha unaweza kuwa mkubwa kama fedha tunazotegemea ni hizi hizi za kodi za wafanyakazi na vitambulisho vya machinga na wafanyabiashara kukadiriwa kodi ya kuwafilisi?
Huoni kuwa Kuna tija kubwa kwa safari za JK ndio maana kwa miaka kumi deni la nchi halikuwa kubwa kama miaka mitano isiyo na safari za nje na deni limekua Mara mbili.?
Wakati JK alisafiri sana lakini wafanyabiashara wadogo wengi na wamiliki wa ardhi na nyumba hawakulipishwa kodi lakini bado Aliweza kuajiri,kupandisha mishahara ,kujenga Kambi za Jeshi nchi nzima,kujenga mabarabara na Madaraja, kununua ndege za Jeshi na vifaa vya Jeshi. Kununua Manowari za Jeshi. Kujenga Bomba la Mafuta toka Mtwara mpaka DSM.
Kujenga vyuo vikuu na mahospitali makubwa yenye madaktari na vifaa kama MRI na CT Scani n.k.
JK ndiye aliyeanziasha EFD machine kwa ajili ya ushuru na faini za barabarani.
JK ndiye alitenunua mavipimo ya Kasi za magari barabarani. Terminal 3 ilianza kujengwa na JK. Wakati huo huo hakuwaumiza wafanyabiashara wala wanasiasa wa vyama vya upinzani. Mlitaka Tija gani tena kwenye safari zake ambazo zilimfanya awe kiongozi mstaarabu duniani?
Vita kuu ya kumbeza ,kumchafua na kumtukana JK ilikua inapangwa na Watu walikua wamejiandaa kwa muda mrefu sana kuiteka jamuhuri ya muungano kuwa ni himaya yoa ya kujipatia Vyeo na kuvikalia wao wenyewe kwa manufaa yao.
JK alitoka kabila dogo lisilo na watu wenye Elimu kubwa ya kuweza kuteka kila idara na kujijenga kipropaganda.
Pia dini yake ilikua ni sababu ya kumjengea fitina kila alipojaribu kuweka usawa mana waliotegemea kujimilikisha madaraka walijijuta wanakosa nafasi ili pawe na balance jambo lilololeta fitina na majungu.
Lakini JK aliiacha nchi hii ikiwa kwenye uchumi mzuri sana.