Spika Tulia Ackson: Mtu akimsema vibaya Rais nyooka naye, akinisema vibaya Nyooka naye
Wakuu nawaletea kideo, spika wa bunge akiwataka vijana kushughulika na yeyote anayemsema vibaya Rais, Mbunge, Diwani au Mwenyekiti wa mtaa kwa tiketi ya CCM...
Ukiwa kiongozi kusemwa vibaya ni kawaida,cha msingi unahitajika uvumilivu mkubwa
 
Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amewasihi vijana wote nchini hususani wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuendelea kushikamana na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo kumpigania Rais wake.

Dkt. Tulia ameyasema hayo Jijini Mbeya wakati akizungumza na Vijana wa CCM hamasa Wilaya na kuwaeleza kuwa ni jukumu la kila Mwananchi hususani Vijana kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kulipigania na kulitetea taifa lao kwakuwa wao ndio nguvu kazi.

Zaidi ya yote Dkt. Tulia amewataka vijana hao kutoa taarifa kwa Viongozi wao wa Chama pindi inapotokea wamepata taarifa zozote zenye viashiria vya kuichafua nchi au chama chao ili Viongozi hao waweze kutafuta ufumbuzi wa haraka.

“Isitokee kijana yeyote anaungana na mtu yeyote iwe ndani ya chama au nje ya chama kumsema vibaya Rais wa Nchi yetu, Mama Samia ni Rais wa nchi lakini pia ni Mwenyekiti wa chama chetu” amesisitiza Dkt. Tulia
 
Hizi kauri sio nzuri, maana watu unaowaeleza huwajui uelewa wao ukoje, nahujui watakao sikia nao wataichukulia vipi kauli hiyo, harafu yakitokea yakutokea tunaanza kulilaumu jeshi la police kushindwa kuzibiti cjui nini nini , kama Mungu anasemwa vibaya sembuse na Rais? Amani na uturivu wa nchi niwajibu wakulindwa na kila mtu .
 
Wakuu nawaletea kideo, spika wa bunge akiwataka vijana kushughulika na yeyote anayemsema vibaya Rais, Mbunge, Diwani au Mwenyekiti wa mtaa kwa tiketi ya CCM...
Kinga walomwekea SPIKA ya kutoshtakiwa iondolewe,

Iliwekwa kihuni, iondolewe kihuni.
 
Maoni ya ki ibirisi kabisa, hafu j.pili utakutana naye kanisani🤣🤣🤣
Vimaneno maneno hutu hutu huwa nichanzo cha machafuko..! Shetani naye alianza hivi hivi, nitakiinua kiti changu nk nk, mala pah! Ikatokea vita mbinguni , huyu mama sikutegea atoe kauri kama za mdude chadema.

Naanza sasa kuwaelewa akina mdude.
 
Spika wa Bunge la Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amewasihi vijana wote nchini hususani wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuendelea kushikamana na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo kumpigania Rais wake.

Dkt. Tulia ameyasema hayo Jijini Mbeya wakati akizungumza na Vijana wa CCM hamasa Wilaya na kuwaeleza kuwa ni jukumu la kila Mwananchi hususani Vijana kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele kulipigania na kulitetea taifa lao kwakuwa wao ndio nguvu kazi.

Zaidi ya yote Dkt. Tulia amewataka vijana hao kutoa taarifa kwa Viongozi wao wa Chama pindi inapotokea wamepata taarifa zozote zenye viashiria vya kuichafua nchi au chama chao ili Viongozi hao waweze kutafuta ufumbuzi wa haraka.

“Isitokee kijana yeyote anaungana na mtu yeyote iwe ndani ya chama au nje ya chama kumsema vibaya Rais wa Nchi yetu, Mama Samia ni Rais wa nchi lakini pia ni Mwenyekiti wa chama chetu” amesisitiza Dkt. Tulia
 
Tuwe wakweli tu Bavicha kama Mdude Chadema anavumilika kweli?

UVCCM wakinyooka naye mtamlaumu Prof Tulia kweli?

Hata Mh Freeman Mbowe alilaani sana mihemuko ya Bavicha
 
Watoto wa chadema utadhani wamejizaa hawana heshima Kabisa Kwa wakubwa zao kiumri na hawaheshimu wadogo zao. Hawa usipowaendesha Kwa mkong'oto wanakupanda kichwani
 
Wakuu nawaletea kideo, spika wa bunge akiwataka vijana kushughulika na yeyote anayemsema vibaya Rais, Mbunge, Diwani au Mwenyekiti wa mtaa kwa tiketi ya CCM...
Kwamba imebidi Tulia atoke nduki kumkimbiza mdude alosepa na nguo zake?

Chama Cha Mapunduzi kimeamua kuyatumia MAPANGA yalotumika ktk Mapinduzi enzi zileee!

Tulia ametangaza vita kupitia Jeshi la uvcc!!!!
 
Back
Top Bottom