Rais Samia: Hatukutoa fursa ya Mikutano ya hadhara watu wakavunje sheria, wasimame kutukana, kukashifu na kuchambua dini za wengine

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama va Siasa na Wadau wa Demokrasia katika ukumbi wa JNICC leo tarehe 11 Septemba, 2023 katika viwanja vya Ikulu, jijini Dares Salaam.

Kituo cha TCD kinafanya kazi vizuri tangu Rais Samia aingie madarakani, na ndie amekipa uhai. TCD ilifanya mkutano na wadau kujadili hali ya demokrasia kuelekea chaguzi za 2024 na 2025, baada ya kujadili kuna mambo tulifanyia maazimio na tutayaleta hapa.

Kuhusu Katiba, mchakato wa kupata katiba mpya uweze kuendelea, lakini kwa muda uliopo huenda tunaweza tusipate Katiba Mpya. Lakini mabadiliko ya katiba yanaweza kufanyika ikiwemo kufanya mabadiliko kifungu cha 74 cha Katiba ili tume huru iweze kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

Pawepo mgombea binafsi, kufanyia marekebisho kifungu cha 39 (2) cha katiba ya sasa kuhusu Rais na kifungu cha 67(1) kuhusu wagombea ubunge. Kuwa Rais tangazwe akishinda kwa zaidi ya 50% ya kura kwa hiyo kurekebisha kifungu cha 41 (6) na uchaguzi wa Rais uweze kuhojiwa mahakamani hivyo kubadilisha kifungu cha 41 (7).

Hii nchi ni kama vile tumelogwa na tuna utawala uliobatilka, hakuna baraka katika nchi! Ardhi ina laana na viongozi hawana kibali cha Mungu katika kutuongoza.

Karibu nchi nzima tuna tatizo la nishati ya mafuta na umeme kwa muda sasa, Badala Rais akae chini na watendaji kufahamu mbivu na mbichi badala yake kila kukicha anawaza namna gani ya kupooza upinzani huku akiwa hana hata uwezo wa kuongoza nchi, .

Wananchi tumeshachoka.
 
Mnafiki sana huyu mama! Afu anadhani wa TZ wote ni wajinga!
Samia is using delaying tactics so that no meaningful legislation can take place before local and the general elections take place.
Haifanyi kazi ya kuongoza nchi; akili yake yote iko kwenye jinsi atakavyofanikiwa kupata muhula wake mwenyewe wa kutawala! Mungu atuepushe na hili balaa lingine.
 
Hii nchi ni kama vile tumelogwa na tuna utawala uliobatilka, hakuna baraka katika nchi! Ardhi ina laana na viongozi hawana kibali cha Mungu katika kutuongoza.

Karibu nchi nzima tuna tatizo la nishati ya mafuta na umeme kwa muda sasa, Badala Rais akae chini na watendaji kufahamu mbivu na mbichi badala yake kila kukicha anawaza namna gani ya kupooza upinzani huku akiwa hana hata uwezo wa kuongoza nchi, .

Wananchi tumeshachoka.
Fanya kazi mkuu hakuna wa kukuletea ugali nyumbani,kulalama hakujawahi kumsaidia mtu kwa lolote!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama va Siasa na Wadau wa Demokrasia katika ukumbi wa JNICC leo tarehe 11 Septemba, 2023 katika viwanja vya Ikulu, jijini Dares Salaam.

Kituo cha TCD kinafanya kazi vizuri tangu Rais Samia aingie madarakani, na ndie amekipa uhai. TCD ilifanya mkutano na wadau kujadili hali ya demokrasia kuelekea chaguzi za 2024 na 2025, baada ya kujadili kuna mambo tulifanyia maazimio na tutayaleta hapa.

Kuhusu Katiba, mchakato wa kupata katiba mpya uweze kuendelea, lakini kwa muda uliopo huenda tunaweza tusipate Katiba Mpya. Lakini mabadiliko ya katiba yanaweza kufanyika ikiwemo kufanya mabadiliko kifungu cha 74 cha Katiba ili tume huru iweze kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

Pawepo mgombea binafsi, kufanyia marekebisho kifungu cha 39 (2) cha katiba ya sasa kuhusu Rais na kifungu cha 67(1) kuhusu wagombea ubunge. Kuwa Rais atangazwe akishinda kwa zaidi ya 50% ya kura kwa hiyo kurekebisha kifungu cha 41 (6) na uchaguzi wa Rais uweze kuhojiwa mahakamani hivyo kubadilisha kifungu cha 41 (7).

