Hebu tuelezee kimoja cha Magufuli kilichofanikiwa.
1.Kuusimamia msikiti wa bakwata pale kinondoni mpaka ukakamilika kama alivyoomba kwa mfalme wa morocco.
2. Kuhakikisha mali za wakfu zinarudishwa kwa waislamu ikiwemo eneo la chang'ombe alilouziwa manji na waislam wasio waaminifu hali iliyosababisha taharuki mara kwa mara kutoka kwa sheikh Ponda enzi za JK.
3. Kuhakikisha eneo la magomeni kotaz linarudishwa kwa wananchi kama ambavyo manispaa ya kinondoni ilishalikabidhi kwa manji kwa miaka 99 na magu akajenga ghorofa ambapo wengi wanaokaa pale ni muslims.
4. Kuhakikisha msikiti wa kule dodoma unajengwa na kuisha kama ambavyo aliitisha michango kwa ajili ya ule msikiti.
5. Kuwaleta pamoja viongozi wa dini na hivyo kuondoa hali ya sintofahamu baina ya dini na dini, madhehebu kwa madhehebu, taasisi za dini mfano tulishuhudia sheikh mkuu akihudhuria shughuli za Al hikma foundation chini ya sheikh Kishki.
6. Alihakikisha sheikh Ponda anaachiwa huru kutokana na kesi ya kuchochea vurugu enzi za JK hivyo kuendelea na shughuli zake za uanaharakati.
7. Alitoa eneo la baba yake kule chato kwa taasisi ya Al hikma ili ujengwe msikiti.
8. Lakini aliivunja MOU kiaina kama ambavyo ilijuwa inalalamikiwa na waislamu kwa kuhakikisha serikali inamiliki vituo vya afya, hospitali, kudahili wanafunzi kwenye vyuo vya serikali kama kipaumbele, serikali ina vyuo na shule zinazotoa matokeo mazuri tofauti na ilivyokuwa awali ambapo serikali ilitegemea kwa kiasi kikubwa hizi huduma kutoka kwenye taasisi za kikristo.
Bahati mbaya mnafiki ni mwepesi kusahau.