Rais Mstaafu Jakaya Kikwete: Msijaribu Kuchanganya Dini na Siasa Hata Kidogo
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka Watanzania kuwanyanyapaa na kuacha kuwasikiliza Viongozi wa dini au Viongozi wa siasa wanaotaka kuitumia dini kwa manufaa yao ya kisiasa kwa sababu ni kitu hatari kwa tunu ya amani na utulivu na iwapo tunu hiyo itavunjwa basi gharama yake itaonekana.

Mstaafu Kikwete ameyasema haya leo kwenye uzinduzi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Charya Kamageta Wilayani Rorya mkoani Mara na hizi ndio nukuu zake.

"Natumia nafasi hii kukumbusha kuhusu tunu nyingine muhimu nayo ni kutokuchanganya dini na siasa tukiivunja tunu hii gharama yake tutaiona, kama kuna Viongozi wa dini wanaotaka kutuelekeza kuitumia dini kwa manufaa ya kisiasa na kama kuna Viongozi wa siasa wanataka kuitumia dini kwa manufaa yao ya kisiasa nawaombeni tuwanyanyapae, siku ikifika Uanachama wa Chama cha siasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na Chama cha siasa anachokifuata ndio mwisho wa Nchi yetu”

"Mtakuwa na Vyama vya siasa vya Wakristo, Vyama vya siasa vya Waislamu, vya Walokole , Vyama vya siasa vya Watu gani, kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, utawala na kiserikali kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari, pia Watu kutazama masuala ya dini kwa mtazamo wa siasa za Vyama vyao sio jambo lenye afya kwa Taifa letu, yote mawili yataathiri umoja na kutishia amani na utulivu tunaoufaidi hivi sasa”

"Zanzibar walifika mahali Waislamu wanamuona Sheikh ambaye ni Mfuasi wa Chama ambacho sio chake sio Sheikh sawasawa kwahiyo wakienda kuswali kama Sheikh ni Mfuasi wa CUF wanangoja amalize kusalisha halafu anaingia Sheikh wa CCM na Wafuasi wake ndio maana nilipokuwa Rais nilipambana sana kupata ule mwafaka Zanzibar”

My Take
Tamko la Kikwete ni la kimkakati. Kupigania bandari yetu sio siasa. Amechochea kuni kwenye hizi harakati
Kikwete, stop that nonsense. Nyinyi mnaojiita viongozi mnatuibia, mnakosa maadili , nyie ndio watu hatari. Wewe umeiba mpaka basi, leo unaleta porojo. Ikibidi dini zitumike tuwaondoe msituibie.
 
Alikuwa aliongea Leo huko Mara alikoalikwa kama mgeni Rasmi kwenye sherehe ya ufunguzi wa jengo la ibada la Kanisa.

My Take
Naunga mkono hoja,TEC na wachochezi wengine wakemewe na waonywe.

=====

"Tukianza kuchanganya dini na siasa, tukageuza...madhabahu ndio mahali pa kuhubiri siasa za vyama vya siasa, kwishiria mbali nchi yetu...lakini Baba wa Taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa, nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni za jicho letu tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo vya aina hii iwe kwa siri au kwa dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya" Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Jakaya Kikwete wakati akizindua kanisa la SDA Rorya mkoani Mara, leo Agosti 20, 2023.

View attachment 2722951
Acha utapeli. Hii speech ni ya miaka 14 iliyopita. Labda kama hujamuona jk hivi karibuni
 
Alikuwa aliongea Leo huko Mara alikoalikwa kama mgeni Rasmi kwenye sherehe ya ufunguzi wa jengo la ibada la Kanisa.

My Take
Naunga mkono hoja,TEC na wachochezi wengine wakemewe na waonywe.

=====

"Tukianza kuchanganya dini na siasa, tukageuza...madhabahu ndio mahali pa kuhubiri siasa za vyama vya siasa, kwishiria mbali nchi yetu...lakini Baba wa Taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa, nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni za jicho letu tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo vya aina hii iwe kwa siri au kwa dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya" Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Jakaya Kikwete wakati akizindua kanisa la SDA Rorya mkoani Mara, leo Agosti 20, 2023.

View attachment 2722951
bandari inahitaj siasa ? yaan kwa akili yako na kikwete ndio maana mnaiingiza nchi shimon , kwamba viongoz wa dini wakitoa maoni wamefanya siasa ? ww ukitoa maoni umefanya siasa ? hv hoja hizo 8 za hao TEC ni za uongo ? bado wajinga ndo mtaji wa ccmu , mtu anajielewa haez sema kutoa maoni ni kifanya siasa
 
"Napenda kuchukua nafasi hii kukumbushana kuhusu tunu nyingine muhimu nayo ni kutokuchanganya dini na siasa. Tukiivunja tunu hii gharama yake tutaiona, na kama kuna viongozi wa dini wanataka kutuelekeza kuitumia dini kwa manufaa ya kisiasa, na kama kuna viongozi wa siasa wanataka kuitumia dini kwa manufa yao ya kisiasa, nawaombeni ndugu zangu tuwanyanyapae.

