Mambo mengine tusipende kuwaonea tu watu.hivi mkuu wewe binafsi ukipewa changamoto na bosi wako unaweza kujiuzulu?
Mkuu hili la kuwabambikia Raia kesi ni kashfa kubwa kwa Jeshi lenye jukumu la kuwalinda Raia na mali zao. Ni Raia wangapi waliohukumiwa kwa kesi na ushahidi wa kuwabambikia?? Kwa mfano Raia anakamatwa na kubambikiwa madawa ya kulevya ama silaha. Hapo shahidi ni Polisi na ushahidi ni kile alichodai kamkuta nacho Raia.

Hapa ningeshauri Mama SASHA angeunda Tume chini ya Mawakili Wabobezi kupita kwenye Magereza yote Nchini kuwaibaini wote walioonewa. Ninaamini wako wengi Magerezani.
 
Samia ana huruma juu ya waTanzania lakini huruma yake inakosa mipaka na baadhi ya watu wanaitumia huruma hiyo kupenyeza ajenda zao kwa manufaa yao......matamko yake mengi yako kisiasa badala ya kiweledi........

Kiweledi kufuta kesi unazodai za kubambikiza bila ya kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua waliobambikizia watu kesi.........Mama anapaswa kujua kuwa yeye ni rais wa Tanzania wote........
 
Shujaa wa Mazezeta alikuwa Raisi mbovu sana,Raisi asiyefuata Katiba na Sheria,hakujua kwamba kutesa Watu hakuwezi kukuacha salama.. Rot in Hell Zezeta lao.
 
Halaiser
Hiyo ni kweli tupu.

Hivi inawezekanaje kwa Jeshi la Polisi linalopaswa kuwalinda raia wake, ndiyo liwe la kuwakomoa raia wake kwa kuwabambikia kesi??

Naunga mkono pendekezo lako, kuwa iundwe Tume Huru, itakayoutafuta ukweli na kubaini ni watu wangapi wapo magerezani kwa kundiwa kesi za kubambika
 
Wewe akili yako ni ndogo sana. Ya iptl ni ya kubambika? Tuanzie hapo kwanza
 
IGP Sirro ni askari mwema na mzuri ila amepata bahati mbaya sana kufanya kazi na Katili Jiwe.

Amemchafua sana
 
Mimi nimeanza kuingiwa na wasiwasi kuwa ninyi sio Watanzania mbona mnapenda ukatili ukatili sisi Watanzania tuna hulka moja ya UPENDO au ninyi ni Interehamwe?
 
IGP Sirro ni askari mwema na mzuri ila amepata bahati mbaya sana kufanya kazi na Katili Jiwe.

Amemchafua sana
Utendaji kazi wake umeingia doa, kwa kuwa huyo mwendazake, anayedaiwa kuwa ndiyo aliyekuwa anamuagiza kufanya uovu wote huo, ametangulia mbele ya haki...........

Sasa balaa kamuachia IGP Sirro, ambaye ameelezwa hadharani na Rais Samia Suluhu, kuwa Jeshi lake ndilo linawabambikia kesi raia wasio na hatia!
 
Hii inchi bana [emoji28], Takukuru [emoji23][emoji23][emoji23], Unapamba na rushwa kwa kubambikia watu kesi
 
Ndiyo maana ni muhimu, kuchunguza kwa umakini, kabla ya mtu kumwingiza kwenye mfumo wa utawala, kujua kama huyo mtu ana Roho wa Mungu au ana roho ya ibilisi...
Mimi ninamuunga mkono Mhe. Raisi Mama Samia Suluhu Hassan a.k.a Mama SASHA kuhusu kufutia kesi watu waliobambikiziwa makesi bila kosa lolote.

Mimi namuomba Mhe Raisi hasiishie kwenye kuzifuta kesi tu za watu waliobambikiwa kesi bali aende mbali zaidi na kuwachukulia hatua kali wale wote waliofaidika na mpango mzima wa kuwaumiza watanzania wenzetu! Kuna watu wameumia sana nchi hii bila kosa lolote.
 
Mimi nimeanza kuingiwa na wasiwasi kuwa ninyi sio Watanzania mbona mnapenda ukatili ukatili sisi Watanzania tuna hulka moja ya UPENDO au ninyi ni Interehamwe?
sijui wewe utatuitaje,ila kwa sababu ya Tanzania sio ishu.
 

Mikumi tena kwa Madame President.

Ni kweli haiwezekani mtu anakaa jela miaka miwili halafu tunaambiwa uchunguzi haujakamlika,sasa kama hamjakamilisha uchunguzi ya nini kumkamata?
 
Kwakweli Samia suluhu amejifunza mambo mengi kupitia mapungufu ya mtangulizi wake. Hapendi kuendeleza mabaya. Tutarajie hata sheria kandamizi hapo mbeleni zitakuja kupelekwa Bungeni kwa marekebisho
Atleast its made difference yo yhose 147 individuals. Lakini anatakiwa aweke process itakayo prevent that from ever happening again!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…