Serikali yatoa kibali kuagiza mchele nje ya nchi
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji akiwa Dar es salaam leo amesema Serikali imetoa vibali vya kuingiza mchele nchini Tani Elfu 90 kwa ruhusa ya Rais Dkt.Samia “Tunatarajia kuanzia mwisho wa mwezi huu wa pili zao la mchele litapungua bei...
Mwanasiasa, tengeneza mazingira ya kuleta tatizo, halafu tengeneza mazingira ya kuonesha unalitafutia suluhusho, upate sifa!
 
Kwa nini mliruhusu kiende nje? Au mlitaka kipungue ili mfanye biashara zenu?
Screenshot_20230216-195210.jpg
 
Dawa yao walanguzi ni ndogo sana sajili wauza chakula cha jumla wote, weka takwa la kuripoti stock levels baada ya mavuno na kila mwezi baada ya hapo.

Hiyo inasaidia serikali ku monitor national food stock level zilizopo kwa wafanyabiashara na kwenye maghala ya serikali ukiona kipo cha kutosha kwa wafanyabiashara na bei zinapanda mwaga cha serikali, agiza stock kufidia, ingia sokoni uza huko wanapouza kwa bei ndogo zaidi.

Hii cartel ya wafanyabiashara ya jumla aitakiwi kuachwa iendelee hivi; walijaribu hivi kwenye saruji enzi za Magufuli yule jamaa alivamia maghala yao na kuwalazimisha watoe hiyo mifuko yao na akaweka price ceiling za bei watake wasitake kila mkoa.
 
Dawa yao walanguzi ni ndogo sana sajili wauza chakula cha jumla wote, weka takwa la kuripoti stock levels baada ya mavuno na kila mwezi baada ya hapo...
That is not sustainable kwani sukari si waliofanya hivyo huyo JPM kwani bei ilishuka? Korosho si walitumia extreme measures mpaka za kuonyesha shamba ila bei ilipanda ule msimu?

Uchumi huwezi tumia mabavu utadhani ni ujamaa Kwa Sasa ni soko huria kama mchele umepanda bei basi ni kuimport Ili supply iwe optimal na demand so bei zitashuka tu kama wakulima hawataki hizo bei basi wakauze nje ya nchi simple and clear.

Hata madawa ya kulevya Yana thamani sababu wauzaji ni limited so Kuna demand kubwa ila supplier Wachache ila siku wakihalalisha madawa hata kwa wiki Moja zile cartel zitakufa maana waagizaji watakua wengi na bei zitashuka so zitakufa naturally.

Kuna wakati ni kutumia akili kuliko mabavu no wonder Nyerere aliua uchumi
 
Hivi hapa kuna wakulima 1000 wanaomiliki matreka na mashine kubwa za kulima na kuvuna.
Serikali hii ya ccm kama alama yao ya jembe itosheleze kilimo
 
Ukiona hivyo wafanya biashara washatoa rushwa mamlaka flani wajilie hela ya masikini.
 
That is not sustainable kwani sukari si waliofanya hivyo huyo JPM kwani bei ilishuka? Korosho si walitumia extreme measures mpaka za kuonyesha shamba ila bei ilipanda ule msimu...
Korosho kilichotokea ni upuuzi wa serikali ku set selling price yao badala ya kukubali bei ya soko inayoamuliwa na suppy and demand.

Matokeo yake mzigo ukawadodea ukizingatia wabanguaji wakubwa ni India na wauzaji wakubwa kwa retailers duniani ni Vietman; msimu ukipita ujauza wakapata kwengine imekula kwako.

Sukari shida ilikuwa kuzuia importation bila kuweka stock kwanza hasa kwa wazalishaji wa viwandani.

The point is hiyo mifano yako ni different scenarios na kinachoendelea leo.

Kwa sasa serikali aina utaratibu wa kuelewa food stock zilizopo kwa wafanyabiashara, wao wanajua kilichopo kwenye maghala yao tu.

Na hili jambo sio zuri kwenye planning na intervention sio tu kisera bali ata kuelewa ni muda gani sahihi wa kuagiza kama kuna ulazima wa kufanya ivyo kabla ya chakula kupanda bei sana, au kutoagiza kwa sababu kilichopo kinatosha na kuwalazimu kutumia mbinu nyingine.

Kama kipo cha kutosha weka price ceiling ni mambo ya kawaida kwenye kuwalinda walaji hasa bei ya basic needs zinapokuwa hatari kuhakikisha usalama wao, au mwaga reserves kuongeza supply.

Lakini kama hujui stock level za wafanyabiashara, halafu ukaagiza karibu na mavuno. Kuna mawili kama kweli wafanyabiashara hawana stock ya kutosha kilichoagizwa hakitakuwa na madhara kwa bei ya mkulima anapovuna maana kitaingia sokoni na kuisha haraka.

Na kama kipo kimefichwa basi kutakuwa na chakula kingi sana wakati wa kuvuna na mkulima ataonewa kwenye bei again serikali inaweza lazimika kuweka price floors au kulazimika kukinunua wao hiko chakula kutoka mashambani.

In short hizi tabia za wafanyabiashara kuhodhi chakula kuna haribu nguvu ya invisible hand kufanya kazi bila ya serikali kuingilia somo na kuondoa umakini wa serikali kwenye mipango yake.

Hizi ndio shida za kuwakabidhi hizi wizara nyeti vilaza na watu wasio elewa jukumu lao kubwa ni kuhakikisha bei ya chakula ni himilivu hasa kwa wenye kipato kidogo.

Gharama za maisha zimekuwa kubwa mpaka wazazi awapeleki watoto shule.
 
Ndio wakati wa vijana kurudi vijijini...utakuta mtu kang'ang'ania mjini anauza katoni Moja ya maji akiwa na uhakika akipata elfu tatu anakula chakula Cha mchana na usiku Kwa mama ntilie.

Gharama na maumivu anapata mkulima! Kisa tunazuia soko lenye kulipa na kumfuta jasho mkulima Ili tulinde wengine vyakula visipande bei
 
That is not sustainable kwani sukari si waliofanya hivyo huyo JPM kwani bei ilishuka? Korosho si walitumia extreme measures mpaka za kuonyesha shamba ila bei ilipanda ule msimu...
Jikite kwenye hoja. Kwa nini muuze chakule nje holela alafu baadae muagize toka nje?
 
Back
Top Bottom