"Siku ikifika ambapo uwanachama wa chama cha siasa au uumini thabiti wa dini ukawianishwa na chama cha siasa kinachofuata ndio mwisho wa nchi yetu, mtakuwa na vyama vya siasa vya wakristu, waislamu, walokole nk. Kuwafanya Watanzania kuyatazama masuala ya kisiasa, kiserikali, utawala kwa mtazamo wa dini zetu ni jambo hatari, halkadhalika watu kuyatazama masuala ya dini kwa mtazamo wa siasa za vyama vyao si jambo lenye afya kwa taifa letu.

"Yote mawili yataathiri umoja na kutishia amani, usalama na utulivu tunaoufaidi hivi sasa. Mfano Zanzibar walifika mahali waisilamu wanamuona shehe ambaye ni mfuasi wa chama ambacho sio chake sio shehe sawa sawa, kwahiyo wakienda kusali kama shehe ni msuasi wa CUF wanangoja amalize kusalisha, halafu anaingia shehe wa waislamu na wafuasi wake.

"Nawaambia vitu halisi na ndio maana nilipokuwa Rais nilishughulika sana pale na kupata muafaka, niliahidi kwenye hotuba yangu ya kwanza ya Bunge 2005 Dec 30, kwamba nitafanya kila ninaloweza tujenge muafaka Zanzibar, haukuwa rahisi. Mkutano ule tuliufanyia Butiama NEC, ilikuwa moja ya kikao kigumu kwelikweli, lakini nikasema pamoja na ugumu wote lazima hapa tuvuke. Tukafika mahali nilipoona mambo yamekuwa makali, nikasema twendeni kwanza tukale, tulipokuwa tunakula ndio tukawa tunaweka mikakati ya namna gani tunalimaliza hili jambo. Tukajipanga nani ataanza kuzungumza, tukakubaliana kwamba tutakwenda Zanzibar kuwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa, na ndio imetusaidia Zanzibar tuna mazingira ya utulivu mpaka sasa, tungekwenda na utaratibu ule ule wa zamani tusingefika.

"…Tukianza kuchanganya dini na siasa tukageuza mimbari za dini na madhabahu kuwa sehemu ya kuhubiri kwishilia mbali nchi yetu. Lakini baba wa taifa ametuasa juu ya hatari ya kuchanganya dini na siasa. Nawasihi Watanzania wenzangu kuitunza tunu hii kama mboni ya jicho letu. Tukatae kuwasikiliza viongozi wa dini na waumini wao wanaofanya vitendo wa aina hii iwe kwa siri au kwa Dhahiri, vitendo hivi vinaweza kutupeleka kubaya."

Kikwete ameyasema hayo leo 20/8/2023 katika ufunguzi wa jengo Kanisa la Kiadventisti Wasabato Mara.
Angemwambia Mama alivyoingia tu akakataa kusalimia Wakristo ila Salamaleko anasema na kuitikia,
 
Kikwete si ni Mwanasiasa? Mbona kaenda kusimama kwenye Jukwaa la Dini na kumhubiri Mungu? Au hiyo siyo kuchanganya dini na siasa?
Kwani yeye JK tangu sakata hili linaanza mpaka mashehe wale ubwabwa walikuwa wanaongelea huu mkataba, mbona hakuja hadharani kukemea hilo la kuchanganya  siasa   na  dini ?? Alikuwa wapi mpaka amesikia tamko la waRoma ndio anaamka?? Wasifanye wa Tz wajinga.
 
Ninaunga mkono hoja udini kwa namna yoyote ile kwenye siasa si mzuri bora ya sisi wapagani. nimesikia mashehe wakizungumza bandari kwa mlengo wa kidini, maaskofu,wachungaji nk wote pamoja na hoja zao nzuri kuhusu madhaifu ya makubaliano/mkataba bado inafungamanishwa na udini na kipindi fulani utanganyika/unzanzibari. Ni kweli mkataba una mapungufu tuujadili wenywe kama wenyewe na serikali ichukue hatua za maboresho ili tubaki na umoja wetu. Umoja kwanza bandari baadaye.
ccmu ndo wanalifanya hilo jambo kufikia huko , tangu hawali walipoambiwa ilibid wajue watu wamestuka na wangerekebisha mapema basi hat tusingefikia huku , kuona maprofesaa na viongoz wa dini wanalijia juu , maana yake wameona kiburi cha Samia ambae anashauliwa ila kakaza shingo , yaan hapa nchi ikiingia vitan mnasingizia wazungu , upumbav kama huu hata Ghadaf na Assad waliufanya ona nchi zao zilipo sasa hv , Samiah anatupeleka huko huko , yeye hajali kikubwa yeye bado ni rais bas kwake inatosha , adui wa taifa ni Samiah wala sio hao masheikh maana hao wanatumia upumbav wa kiongoz wa nchi
 
Leo ndio amekumbuka maneno ya baba wa taifa?

