Rais Magufuli: Nataka nimwambie Mheshimiwa Kassim, kazi ya uwaziri mkuu haina 'guarantee'

Rais Magufuli: Nataka nimwambie Mheshimiwa Kassim, kazi ya uwaziri mkuu haina 'guarantee'

Kwani hapo tatizo liko wapi?Wakosoaji mmekosa vitu vya kukosoa
 
Nilikuwa hapa Singida nikielekea Mwanza. Niliamua kusimama kwa muda mchache kufuatilia hotuba ya Rais Magufuli baada ya kumuapisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. Katika maneno mengi aliyozungumza, nimebeba yafuatayo:

Yes tufanye kazi. Turuhusu watu serious wa nje waje kuwekeza. TRA waache kuua biashara kwa kulazimisha kodi zisizostahili.
Mwisho wa yote, nchi itajengwa na sisi wananchi. Muda wa longolongo umepita. We all need each other for propelling forward our mother land
 
Pamoja na Rais kusema wabunge wote ni super, tukubaliane na rais kwamba uwaziri ni kazi ya watu makini. Kuna kipindi tumekuwa tukijiuliza kwamba ilikuwaje au inakuwaje watu hawa ni mawaziri. Kwa uwaziri, inatakiwa rais uoneshe uangalifu wako na niya yako kwa wananchi. Uwaziri isiwe ni nafasi ya shukrani.
 
1605521398964.png

“Mpango umesema Mkeo anakupa raha, mwaka huu hakuna cha raha sana, Waziri Mkuu umesema unampa raha Mkeo mwaka huu hakuna raha, kwasababu hata Mimi sipati raha sana kwa Mke wangu, mlikuwa mnamuona Makamu wa Rais anazunguka kila siku unafikiri alikuwa anapata raha kwa Mume wake?, ni kuchapa kazi, lazima tuteseke Wananchi wapate raha”-JPM Ikulu ya Chamwino Dodoma leo.
 
Tafuta popote nilipowahi kusema wastaafu wamesusa. Nilitarajia ungeniambia tija ya hao wazee kuwepo kwenye hizo hafla, mfano Melecela na umri alio nao na hali yake kiafya. Ni kweli JK alikuwa anafuja fedha za umma kwa safari zisizo na tija huko ng'ambo, je hiki kinachoendelea sasa chini ya awamu ya tano ukiacha style ya ufujaji, tofauti ya ufujaji iko wapi?

Hivi safari za JK hazikuwa na Tija kwa taifa.

Hapo ndipo tunapomkosea sana Mzee wetu Kikwete.

Safari zake ziliingiza mabilioni ya fedha.
Hivi MTU akitumia mfano milioni Mia moja kwa safari kisha akapata marafiki nchi ikaingiza bil. 20 hiyo sio tija.
Wakaja watalii maarufu wakaingiza mabiliona ya fedha na mahoteli yetu yakaingiza fedha n.k. Hiyo siyo tija kwa nchi?

Kuna wakati mmoja walikua maraisi wastaafu wa Marekani na Obama akiwa madaraka ni unategemea ugeni wao uliingizia taifa na wafanyabiashara Sh .ngapi?

Unafikiri mzunguko wa fedha unaweza kuwa mkubwa kama fedha tunazotegemea ni hizi hizi za kodi za wafanyakazi na vitambulisho vya machinga na wafanyabiashara kukadiriwa kodi ya kuwafilisi?

Huoni kuwa Kuna tija kubwa kwa safari za JK ndio maana kwa miaka kumi deni la nchi halikuwa kubwa kama miaka mitano isiyo na safari za nje na deni limekua Mara mbili.?

Wakati JK alisafiri sana lakini wafanyabiashara wadogo wengi na wamiliki wa ardhi na nyumba hawakulipishwa kodi lakini bado Aliweza kuajiri,kupandisha mishahara ,kujenga Kambi za Jeshi nchi nzima,kujenga mabarabara na Madaraja, kununua ndege za Jeshi na vifaa vya Jeshi. Kununua Manowari za Jeshi. Kujenga Bomba la Mafuta toka Mtwara mpaka DSM.

Kujenga vyuo vikuu na mahospitali makubwa yenye madaktari na vifaa kama MRI na CT Scani n.k.

