Mgombea urais kupitia CCM, Dr JOHN POMBE MAGUFULI anatarajia kuunguruma katika jiji la Mbeya, tukio zima litarushwa mojakwamoja na vyombo mbalimbali vya habari ikiwa ni pamoja na radio na TV
Wanainchi wote wa Mbeya wamekuwa na hamu kubwa kwa muda mrefu ya kutaka kufikisha kero zao kwa Mh Magufuli.
MGOMBEA urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli, amewataka wanaosema kuwa hataweza kuleta mabadiliko kwa kuwa yuko ndani ya mfumo wa chama hicho, wakajifunze China.
Akizungumza katika mikutano, Dk Magufuli alisema China imefanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi, kiteknolojia na kijamii, kwa kutumia chama cha Kikomunisti chenye mfumo wa kijamaa kama CCM.
Kwa mujibu wa Dk Magufuli, walichofanya katika nchi hiyo ni kutumia watu wa ndani ya chama hicho cha Kikomunisti, kuleta mabadiliko yanayoonekana dunia nzima leo mpaka Marekani imeshangazwa.
Nchi ya China ilikuwa chini ya Chama cha Kikomunisti chini ya Mwenyekiti Mao, walipopata uzoefu wakafanya mabadiliko bila kuondoa chama kilichokuwepo madarakani, alisema.
Dk Magufuli pia aliwaonya Watanzania kuwa uongozi wa nchi haujaribiwi na hata yeye alipochukua fomu za kuwania urais, alijua kuwa haombi urais kwa ajili ya majaribio, ndio maana alichukua fomu na kutafuta wadhamini kimya kimya, huku akimtanguliza Mungu mbele.
Aliwahadharisha Watanzania uwezekano wa kutokea watu watakaowapa fedha, ili wawachague na kuwataka wawaepuke kwa kuwa watakuwa na deni watakalotakiwa kulipa huko walikotoa fedha.
Alisema yeye deni lake ni kutumikia Watanzania wote bila kujali vyama vyao, lakini si deni la fedha kwa watu wenye fedha kwa kuwa hatoi fedha mahali popote ya kuomba kuchaguliwa.
Magufuli akielekea uwanjani ili kujinadi katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Ruanda Nzonve, Mbeya
Magufuli akiwa na watoto ambao walikuwa na hamu ya kutaka kumsalimia kwa kumpa mikono.
Magufuli akijinadi kwa wananchi katika mkutano
Wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mgombea Urais kwa Tiketi ya CCM, John Magufuli
JPM
Sugu kiboko yake inatia timu kesho hatumwi m2 dukani, jembe linakubalika kila kona sasa zamu ya monduli weweeee......ukawa mtakufa kwa presha
Sehemu zote alizopita Magufuli wananchi wanasema huyu Lofa hapati kitu. Huko Mbeya kumbuka kwamba Bara bara zake zimejengwa chini ya kiwango na kupelekea mauti kwa watanzania wengi. Ni miezi michache tu imepita tumepoteza ndugu zetu zaidi ya 50 kwa bara bara zilizojenga kwa gharama kubwa na kwa chini ya kiwango kikubwa. Magufuli hafai huyu Chunusi mtu.
Katika hali isiyo ya kawaida Magufuli ameugua ghafla akiwa jukwaani na kushindwa kuongea akiwa kwenye mkutano wa hadhara mbeya
Lazima afya za wagombea zikapimwe magufuli si mzima
Source:Chanel 10
atawaelezea matatizo ya watanzania yaliyoletwa na ccm, Lowassa anakuja kuwapa solution.
au mkuu umesahau kazi ya kampeni meneja.
kwa hiyo hesabu rahisi utajua nani atajaza watu.
ila kazi kubwa atamsaidia lowasa ni bariadi, sengerema na muleba
Hizi post za kufuli mbona hazina wachangiaji?
Hahahahah kweli CCM mmekwisha!! yaani mnaanzisha thread in a negative way kuvutia watu wafungue au wasome nyuzi zenu!!!
Nakwanini wawe CCM??Pigeni mpaka wa dedi
mkuu nimekubali kweli magufuli ni mtu sahihi ili tusichague chama tuchague mtu ,na magufuli atatusadie
Subiri uone jamaa yako kesho atakavyo kuwa anatetemeka. Dakika 5 tu, atakalishwa chini.Lowasa rais wetu ajae Watanzania tunampenda sana
Asifanishe na China, China wezi wananyongwa haijalishi una cheo i'la tz wanaongezwa vyeo au kubadilishiwa majukumu kumbe hana nia nzuri ya kututoa tulipo
Nimepenyezewa video clip inayoonyesha magufuli akizomewa mbeya, na kukutana na alama ya vidole viwili (inayotumiwa sana na chadema), mpaka ikabidi nayeye atumie vidole viwili, kuonyesha vijana waliokuwa barabarani kwamba nayeye anakubali upande wa pili.
Tatizo sio magufuli, tatizo kubwa tulilonalo watanzania wengi, ni mfumo wa CCM, na lichama lao la kuneemeshana wenyewe, huku wakigandamiza haki na maendeleo ya wenge.
Pole sana magufuli, hiyo ndio CCM yako, anayokuachia Kikwete, ufe nayo!
Peeeeeeeeeppppoooooooooooooooooooozzzzzzzzzzzz!!!!!!!!!!!!!!!!
Utakua lini mkuu? Kwel mahaba ya chama fulan yanasababisha uhamasishe mtanzania mwenzako apigwe?
Ili wanaJF wafungue hii thread lazima heading isomeke kinyume! Kweli CCM imefika pabaya!
UMEME HAKUNA, MAJI HAKUNA, HUDUMA ZA AFYA HAKUNA, MIUNDOMBINU HAKUNA, halafu wanataka tuwape kura tena! OVER MY DEAD BODY..........!!!!!!!!!!!!!!!!!
CCM imeshachoka, ipumzike kwa Amani! HAKUNA NAMNA TENA!!!!!!!
Ndugu,Magufuli anatumia hoja za ki UKAWA kuvutia watu!!!
Nawewe unaandika heading ya ki UKAWA ili. kuvuta watazamaji!!!
hahahahah mmekwisha
Chini ya Magufuli Tanzania itakuwa salama...