Kuna uwezekano mkubwa wale masheikh wakaachiwa huru. Kwa trend na messaging hii ya mama.

Kama hakuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani wawaache huru tu.

Ingawa hili zigo hasa ni la JK na sio JPM.
 
Hawa TAKUKURU walinichefua siku wana gwaya kuwafungulia mashitaka wanasiasa walonaswa na rushwa kwenye chaguzi za 2020 eti wakadhitakiwe na CCM
 
Hicho chombo kingine kikiundwa watakaofanya kazi huko ni watanzania hawa hawa au aliens? Sisi kama taifa tuna tatizo kubwa sana when it comes to uaminifu na weledi #Doing the right thing hata kama hakuna mtu anakuona! Tuko na safari ndefu sana Mungu atuongoze tu!
 
Huyu mama ana huruma kwakweli. Sina mashaka kwake kuhusu UAMSHO, soon watakua huru.
 
Mh rais wachukulie hatua pia wale waliowabambikia kesi watz na kuwasumbua
 
Kabla ya kushangilia shinikizo la rais kwa vyombo vya usalama kuhusu kufutwa kesi zinazoitwa za kubambikiwa watu tujue kwanza kesi zenyewe ni zipi na nani wanahusika kubambikiza kesi hizo

Nasema hivyo kwa sababu kuna kesi za uhujumu mkubwa kama ile ya iptl ambazo zina ugumu kutokana na wahujumu na washirika wao kua na uwezo mkubwa kuvuruga ushahidi au kuzuia ushahidi. Isitoshe licha ya matendo ya uhujumu wao kuleta madhara makubwa kwa uchumi wa nchi watu hao wakiachiwa eti kwa kukosekana ushahiti bila shaka wataendelea kutumia mahakama kulihujumu taifa kwa kufanya madai ndani na nje ya nchi ambayo yatakua na athari kubwa kwa uchumi wetu.

Kwa hivyo yafaa serikali kuweka wazi kesi zipi zinaitwa za kubambikiza na nani wanashutumiwa kubambikiza. Na kwamba hatua gani zinachukuliwa kwa wabambikizaji. Vinginevyo tutaona fisadi wakubwa wakubwa ambao baada ya kutupwa lupango tumeona utulivu mkubwa wa uchumi na kupungua kwa kasi hujuma kwa uchumi wa nchi.
 
Wewe mwaka miaka ushahidi bado haujakamilika?? DPP kakalia kesi hadi kamaliza muda wake eti Upelelezi bado unaendelea kwako wewe ni poa tu??

Kama Washitakiwa wameonekana wana hatia ina maana na ushahidi upo sasa ucheleweshaji wa mashauri yale kusikilizwa na Wahusika kuhukumiwa ni wa nn??
 
Wananchi wa nchi hii wamekuwa wakitoa malalamiko yao ya muda mrefu sana, kuwa Jeshi la Polisi linawabambikia kesi wananchi wasio na hatia, hususani wale wanaowaona wanà mlengo wa kisiasa wa vyama vya upinzani.

Kauli hiyo imekuwa ikipingwa vikali na Jeshi la Polisi, likidai kuwa Jeshi la Polisi linafanya kazi yake kwa weledi na kila mshukiwa wa kesi anapaswa ajibu mashtaka yake kwenye vyombo vya sheria.

Hata hivyo leo hii Rais Samia Suluhu Hassan amekitengua kitendawili hicho kwa kueleza ukweli kuwa Jeshi hilo linawabambikia kesi wananchi wasio na hatia na hivyo kuleta msongamano mkubwa usio na ulazima huko magerezani.

Kwa kauli hiyo iliyotoka mdomoni kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, ni kwanini IGP Sirro hataki kujiuzulu??

Kama IGP Sirro atagoma kujiuzulu, basi tunamuomba Rais Samia Suluhu, amfute kazi Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi, kwa kuwa amekuwa akidanganya kwa kusema kuwa Jeshi lake linafanya kazi kwa weledi, wakati katika hali halisi, linafanya uonevu wa hali ya juu kwa wananchi wasiokuwa na hatia.

Tukumbuke pia wajibu namba moja wa Jeshi la Polisi nchini ni kuwalinda raia na mali zao.
 
Afrika hakuna kujiuzulu, ajiuzulu ale wapi? watoto wasiende chooni? sahau... unafia ofisini mpaka ufurushwe
 
Mambo mengine tusipende kuwaonea tu watu.hivi mkuu wewe binafsi ukipewa changamoto na bosi wako unaweza kujiuzulu?
 
Nimeandika huyu IGP hafai, kuna member amenishambulia sana kwa matusi kuwa he is the best IGP ever seen in the country since independence
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…