Rais Samia: TAKUKURU wamefuta kesi za kubambikizia 147, Polisi na nyie jitazameni
Huoni hata leo IGP kajikakamua kusema mapato ya usalama barabarani yamepungua kwa vile watu hawafanyi makosa tena. Akidhani ni ujiko kukusanya fine za barabarani. Mh. Rais kamzodoa kwamba wasitegemee fine kama chanzo cha mapato. Bali watoe elimu watu wasifanye makosa.
wacha twende tutafika nchi ya ahadi anayotupeleka mama.

nchi ambayo kila mtu atabembelezwa achague adhabu ipi inamfaa baada ya kutenda kosa.
mtu anatenda kosa barabarani makusudi anashauri aonywe[emoji23][emoji23][emoji23].

uzuri ni kwamba hazina hakuna biashara inafanyila kule,zinaingia ambazo zilitoka[emoji2223][emoji2223][emoji2223]
 
Kabla ya kushangilia shinikizo la rais kwa vyombo vya usalama kuhusu kufutwa kesi zinazoitwa za kubambikiwa watu tujue kwanza kesi zenyewe ni zipi na nani wanahusika kubambikiza kesi hizo
Nasema hivyo kwa sababu kuna kesi za uhujumu mkubwa kama ile ya iptl ambazo zina ugumu kutokana na wahujumu na washirika wao kua na uwezo mkubwa kuvuruga ushahidi au kuzuia ushahidi. Isitoshe licha ya matendo ya uhujumu wao kuleta na madhara makubwa kwa uchumi wa nchi watu hao wakiachiwa eti kwa kukosekana ushahiti bila shaka wataendelea kutumia mahakama kulihujumu taifa kwa kufanya madai ndani na nje ya nchi ambayo yatakua na athari kubwa kwa uchumi wetu.
Kwa hivyo yafaa serikali kuweka wazi kesi zipi zinaitwa za kubambikiza na nani wanashutumiwa kubambikiza. Na kwamba hatua gani zinachukuliwa kwa wabambikizaji. Vinginevyo tutaona fisadi wakubwa wakubwa ambao baada ya kutupwa lupango tumeona utulivu mkubwa wa uchumi na kupungua kwa kasi hujuma kwa uchumi wa nchi.
Nami najiuliza Rais SSH ana mpango wakuvunja Mahakama ya Mafisadi? Kama mwelekeo ndio huo "Mission Town" zitarejea ikiwa ni pamoja na vijiwe vya madawa ya kulevya.


Ila kwa uhakika hotuba zake zinatia matumaini ya Uhuru na Haki. Lakini kwa jinsi ya Watanzania tulivyo, yatabaki kuwa tu maneno ya kwenye jukwaa.
 
Nchi ikikosa Rais mzuri mifumo yote inakuwa ya kishetani. Akina Igp siro leo wanafanya kazi kwa uhuru kwa mujibu wa sheria za nchi. Wametukosea sana kwa kushiriki maovu na vitendo vibaya wakati wa Ibilisi Jiwe.
unadiriki kumwita binaadam mwenzako ibilisi mkuu??

ni hasira kiasi gani ulizo nazo kwa marehemu??

usimkasirishe Mungu akakugeukia kwa ghadhabu kuu,kubali kwamba maamuzi yake yametosha usizue mengine kwenye maisha yako.
 
Chuki zaidi ya uhalisia. Ungekuwa na ndugu anayesota mahabusu kwa kesi isiyo na kichwa wala miguu usingesema haya. Ungekuwa na ndugu ambaye kosa lake ni kupiga kampeni tu na kisha kuwekwa mahabusu KWA kesi ya uhujumu uchumi usingesema haya.
upige kampeni upewe kesi ya uhujumu uchumi!!!lisu angefungwa sasa,maana amepiga kampeni miezi 3 na kamaliza akaelekea zake ulaya.
 
