Spika Tulia Ackson: Mtu akimsema vibaya Rais nyooka naye, akinisema vibaya Nyooka naye
Rais mwenyewe alitoa go ahead ya kukosolewa, isipokuwa angalizo ni iwe kwa staha...

Huyo Tulia hakusikia hayo maneno au ni mwendo wa kutafutwa kulambishwa asali
 
Mlishangilia sana hawa mbwa walivyowashughulikia panya road bila kufuata au kujali haki ya mtu hata kama ni mtuhumiwa, hawana sababu ya kuheshimu haki ya raia maana wote sasa ni panya road, Nyerere alisema vizuri sana kuhusu dhambi ya ukabila, walianza na panya road sasa wasiokubaliana nao ni panya road na kitakachofuata watageuzana panya road wenyewe kwa wenyewe
 
Wakuu nawaletea kideo, spika wa bunge akiwataka vijana kushughulika na yeyote anayemsema vibaya Rais, Mbunge, Diwani au Mwenyekiti wa mtaa kwa tiketi ya CCM.

Hivi karibuni kuna ndugu wa Temeke alisema wao kazi yao ni kuwashugulikia wakosoaji na wazee watawaombea radhi kwa watanzania.

Sijui nataka niseme nini ila pateni kideo hapo.
View attachment 2375676

========

Akihutubia Vijana wa CCM katika Jimbo lake, Mbunge wa Jimbo ya Mbeya Mjini ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka vijana wa Jimbo hilo kutoshiriki katika Kumsema vibaya, Rais na Viongozi wa Jimbo hilo

Amesema, “Isitokee Kijana yeyote anaungana na mtu yeyote anayemsema vibaya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Samia ni Rais wa Nchi lakini pia ni mwenyekiti wa Chama chetu. Asitokee mtu yeyote wa Nje ya Chama, wa Ndani ya Chama akawa anamsema vibaya Rais halafu wewe ukamtazama, shughulika naye, CCM hoyeeeee”

Ameendelea, “hata mimi Mbunge wako akiwa ananisema vibaya nyooka naye, unajua sababu ni nini? Hata Diwani, Madiwani wote wa Mbeya Mjini sasa hivi ni CCM, hata akimsema vibaya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, na yeye ni CCM, nyooka naye’
Huyu Tulia alivyo mbaya wa sura na ata roho na akili yake ni mbaya!
Ndio maana balozi wa US leo amemtembelea mh.Sugu na kuachana na mbunge wa wizi wa kura,ni aibu na msg tosha kuwa dhulma hailipi..ni suala la muda tu ataanza kulipia uovu wake,ubaya haujawahi kushinda wema.
 
Akili kichwani mwako, hakuna mtu atakuja kukuletea ugali au kukutoa lupango, ukishuhulika utashuhulikiwa
 
Wakuu nawaletea kideo, spika wa bunge akiwataka vijana kushughulika na yeyote anayemsema vibaya Rais, Mbunge, Diwani au Mwenyekiti wa mtaa kwa tiketi ya CCM.

Hivi karibuni kuna ndugu wa Temeke alisema wao kazi yao ni kuwashugulikia wakosoaji na wazee watawaombea radhi kwa watanzania.

Sijui nataka niseme nini ila pateni kideo hapo.
View attachment 2375676

========

Akihutubia Vijana wa CCM katika Jimbo lake, Mbunge wa Jimbo ya Mbeya Mjini ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka vijana wa Jimbo hilo kutoshiriki katika Kumsema vibaya, Rais na Viongozi wa Jimbo hilo

Amesema, “Isitokee Kijana yeyote anaungana na mtu yeyote anayemsema vibaya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Rais Samia ni Rais wa Nchi lakini pia ni mwenyekiti wa Chama chetu. Asitokee mtu yeyote wa Nje ya Chama, wa Ndani ya Chama akawa anamsema vibaya Rais halafu wewe ukamtazama, shughulika naye, CCM hoyeeeee”

Ameendelea, “hata mimi Mbunge wako akiwa ananisema vibaya nyooka naye, unajua sababu ni nini? Hata Diwani, Madiwani wote wa Mbeya Mjini sasa hivi ni CCM, hata akimsema vibaya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, na yeye ni CCM, nyooka naye’
Duh !!
 
Yupo sahihi ikiwa anawaambia Vijana wake wa CCM.
Ila hayuko sahihi Kama atakuwa anamaanisha vijana wa nchi nzima.

Kama ndio Katiba ya ccm ndivyo isemavyo yupo sahihi
Definitions ya kushughulika naye na nyooka naye ni nini ?? !! Mimi nashangaa nimeshindwa kuelewa naona maruweruwe !! Sitaki mtu anyooke na mimi !!
 
Hii kauli tu KWANZA ni uchochezi, yeye anafikili KWa akili yake na Kama kiongozi hao vijana walifanya hivyo vijana wa upande mwingine wakajibu mapigo Kuna tanzania hapo

Na anafikili rais wa nchi ni wa ccm tu au watanzania wote

Ni shida kuwa na viongozi wa namna hii kwenye taifa lolote, mauaji ya kimbali huanza na kauli za ajabu za namna hii na KWa kauli hii ndani ya nchi pitia KWa vijana hao inatosha kabisa ndani ya nchi

Kutoendelea kalia kiti alichonacho, kufukuzwa ndani ya chama Chake na Kama haitoshi ,kuburuzwa mahakani , hizi ni kauri Hatari Sana KWa maslahi mapana ya taifa,

I wish angekua SA akutane na MALEMA na kauli yake hii , tuone Kama angekalia hicho kiti KWa siku 2

Kauli ya Tulia ina maslahi mapana ya umma na taifa Mara 10 ya ile ya Ndugai, anatakiwa kujiuzuru Mara MOJA,
Aombe radhi tu yaishe kama na yeye ataona ulimi uliteleza tu na kwamba hakuwa na maana mbaya!! Mimi sitaki mtu anyooke na mimi kwa kweli !!
 
Baadhi ya viongozi wapo kibahati mbaya tu kwenye nafasi zao

Laiti wangejua nguvu ya maneno wangechuja kabla ya kuyatoa
 
Back
Top Bottom