Kukemea rushwa iliyosababisha bandari zetu zikatolewa bure milele kwa mwarabu hakuwezi hata siku moja kuwa kuchanganya dini na siasa.

Hayo maneno kuchanganya dini na siasa hutumiwa na wanasiasa ili wapate uwanja mzuri wa kufanya michezo yao haramu kwa manufaa yao, na sio manufaa ya watanganyika.

Siasa inahusisha watu, na dini zinahusisha watu hao hao, hawa hawatenganishiki, tendeni mema kwa wananchi wenu mkae kwa amani, kinyume na hapo lazima muambiwe ukweli.
Nyie ni watu hatari sana kwa amani ya nchi hii.
 
Ndo nia yenu kumbe? Sasa sikiliza. Samia ndo Rais wako hadi 2030. Wafikishie salamu wenzako
ww ni mpumbav badala ya kuangalia ukwel au uongo kti hoja za hao TEC , ww unaangaika na wasifu wao , masheikh wameongea sana , iweje TEC walipotoa hoja za msingi wao waonekane wanachanganya dini na siasa , je masheikh wao hawachangany dini na siasa , endelea kulala chumba kimoja na shetan mudan ukifika atakukula ww , si unazan mpo safari moja kisa wote wa rangi moja [emoji23]
 
JK leo amepanda gari jioni.

Tamko limeshasomwa Nchi zima anaibukia Mara!!!

Siku zote alipiga kimyaaaaa!!!

Sasa Tamko linasomwa anaanza hotuba ambayo imeshakuwa overtaken by event.

Suala la bandari sio siasa wala dini ni raslimali za Tanganyika ( zawananchi).
 
Upumbavu mtupu, alikuwa wapi wakati mchi inauzwa?

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Cha kushangaza na kusikitisha zaidi, yeye siyo padri wala mchungaji bali ni mwanasiasa lakini kahudhuria kwenye tukio la watu wa dini na kaongelea mambo ya kisiasa.
Watu wa siasa wana dini zao na siasa ni maisha ya watu...
 
ww ni mpumbav badala ya kuangalia ukwel au uongo kti hoja za hao TEC , ww unaangaika na wasifu wao , masheikh wameongea sana , iweje TEC walipotoa hoja za msingi wao waonekane wanachanganya dini na siasa , je masheikh wao hawachangany dini na siasa , endelea kulala chumba kimoja na shetan mudan ukifika atakukula ww , si unazan mpo safari moja kisa wote wa rangi moja [emoji23]
Umeshawahi kuniona nikiunga mkono matamko ya kidini humu?
 
Haya sasa , msichanganye dini na siasa🤣
 
Attachments

  • C43C4D23-FF95-4CFF-A93B-BFC963AF6F81.jpeg
    C43C4D23-FF95-4CFF-A93B-BFC963AF6F81.jpeg
    25 KB · Views: 1
  • 736403F3-1C00-4708-B016-875DE3556359.jpeg
    736403F3-1C00-4708-B016-875DE3556359.jpeg
    39.8 KB · Views: 1
Cha kushangaza na kusikitisha zaidi, yeye siyo padri wala mchungaji bali ni mwanasiasa lakini kahudhuria kwenye tukio la watu wa dini na kaongelea mambo ya kisiasa.
Watu wa siasa wana dini zao na siasa ni maisha ya watu...
Kikwete ni hopeless hana uwezo wa kudeal na mambo mazito
 
Cha kushangaza na kusikitisha zaidi, yeye siyo padri wala mchungaji bali ni mwanasiasa lakini kahudhuria kwenye tukio la watu wa dini na kaongelea mambo ya kisiasa.
Watu wa siasa wana dini zao na siasa ni maisha ya watu...
 
Attachments

  • 33D4BE9C-7BE3-43C6-86B7-C35BD66E4D13.jpeg
    33D4BE9C-7BE3-43C6-86B7-C35BD66E4D13.jpeg
    25 KB · Views: 1
Back
Top Bottom