JK ndiye aliyeanziasha EFD machine kwa ajili ya ushuru na faini za barabarani.

JK ndiye alitenunua mavipimo ya Kasi za magari barabarani. Terminal 3 ilianza kujengwa na JK. Wakati huo huo hakuwaumiza wafanyabiashara wala wanasiasa wa vyama vya upinzani. Mlitaka Tija gani tena kwenye safari zake ambazo zilimfanya awe kiongozi mstaarabu duniani?

Vita kuu ya kumbeza ,kumchafua na kumtukana JK ilikua inapangwa na Watu walikua wamejiandaa kwa muda mrefu sana kuiteka jamuhuri ya muungano kuwa ni himaya yoa ya kujipatia Vyeo na kuvikalia wao wenyewe kwa manufaa yao.

JK alitoka kabila dogo lisilo na watu wenye Elimu kubwa ya kuweza kuteka kila idara na kujijenga kipropaganda.

Pia dini yake ilikua ni sababu ya kumjengea fitina kila alipojaribu kuweka usawa mana waliotegemea kujimilikisha madaraka walijijuta wanakosa nafasi ili pawe na balance jambo lilololeta fitina na majungu.

Lakini JK aliiacha nchi hii ikiwa kwenye uchumi mzuri sana.
 
Yaani Kabudi anamuabudu Magufuli.
Anajilinganisha miaka zaidi ya 20 aliyotumikia idara nyingine na Miaka mirano ya Ubilionea aliupata baada ya kuwa waziri anaona ni kama Ardhi na Mbingu. Ana kila sababu ya kumtukuza mtu aliyempa fursa ya kuyabadili maisha yake kwa muda mfupi sana.

Madaraka Afrika ni kila kitu .
 
Anajilinganisha miaka zaidi ya 20 aliyotumikia idara nyingine na Miaka mirano ya Ubilionea aliupata baada ya kuwa waziri anaona ni kama Ardhi na Mbingu .
Ana kila sababu ya kumtukuza mtu aliyempa fursa ya kuyabadili maisha yake kwa muda mfupi sana.

Madaraka Afrika ni kila kitu .
Ila kweli Ualimu wa chuo kama hauna vimiradi na unategemea mshahara tu ,ni umaskini kabisa.
 
Mabeberu hawana haraka wanajua magombe kama hayajapigwa bakora hayaondoki ,magombe mara hii lazima watajua kuongoza njia.
 
Ni kwa vile humu vijana ni wengi. Tangu baada ya uchaguzi wa vyama vingi mawaziri wakuu wote walipita bila kupingwa.

2000 sumaye alipita bila kupingwa
2005 Lowassa alipita bila kupingwa
2010 Pinda alipita bila kupingwa
2020 Kassim kapita bila kupingwa
Rushwa na ahadi za vyeo.

Hakuna kingine. Tatizo bado hatujawa na tume huru na katiba inayompunguzia mungu wa wapenda vyeo madaraka makubwa.

Lakini pia CCM bado imehodhi kila kitu mpaka vyombo vya dola hivyo mtu akikataa rushwa basi anaweza akapoteza kila kitu ikiwemo uhai wake na anayeua mpinzani wa CCM mara nyingi hahesabiwi dhambi na mungu wa madaraka hivyo ni bora mtu ajitoe na malaika wa miungu wa madaraka wapite bila kupingwa.

Kabudi ni lazima aabudu na kusifu mana anakumbuka magwiji wa sheria na katiba kama akina Prof. Chachage, Prof. Mwakyusa na Dr .Mvungi walivyozimika kama mshumaa kwenye mvua ya masika.

Kama Prof. Wa Chuo Kikuu anaishi maisha kama mtu anayekaa Jalalani ukilinganisha na Mbunge na Waziri basi ujue nchi yetu INA safari ndefu sana kupata ufalme wa Mungu.
 
Kwa waliosikiliza kilichosemwa leo tayari serikali ya CCM na viongozi wake wapo mguu ndani mguu nje. Wanaondoka na tuseme wanaondolewa au neno zuri la kikwetu wanafurushwa na haizidi mwaka.

Kilichosemwa leo kwa ufupi wana uhakika gani kama watamaliza miaka mitano? Akili kichwani mwako ongeza za kuchagiwa.
 
Back
Top Bottom