JENISTA MHAGAMA, WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE NA URATIBU)
Amemshukuru Rais Samia kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huu.

Kwenye siku tatu za Mkutano huu, wajumbe watashiriki kujadiliana ni namna gani taifa letu litaimarisha na kuboresha demokrasia hapa nchini.

Pia, tathimini ya maoendekezo ya kikosi kazi yatajadiliwa kwenye mkutano huu.

Rais Samia amedhihirisha kuwa ni kiongozi anayezingatia utawala bora na kutenda haki kwa watanzania wote.

SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Leo tunapokutana na kuzungumza mapendekezo ya kikosi kazi ni mapendekezo ambayo wote wadau wa siasa nchini wameyaleta kwa pamoja.

Tutapishana tu kwa jinsi ya kusukuma utekelezaji, huyu anataka kalileta leo lifanywe kesho, mwingine ana subira kidogo, lakini wote maono yetu ni kama yanaenda pamoja.

Tayari Serikali imeanza kuchukua hatua ya baadhi ya mapendekezo ya kikosi kazi na mnayajua, kwa mfano kuruhusu Mikutano ya hadhara, tayari imeruhusiwa watu wanakwenda na tunawasikia yanayosemwa huko.

Lakini pia tulishauriwa kuunda kanuni za kuendesha hiyo mikutano ya hadhara, zimeundwa na zinatekelezwa, hilo limeshafanyika.

Lakini pia kuna jambo mahsusi ambalo ndio kila mtu analisubiri la katiba, marekebisho ya katiba yetu ambalo nalenyewe limeanza kufanyiwa kazi na pengine mkutano huu ni kuelekea huko pia.

La mikutano ya hadhara, tumeruhusu tukiwa na nia ya vyama vya siasa vizungumze wananchi wasikie sera zao, mada zao, mipango yao ili vyama vikue na virudishe watu wale walio wapoteza, vyama visimame, viwe madhubuti, tukienda kwenye uchaguzi kila chama kimejijenga vya kutosha na ndio maana ya kutoa fursa hii ya mikutano ya hadhara.

Hatukutoa fursa ile watu wakavunje sheria, watu wakasimame kutukana, watu wakasimame kukashfu, watu wakasimame kuchambua dini za watu. Lakini sishangai kwanini haya yanatokea, kwa sababu ya kuzungumzwa hakuna.

Tulianza na katiba, tukaenda ikakatika katikati, bandari imeenda sasa katiba tena. Tumieni hiyo fursa kajijengeni kwa wananchi, elezeni sera zenu, mtafanya nini, ili wananchi warudi wawaunge mkono ili tukienda kwenye uchaguzi vyama vyote vimejijenga vizuri.

Uendeshaji wa Tanzania unahitaji fikra za kila mtu, hakuna mtu mwenye hati ya kuimiliki, hata kitoto kilichozaliwa yeye kina haki, ili tuendeshe vizuri kila kundi litoe mawazo tuendeshe nchi yetu.

Niseme tena, fursa hii iliyotoka isiende kuharibu neema na baraka aliyotupa Mungu. Isiende kuharibu misingi ya uendeshaji nchi hii wazee wetu waliyotuachia.

Lingine, hakuna aliye juu ya sheria. Kila anayefanya makosa sheria itamshika. Kama umekiuka sheria, sheria itakushika. Ajenda yetu kubwa kama watanzania ni kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Tulitoa uhuru wa maoni, maoni mengi sana yanatoka kwa watanzania, tunayaona, mazuri tunayachukua na mengine unayapima maoni yao. Nina kikundi maalumu kinachoangalia maoni yote maoni na kuchukua yale mazuri na kuyaweka kwenye mipango yetu kuyafanyia kazi.

Kuna uhuru wa maoni lakini huu uhuru wa maoni una mipaka yake, sio tu kisheria, hata kibinadamu.

Mama wakikuzingua piga pini mazima kama Mwendazake au watiwe korokoloni wanataka kukuzoea.
 
Yeye hajionu anavyovunja sheria ...
 
Back
Top Bottom