Serikali: Walimu sasa kufanya mtihani wa kupima uwezo kabla ya kuajiriwa

Sawa ila sisi tulioajiriwa juzi na tumekwenda kuripoti maeneo yetu yakazi mbona hatujapata pepa au ndo tumepona
 
wapi huko,mbona walimu wamepangwa juzi tu na hakuna cha mtihani Wala Nini!!!???
 
Vyuo haviaminiki tena vilivyowaandaa walimu?
Na vyuo vya uhasibu, na fani zingine haviaminiki mpaka waomba kazi wafanyiwe usaili?
Issue ni uhitaji mdogo kuliko upatikanaji wa walimu wenyewe.
Zamani mpaka kazi ya uhasibu hapakuwa na usaili.
Majeshini nako kwa wenye emilu kidogo waliangaliwa afya tu
 
Huu ni upumbavu wa kupitiliza. Kama hawaamini vyuo wanavyosoma si bora wavifute tu? Wapuuzi wakubwa!
 
Ni kawaida sana kuona viongozi wa serikali wenye akili za kukariri madesa kuwekeza kwenye mambo ya kipuuzi kama haya, huku yale ya msingi wakiyapuuza.

Unamlipa mwalimu mshahara mbuzi, halafu unatagemea maajabu! Kwa nini wasinde kujifunza kwenye zile shule binafsi zinazofanya vizuri, ili kumbaini mchawi?
 
Professor Mkenda, wazo lako ni nzuri na umelileta wakati sahihi.

1. Mitihani hiyo itatungwa na nani?
2. Mitihani hiyo itasahihishwa na nani.
 
Aliyekuambia mwalimu analipwa mshahara mbuzi ni nani?
 
Yaani bado tatizo litakuwa vile vile, mtu kasoma miaka mitatu unakuja kumpa kimtihani ya page tatu afu um judge kwamba hafai kisa kashindwa icho kimtihani... linatengenezwa bomu la kukithiri rushwa kwene upatikanaji wa izo ajira.
Ilitakiwa vigezo vya kusoma ualimu viwe vinachukua wanafunzi bright na maslahi yao yaboreshwe walau kwa kiasi itsaidia
 
Hao walimu mnawalinganisha na akina nani kwenye kupima udogo wa mishahara yao?
 
Nimemsikia profesa akijaribu kutumia lugha nzuri katika jambo ovu ! Kwamba sekta ya ualimu watakuwa wanafanyiwa mtihani Tena ndio wapewe ajira! Bado unaendeleza harakati za kudharau taalumu inayotolewa vyuoni kwamba haitoshelezi ...kama ni hivyo sekta zote wafanyiwe mitihani hata nyinyi wabunge na mawaziri mkiteuliwa mpewe kwanza mitihani ,mainjinia madaktari na idara zote...acha kuifanya idara ya ualimu ndio ya wapumbavu ...siungi mkono hiyo hoja ni uchawi kwa watoto wetu wanaokaa vyuoni miaka mitatu Leo uje kuifanyisha mitihani mingine kwa mshahara Gani unaowalipa? Ajenda Yako ni mbovu na inadharau taaluma ya ualimu
 
Nakumbuka mwaka flani walimu tulifanya mtihani flani kwa ajili ya kazi za serikali na 99%tulipiga daraja A wachache sana walipata daraja B
Kati ya watu wako vema ni walimu tz serikali ishughulikie vitu serious kama mishahara promotion madeni miundo mbinu ya shule na vifaa vya kufundishia waone kama watu hawatapiga kazi to the fullest
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…