Simba SC 1-3 Jwaneng Galaxy FC | CAFCL | Simba yatolewa klabu bingwa Afrika

Simba SC 1-3 Jwaneng Galaxy FC | CAFCL | Simba yatolewa klabu bingwa Afrika

Simba tumefungwa kihalali na hakuna sababu yakutafuta mchawi.hao jamaa ni wazuri na wanamipango inayoonekana tofauti na simba waliokua wanacheza kwa kuridhika kama vile wanacheza mechi yakutafuta point sio kusonga mbele.ila pia lile tatizo la simba kukosa mfumo/mbinu mbadala bado linamsumbua mwalimu.Mechi ya kwanza hao jamaa pamoja nakwamba tuliwafunga lakini walicheza mpira unaoonekana kuliko simba sasa ilitakiwa simba waje na mfumo mwingine tofauti na ule wa mechi ya mwanzo.Sasa hilo lilikua linawapa galaxy hamasa yakupambana maana walikua wanaona mapungufu ya simba na makosa yanayoweza kuwapa nafasi.ndo maana walipopata goli la kusawazisha wakajiamini zaidi wakaanza kupush zaid kwenda mbele uku simba pamoja na mwalimu kufanya sub bado uchezaji wa timu ulibaki kua ule ule.Mwalimu afanye mabadiliko ya mbinu zake vinginevyo ata timu za ligi yetu zitatusumbua sana msimu huu.
 
Pole sana. Wengi hatukutegemea kuwa matokeo yangekuwa ya kikatli kwetu kwa kiwango hiki, hasa baada ya matokeo mazuri ugenini. Tulishakuwa na uhakika kuwa tunaingia hatua ya makundi. Na si ajabu ukakuta mashabiki ndio tunaumia zaidi kuliko wachezaji.
Utuwa umeumia kama yule alibeba beib wake na jezi wakaavaa naona jioni hii wamepita hapa kwangu wamenuna hao sijui leo ndani kutakuwaje
 
Man u naye keshafungwa 4 na ndo half time.
Shabiki wa simba ambaye ni man u usifuatilie matokeo kafanye mambo mengine usije ukapata degedege.
Man u wabadilishe kocha.Timu ni nzuri ila mwalimu kaishindwa.sasa sijui uongozi unamwogopa kwa heshima ya sir.Alex au shida nini.
 
Hili ndilo tatizo la wachezaji na viongozi wa timu ku bet mechi wanazocheza. Hii mechi, uchunguzi ufanyike kwa makampuni ama maajenti wa biashara za kamali nchini. Betting is killing our football game.

Poleni watani zangu.
Kilichotokea ni matokea tu ya uwanjani.ukifanya uzembe lazima uadhibiwe wala hakukua na hayo unayoyasema.
 
Nazani hujui unaongea nn, ila kwa kuwa ni jamii forum na kila mtu anahaki ya kutoa maoni anayojiskia basi tukuache, ila nakushauri achana na masuala ya mpila.
Mwisho naomba nkukumbushe huyu ndiye kocha aliyeshinda mechi 4 na kusare mechi 1 na kufungwa 1 latika group stage yenye timu kama All ahly,, Ell melleki, na As vita na aliongoza kundi
Karithi timu yenye momentum wala hakuna maajab aliyoongeza. Alirithi timu yenye connection na iliyojengwa na watangulizi wake.

Mtu asiye na qualifications anatetewaje? Simba aliyoirthi ni kubwa kuliko uwezo wake. Na inaonekana hata mwenyewe humjui. Huyo jamaa stage ya mbali aliyowahi kuachive ni kufika Quarter finals za Champions League akiwa na Simba. Hana la ziada
 
Bora hata wacheze Onyango na Inonga- Wawa ameishachoka jamani mipira ya juu haruki- kule mbele ndio kabisa - Bocco kachoka- Dilunga kachoka- Kagere kachoka- Mugalu hakuna kitu- waliosajiriwa nao hakuna kitu- shabalala na Kapombe nao shida- kwa kweli uongozi kazi wanayo.
Wakishinda kuchoka kwako hakuonekani.mambo mengine ni matokeo tu ya mpira maana ata wapinzani wetu nao wanajiandaa na wanatumia mapungufu yetu munufaika.timu iko vizuri ni marekebisho kidogo tu yanahitajika.
 
Back
Top Bottom