That is not sustainable kwani sukari si waliofanya hivyo huyo JPM kwani bei ilishuka? Korosho si walitumia extreme measures mpaka za kuonyesha shamba ila bei ilipanda ule msimu...
Korosho kilichotokea ni upuuzi wa serikali ku set selling price yao badala ya kukubali bei ya soko inayoamuliwa na suppy and demand.
Matokeo yake mzigo ukawadodea ukizingatia wabanguaji wakubwa ni India na wauzaji wakubwa kwa retailers duniani ni Vietman; msimu ukipita ujauza wakapata kwengine imekula kwako.
Sukari shida ilikuwa kuzuia importation bila kuweka stock kwanza hasa kwa wazalishaji wa viwandani.
The point is hiyo mifano yako ni different scenarios na kinachoendelea leo.
Kwa sasa serikali aina utaratibu wa kuelewa food stock zilizopo kwa wafanyabiashara, wao wanajua kilichopo kwenye maghala yao tu.
Na hili jambo sio zuri kwenye planning na intervention sio tu kisera bali ata kuelewa ni muda gani sahihi wa kuagiza kama kuna ulazima wa kufanya ivyo kabla ya chakula kupanda bei sana, au kutoagiza kwa sababu kilichopo kinatosha na kuwalazimu kutumia mbinu nyingine.
Kama kipo cha kutosha weka price ceiling ni mambo ya kawaida kwenye kuwalinda walaji hasa bei ya basic needs zinapokuwa hatari kuhakikisha usalama wao, au mwaga reserves kuongeza supply.
Lakini kama hujui stock level za wafanyabiashara, halafu ukaagiza karibu na mavuno. Kuna mawili kama kweli wafanyabiashara hawana stock ya kutosha kilichoagizwa hakitakuwa na madhara kwa bei ya mkulima anapovuna maana kitaingia sokoni na kuisha haraka.
Na kama kipo kimefichwa basi kutakuwa na chakula kingi sana wakati wa kuvuna na mkulima ataonewa kwenye bei again serikali inaweza lazimika kuweka price floors au kulazimika kukinunua wao hiko chakula kutoka mashambani.
In short hizi tabia za wafanyabiashara kuhodhi chakula kuna haribu nguvu ya invisible hand kufanya kazi bila ya serikali kuingilia somo na kuondoa umakini wa serikali kwenye mipango yake.
Hizi ndio shida za kuwakabidhi hizi wizara nyeti vilaza na watu wasio elewa jukumu lao kubwa ni kuhakikisha bei ya chakula ni himilivu hasa kwa wenye kipato kidogo.
Gharama za maisha zimekuwa kubwa mpaka wazazi awapeleki watoto shule.