Beatrice Kamugisha
JF-Expert Member
- May 18, 2019
- 762
- 6,984
Rais ametangaza rasmi kwamba wanawake watakuwa na kazi yakumpata Rais mwanamke 2025 means kwa kauli hii amewaambia chama chake kwamba mgombe atakuwa mwanamke aidha yeye au mwanamke mwingine. Hii inatoa tafsiri ya wazi kwamba wanaume kwa upande wake awataruhusiwa kupambana na mwanamke atakayepitishwa hivyo kwa kukuwa yeye ni Mwenyekiti wa chama mapinduzi, wanaume wote waliotamani kugombea nafasi ya Urais 2025 kupitia chama hicho waanze kutafuta kazi nyingine yakufanya vinginevyo Mwenyenzi Mungu afanye miujiza.
Kwa upande wa pili, kauli hii haiwezi kuwa na nguvu upande wa upinzani kwa sababu wao bado wanao mfumo wao wakupata wagombea Urais. Mfumo huo haufungwi na kauli za Rqis, lakini pia kwakuwa ametangaza adharani na kwa nafasi yake maana yake kampeni za uchaguzi 2025 zimeanza rasmi leo.
Nasema zimeanza rasmi leo kwa sababu muda si mrefu kila atakayekuwa anasimama jukwaani atakuwa anampigia chapuo mwanamke wa 2025, hii kauli ni maelekezo kwa Mawaziri ,wabunge wa CCM na wengine wote ambao wanaishi kwa kasababuu ya uteuzi qa Rais na serikali iliyopo. Kampeni hizi naamini na natabiri zitamabtana na nyimbo, zitaambatana na matangazo kwenye vyombo vya habari na zitaambatana pia wale wanaopinga agizo hili au wanaoonekana kutaka kuwa na nguvu zaidi ya mwanamke kuwajibishwa.
Ni muda Sasa vyama vya upinzani navyo kuanza KUJIANDAA kuanzia ngazi ya mtaa kuwashawoshi wapiga kura ambao kwao wao hawachagui jinsia Bali wanachagua kiongozi. Kwamba tuchague jinsia hii haitaweza kuwa agenda kwa wananchi 2025 Bali agenda itakuwa maji, elimu, demokrasia, katiba, afya na mapambano ya tozo zinazouma.
Kuendelea na kauli mbiu ya kuacha siasa tufanye maendeleo wakati upande mmoja unafanya siasa na kuandaa wagombea pamoja na kuwanadi nikuendeleza ukandamizaji ambao haitakuwa na tija kwa Taifa Bali utakuwa na tija kwa huyo Mwanamke anayeamini kupata urais bila democracy.