Tatizo la wasaidizi wa Mh Rais ni mihemko. Hawajui kinacho takiwa. Wapo kwa ajili ya kupiga tuu. Hawana huruma na Watanzania.
Mmoja anasema acha wakulima usiwapangie. Mwingine ana dharau bunge na kusema wajadili uganga wa kienyeji. Na Mama bado ana waona wako sawa.
Tuna fanyiwa majaribio.
 
Hii nchi Bado sana,sasa tulikuwa na nafaka nyingi,bei ilikuwa poa,mkazuia wakulima wasiuze nje,baadae mksruhusu,nafaka ikauzwa nyingi nje,sasa mahitaji yakawa makubwa,bei ikapanda,sasa hv nafska imekuwa haba,mmeruhusu tuagize nje!!
Swali langu kwenu nyie kenge maji,kwani haiwezekani tulime wenyewe,mkulima apate faida,na mnunuzi apate unafuu wa kununua?
Mchele uwe buku moja,mkulima apate faida hata ya 300 kwa kila kilo,kwanini mnatuhusu nafska iuzwe nje mpaka bei inapanda juu ndani ya nchi
 
Ni aibu kwa serikali kuagiza CHAKULA kutoka nje kusikojulikana ili iwauzie WANANCHI wake.
 
Mjinga tuu huyo Waziri wenu,hakuna sababu ya kuagiza mchele Nje ya Nchi maan upo wa kutosha Nchini.
 
Baadhi ya sisi waafrika ni watu wa ajabu sana.
 
Haya sasa....
 
Wakulima wa Tanzania wataanza kulalamika, maana wanaogopa sana ushindani na bidhaa kutoka Nje!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Wakulima wa kitanzania wakizidisha uzalishaji mashambani na kuweka akiba ya chakula bado wana nafasi ya kuwashinda hao waingizaji chakula kibovu kutoka nje.

Kumbuka wafanyabiashara wao hujali faida zaidi kuliko afya na utu.
 
Mjinga tuu huyo Waziri wenu,hakuna sababu ya kuagiza mchele Nje ya Nchi maan upo wa kutosha Nchini.
Ungekuwepo wa kutosha kungekuwa na mfumuko? au unamtetea bwashee kutoweka control ya biashara ya mazao ya chakula kwenda nje, maana tunaambiwa wageni walikuwa wanaenda kununua mazao hadi vijijini kinyume na utaratibu....
 
Lilisitishwa Zanzibar
Kwa hiyo huku bara tupo kama popo, upande mmoja tunauza nje, upande mwingine tunaagiza toka nje, halafu tunasema tuna serikali!

Tunajiendea zetu tu, kama kundi la wana kondoo.
 
Hii kitaalamu inaitwa,"NJE NDANI".
 
Mbona ma basmati yamejaa kwenye hoteli za wazenji na Michele huo ni test less kwani ulikuwa unaingiaje nchini na kibali kilikuwa hakipo?
 
Safi kabisa si walisema ni free market ingawa ilikuwa ya upande mmoja kwa mkulima wa ndani kuuza kokote ilihali wa nje kuleta ndani ilizuiliwa kwa hapa kuruhusu itasaidia sana maana wameona DD>SS

Though inafikirisha was it really for the sake of mkulima hizi sarakasi zote za Bashe au palikuwa na kitu nyuma ya pazia huenda watu walilangua mazao ya wakulima wakaweka store mbinu zikasukwa waziri akaingia kingi wameuza mzigo umeisha ndiyo ruksa ya kuagiza nje imetoka watu wameneemeka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…