Na sasa hivi ndiyo inazidi kupigwa pini kwa vikwazo vya kimataifa na nchi za Magharibi.
Kwanza nitoe Salam zangu kwako mkuu, maana nilikuwa mfuatiliaji mkubwa jf kutokana na mada zako.
Unaposema Dunia nzima una maanisha nini?
Hao western Europe watalazimika kutumia Rubo wanapofanya miamala kule Urusi.
Nakukumbusha tu hata Mbolea ambayo inahitajika huko Amerika inakwenda kununuliwa kwa Rubo.
Tunachokosea pia tunapowaza Magharibi mwa Ulaya, tunayawaza tu Mataifa yenye nguvu za Kiuchumi tu kama Ujerumani, Uingereza, Ufaransa na kidogo Hispania.
Ila kiukweli Kuna vinchi vingi vidogo kama Latvia, Lithuania, Hungary, Bulgaria, Greece, Austria ambazo chumi zao zinaitegemea mno Urusi, hivyo mahitaji ya Rubo yataongezeka kwenye bidhaa nyingine.
Watalazimika kuhifadhi pesa ya Urusi ili waweze kununua mahitaji muhimu ikiwemo Shayiri, Ngano, Mafuta ya kupikia na bidhaa mbalimbali.
Tuje nchi za central Asia hapa tunawagusa Kazakhstan, Tajikistan, Uzbekistan, Turkmenistan, Armenia, Afghanistan, Azerbaijan hawa wataongeza kiwango Cha ununuzi wa bidhaa kwa kutumia pesa ya Urusi na akiba yake.
Tukienda Mashariki ya mbali huku nadhani wanajaribu kulink system zao pamoja na Urusi kwenye masuala ya fedha.
Mataifa mama Uchina, Vietnam, Myanmar, Laos, Bangladesh.
India kila mtu anajua kinachoendelea.
Brazil hawa wanatafuta namna ya kulipia kwa Rubo hasa Ile system insyojaribiwa ikikaa vizuri.
Afrika ya kusini kila mtu anajua.
Hivyo matendo waliyoyafanya watu wa Ulaya ni kuilazimisha Urusi rasmi kuegemea upande wa Mashariki ambao ni hatari kubwa kwa baadae.