Kwahiyo kesi zote 147 zilikua za kuumiza watu wasiyo na hatia? kweli ngozi nyeusi hatupendani...yaani mtu anaona rahaa kwa mwenzie kupoteza rasilimali zake bila hatia yoyote.
Yule mjeda aliona raha kuwa na mikesi mingi.....
Mama alimuambia kuwa sio sifa kuwa na makesi mengi yasiyo na ushahidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mataga watapata tabu sana awamu hii ya 6. Hii psychological torture wanayopewa kila uchao sio ya kitoto ati!
ajabu nyumbu ndio wanapiga kelele[emoji23][emoji23][emoji23]
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Hii ni baada ya kutakiwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa kesi za kubambika.

====




Rais Samia Suluhu: Kwenye suala la wingi wa mahabusu, labda niseme kwamba jana nikiapisha majaji nililigusia hili, uharakishwaji wa kesi na nimezitaka taasisi zote ikiwemo jeshi la polisi ambalo uchunguzi unaanza kwenu kuharakisha chunguzi za kesi mbalimbali zilizopo ili kuharakisha kesi kusikilizwa na iadha kufutwa au mtu kuhukumiwa ipasavyo lakini pia niongee na jeshi la Polisi kupunguza kesi za kubambikiza.

Kuna mlolongo mkubwa wa makesi ya kubambikiza, huu ukipungua na mahabusu watapungua, kwasababu wengi wapo wanasubiri kuhukumiwa, kesi haiendi, ushahidi hakuna, mpelelezi anashindwa kupeleka kesi kwasababu hakuna ushahidi.

Niombe sana, nilizungumza hili na TAKUKURU, wameweza kufuta kesi 147 ambazo waliwabambikizia watu, kwahiyo nanyi Jeshi la polisi jikagueni kama kuna za aina hiyo nazo zifutwe ili tupunguze wingi wa mahabusu kwenye majela yetu.
Yaani "legacy" inazidi kudidimia tu.

Muosha, huoshwa. Zamu yake sasa.

...wafuasi wake ndio hivyo watafute namna nyingine ya mungu wao kuendelea kuwa relevant akiwa 6' under.
 
Huoni hata leo IGP kajikakamua kusema mapato ya usalama barabarani yamepungua kwa vile watu hawafanyi makosa tena. Akidhani ni ujiko kukusanya fine za barabarani. Mh. Rais kamzodoa kwamba wasitegemee fine kama chanzo cha mapato. Bali watoe elimu watu wasifanye makosa.
Ila polisi walizidisha aisee wanaweza kupiga hata 90000

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo kesi zote 147 zilikua za kuumiza watu wasiyo na hatia? kweli ngozi nyeusi hatupendani...yaani mtu anaona rahaa kwa mwenzie kupoteza rasilimali zake bila hatia yoyote.
Sio zifutwe tu!!?
serekali inabidi ilipe fidia....
ili iwe fundisho kwa viongozi wabambikaji kesi
 
Kwahiyo kesi zote 147 zilikua za kuumiza watu wasiyo na hatia? kweli ngozi nyeusi hatupendani...yaani mtu anaona rahaa kwa mwenzie kupoteza rasilimali zake bila hatia yoyote.
Ndiyo maana ni muhimu, kuchunguza kwa umakini, kabla ya mtu kumwingiza kwenye mfumo wa utawala, kujua kama huyo mtu ana Roho wa Mungu au ana roho ya ibilisi.

Makosa yaliyofanyika mwaka 2015, sote tumeshuhudia madhara yake miaka 5 iloyofuatia. Angalia jinsi watu walivyoumizwa. Wapo waliobambikiwa kesi, wapo waliouawa, wapo waliotekwa na kupotezwa, wapo walioshambuliwa kwa risasi mithili ya simba mla watu.

Hongera Mama Samia, kwa kutaka kulirudisha Taifa letu kwenye ustaarabu baada ya uharibifu wa miaka wamiaka 5.
 
Wabambikizaji ni ccm.
Ambapo hata yule anayesema za kubambika ndio kiongozi wake.....anamlenga nani.......jiwe gizani........tunasubiria pia wanajeshi watapewa changamoto ipi kuhusu operesheni 'MKIRU' hapo ndipo penye kipimo cha 'impartiality justice'
 
Back
Top Bottom