Haiwezekani kati ya rufaa 178 zilizopelekwa zilizoamuliwa na ofisi ya TUME YA UTUMISHI WA UMMA tena kwa kuchelewa, ni rufaa 5 tu ndizo zilizoshinda!!!

Tume ya Utumishi wa Umma inashirikiana na waajiri wasio na maadili kuwakandamiza na kuwanyima haki watumishi wa umma.

Mama President, kindly take up this matter seriously!!

Asante sana.
 
Lazima tuwe na sheria ya watu wanambambikia watu makosa,hivihivi yatajirudia..Bunge limelala,tungeni sheria,ili suala hamlioni???
 
Waizi watarudi mitaani Tu enzi zake zimefika
Chuki zaidi ya uhalisia. Ungekuwa na ndugu anayesota mahabusu kwa kesi isiyo na kichwa wala miguu usingesema haya. Ungekuwa na ndugu ambaye kosa lake ni kupiga kampeni tu na kisha kuwekwa mahabusu KWA kesi ya uhujumu uchumi usingesema haya.
 
... kumbe hii issue ya kubambika kesi nikajua ni polisi kumbe hadi TAKUKURU ipo? Dah; kwanini hao waliofungua hayo mafaili ya kubambika raia wema kesi wasitimuliwe na kushitakiwa? Huu ujinga utaendelea kutamalaki hadi lini!
Sio kama wanabambikiwa bali ushahidi ulipo ni hafifu kuwatia hatiani.
 
Kama jinsi Jeshi la Polisi linavyowabambika kesi raia basi ni hivyohivyo jinsi Waajiri waliokosa maadili wanavyowabambika kesi watumishi wao.

Na bada ta watumishi hao kupeleka malalamiko au kukata rufaa TUME YA UTUMISHI WA UMMA, Tume ya Utumishi wa Umma wa umma wanashindwa kufanya critical review ili kutoa the balanced conclusion bali wamekuwa wanaegemea upande wa mwajiri ili kumkandamiza Mtumishi wa Umma.

Asante.
 
Ndio maana inabidi raia wapiganie upatikanaji wa Katiba mpya itakayosimamisha mifumo imara katika nchi
Nchi ikikosa Rais mzuri mifumo yote inakuwa ya kishetani. Akina Igp siro leo wanafanya kazi kwa uhuru kwa mujibu wa sheria za nchi. Wametukosea sana kwa kushiriki maovu na vitendo vibaya wakati wa Ibilisi Jiwe.
 
kuzuia fao la kujitoa ni sheria kandamizi inabidi hili pia aliangalie kwa umakini. wengi wetu kazi zetu za mikataba inapoisha unateseka sana ni bora mtu achukue mafao yake akafanye biashara zake na kuachana na hizi ajira zenye mateso.
 
Nchi ikikosa Rais mzuri mifumo yote inakuwa ya kishetani. Akina Igp siro leo wanafanya kazi kwa uhuru kwa mujibu wa sheria za nchi. Wametukosea sana kwa kushiriki maovu na vitendo vibaya wakati wa Ibilisi Jiwe.
Yule kwangu sioni kama alikuwa binadamu wa kawaida. Binadamu gani anaona fahari watu kupigwa risasi, kuokotwa kwenye viroba, kupotezwa jumla, kudhalilisha watu hadharani n.k.
 
Sio kama wanabambikiwa bali ushahidi ulipo ni hafifu kuwatia hatiani.
... Rais kasema ni kesi za kubambika wewe unasema ni kesi zenye ushahidi hafifu sijui nani mjuvi kuliko mwingine.
 
Mama anataka kama wewe ni polisi tenda haki
Hakimu tenda haki
Takukuru tenda haki
Polisi tenda haki
NEC tenda haki.
 
... kumbe hii issue ya kubambika kesi nikajua ni polisi kumbe hadi TAKUKURU ipo? Dah; kwanini hao waliofungua hayo mafaili ya kubambika raia wema kesi wasitimuliwe na kushitakiwa? Huu ujinga utaendelea kutamalaki hadi lini!
Shida ipo kwa waliokwamia bado awamu,ile nawaliokubali kutekeleza mawazo ovu almuradi mkono uende kinywani,hao ni wakusaka na kufurushwa kwani wataendelea na uchafuzi na kutaka kuikwamisha nia njema iliyopo kwakuwa walinufaika,au kujinufaisha na mfumo walioupenda.
 
Lazima tuwe na sheria ya watu wanambambikia watu makosa,hivihivi yatajirudia..Bunge limelala,tungeni sheria,ili suala hamlioni???
Walikuwa mbio kuipitisha miswaada kandamizi waliyoona inamaslahi kwao kwa hati za dharura,ila zile za kulisaidia taifa haikupewa kipaumbele kwa hizo hati za dharura,kama za kuwadhibiti wa bambikia kesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…