Uchaguzi 2020 Samia Suluhu Hassan: Askari wa Serikali ya CCM akipiga mtu risasi 3 akamkosa atawajibika

Uchaguzi 2020 Samia Suluhu Hassan: Askari wa Serikali ya CCM akipiga mtu risasi 3 akamkosa atawajibika

issenye

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Posts
3,788
Reaction score
5,217



Mama Samia Suluhu Hassani ambaye ni Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) amesema kuwa anawaomba wafanye kampeni kwa amani wakipita wawasikilize wala wasigombane nao.

Amesema kuwa wapo wagombea watakwenda kuwaambia kuwa walivunjwa miguu na mwingine alimsikia akisema kuwa alipigwa risasi 16.

''Watakuja kuwaambieni wamevunjwa miguu lakini waulizeni ilikuwaje wakavunjwa miguu, wengine jana nilisikia mmoja anasema amemimiwa risasi 16 nataka niwaambie huyo sio askari wetu wa serikali ya chama cha Mapinduzi, askari wetu akipiga mtu tatu akamkosa atawajibika sikwambii askari aliefundishwa akapiga 16 huyo mtu atoke mzima".
 
Lissu itakuwa alipigwa risasi na Wadeni wake au alikua anachukua wake za watu, ndiyo hayo matatizo kajisababishia!!
Hao wadeni wake baadae wakaenda kun'goa CCTV

Lakini kabla ya shambulizi hao jamaa ambao walichukuliwa wake zao walihakikisha walinzi wote hapo Area D wanaondolewa amaa kweli hao watu wananguvu serikalini
 
Hapo kasema ukweli mtupu Maana yeye ndo miongoni mwa maboss wa Askari wao wa CCM hivyo anawajua vizuri weredi wao. Kwahiyo Mimi naamini alichokisema na ndo uhalisia.

Zitto aliutaka uenyekit wa chadema akafukuzwa Chama.
Ben sanane aliutaka uenyekit wa Chama akapotea mpaka leo.
Tundu lissu aliutaka uenyekiti wa Chama akapigwa na vitu vinavyosadikika ni risasi.
F. SUMAYE aliutaka uenyekiti wa Chama akaambiwa kuwa Sumu haionjwi kwa usalama wa maisha yake akaamua kujiweka pembeni na kuchomoka kwenye himaya za mtia Sumu.

Swali; kwanini Kila anaeutaka uenyekiti wa Chama CDM anapatwa na matatizo Ni ipi Siri iliyopo Hapo nyuma?

Je nikweli Mbowe Ni kibaraka wa serikali kwamba hawezi kutoka kwenye kile kiti kwa masilahi ya Taifa?
 

Tumwambie tu huyu mke wa Coplo wa zimamoto kuwa wauaji waliowatuma kumuua Lissu hawakumkosa, walimpata, walimimina zaidi ya 30, na zote zililenga pale pale anapokaa Lissu kwa upande wa ndani. Hongera huyo askari kaiva kwenye shabaha.
Mliwatuma wakatekeleza maelekezo.
Ila hata siku moja shetani hajawahi kumzidi Mungu!
Nilikuwa nakuona ww mama mstaarab umekaa kimya haufungamani na hao wenzako, kumbe ulikuwa umeficha makucha, Lissu mliyomtwanga marisasi ya kutosha Mungu akasema no, huyu mtu ni mpango wangu, ni lazima aishi! Mna roho mbaya sana ninyi watu, sijui mwanamke gan ww, hukuzaa??
 
Back
Top Bottom