Rais Samia: Hatukutoa fursa ya Mikutano ya hadhara watu wakavunje sheria, wasimame kutukana, kukashifu na kuchambua dini za wengine

Rais Samia: Hatukutoa fursa ya Mikutano ya hadhara watu wakavunje sheria, wasimame kutukana, kukashifu na kuchambua dini za wengine

Huyu anaona kila kitu anachoambiwa asichopenda kusikia ni kutukana, kwa sababu hulka ya watu hawa ni ya kufanya mambo kiujanja ujanja, au kutumia laghai nyingi kupitisha wanayoyataka wao.

Anataka lugha za kuzungushana, huku akiendelea na mipango yake kwa kutumia ujanja.

Kashindwa kuzungumzia chochote kuhusu DP World, kwa sababu watu wamemwambia 'direct' ukweli wa upotofu anaoufanyia taifa kiujanjaujanja.

Mwishowe watu sasa wameelewa matumizi ya hadaa nyingi katika utendaji wake.
 
Kuna kiongozi mmoja alitoa kauli fulani kuhusu katiba kisha Mdude akampa za uso huko twitter halafu watu wakaanza kumshambulia kuwa ametumia lugha kali.

Sasa kwa matamshi ya Mama akiongea maneno kama ya huyo msaidizi wake kuhusu katiba, naona Mdude huwa yuko sahihi sana kwani hawa watu wanacheza na akili zetu na kufanya nchi nzima watoto.

Pia, Dr. Slaa nae alitumia lugha sahihi kwa hawa watu.

Katiba mpa haiwezi kupatikana hivi hivi ni lazima tuwe na maamuzi magumu.
 
Kwani wasomi wachache waliopo katika nchi hii hawatoshi kutoa maoni na katiba ikarekebishwa!?

Kwani si lilikuwa na Bunge La Katiba ili kutoa uwakilisho wa Watanzania wote!?

Alafu so ni yeye ndio aliliongoza Bunge lile!?

Kwanini ameongea maneno Yale.
Ehh!??
 
Hayo ni madhara ya kutopangilia maneno ya kuongea,kujenga hoja,kushawishi na kuzitetea.Hatari.Si wote tuna vipaji vya kuhutubia bila kusoma.Tumekosea.Na kujisahihisha au kuanza upya si ujinga.
 
Hayo ni madhara ya kutopangilia maneno ya kuongea,kujenga hoja,kushawishi na kuzitetea.Hatari.Si wote tuna vipaji vya kuhutubia bila kusoma.Tumekosea.Na kujisahihisha au kuanza upya si ujinga.
Hatuwezi kwenda hivi mpaka 2030...
Never.
We need an immediate change... Hapana.

Kama vipi mi nihame nchi. Sitaki Aibu hizi.
 
1. Utangulizi:

Mh. Mwenyekiti na Wajumbe,


Kama wengi wetu tunavyojua Kikosi Kazi cha Mh. Rais kiliundwa tarehe 23 Desemba 2021, kikiwa na wajumbe ishirini na nne (24). Kikosi Kazi kiliwasilisha mapendekezo yake kwa Mh. Rais tarehe Oktoba 21, 2022.

Kikosi kazi kilipitia hadidu za rejea, kikachambua hotuba za ufunguzi za Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kikachambua mapendekezo yaliyotolewa katika mkutano wa wadau huko Dodoma, kikapokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali, na hatimaye kuainisha na kuandaa mapendekezo baada ya kufanya kazi kwa mda wa miezi kumi. Mapendekezo haya yaliyowasilishwa kwa Mh. Rais na Watanzania wote kwa ujumla hapo Oktoba, 2022, Ikulu Dar es Salaam.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuokoa mda, ninawasilisha mapendekezo tu. Nayo ni haya yafuatayo:
2. Mikutano ya Vyama vya Siasa
2.1. Kuhusu mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa

Kikosi Kazi kilipendekeza kuwa:
Mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa iruhusiwe kufanyika kwa mujibu wa Katiba na Sheria;
Mikutano ya ndani ya vyama vya siasa iendelee kufanyika bila vikwazo vyovyote;
yafanyike marekebisho ya Sheria, ili kuhakikisha mikutano ya hadhara inafanyika kwa ufanisi. Sheria hizo ni pamoja Sheria ya Vyama vya Siasa Sura ya 258, Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi Sura ya 322 na Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa za Mwaka 2019.
 

Attachments

Kwani wasomi wachache waliopo katika nchi hii hawatoshi kutoa maoni na katiba ikarekebishwa!?

Kwani si lilikuwa na Bunge La Katiba ili kutoa uwakilisho wa Watanzania wote!?

Alafu so ni yeye ndio aliliongoza Bunge lile!?

Kwanini ameongea maneno Yale.
Ehh!??
Kwani unekatazwa kutowa maoni yako ya katiba?
 
Siku ya leo tarehe 11/9 umefanyika mkutano ambao Rais alitoa hotuba. Na asilimia kubwa Rais alitumia kujitetea dhidi ya uhuru wa mikutano ya Siasa, mabadiliko ya katiba na kadharika. Kazi ambayo ilitakiwa ifanywe na Chawa (Mataga).


View: https://www.instagram.com/p/CxDnxEbqY8f/?igshid=MzRlODBiNWFlZA==

Lakini wengine wanasema kuwa Machawa wanashindwa kutetea kwa sababu kiuhalisia hakuna kitu Rais anachofanya ambacho wanaweza kukitumia kama Weapon of destruction.

Ukizungumzia uhuru wa mikutano ya siasa, utabananishwa kuhusu Sakata la Tundu Lissu kule ngorongoro. Ukileta kwenye maendeleo utabananishwa na sakata la bandari, ukileta huduma za kijamii utabananishwa na Sakata la Petrol na Mgao wa umeme unaoendelea nchini. Ukileta mambo ya Uchumi utabananishwa kuhusu upungufu wa Dollar Nchini na kadharika. Bado swala la katiba na uchaguzi huru.

Hivyo kupelekea Mataga a.k.a Chawa wa Rais kukosa namna ya kumtetea kiongozi wao. Na mwishowe Rais inabidi ajitetee mwenyewe kwenye mikutano ya hadhara.
 
Back
Top Bottom