Tabia ya Hawa wafanyakazi wenzangu, inaninyima raha

Kweli binadamu tuko tofauti yaani Kuna watu kwao aibu hakuna kabisa
 
Vijana wengi walionunua magari lengo lao kuu ni kubeba mademu tu hamma la maana .
Sio kweli mkuu, lengo la kununua gari ni kuondoa adha ya usafiri.
Pia kukupa uhuru wa mambo yako
 
Punguza wema mkuu,binadamu wenyewe hawana hata kumbukumbu hawa.

Aliyekuazima gari siku akila mzinga huko utajiona mjinga sana!

Gari aazimishwe/apewe mwenye gari tu,hawa wasiokuwa hata na uzoefu barabarani ni kutafuta lawama.
Na ukimlipisha atakuona una roho mbaya
 
Hii nayo mbinu nzuri naichukua
 
Hizo ndio sifa za umasikini huna gari unaenda omba gari ya jirani unaitumia huweki mafuta wala safisha nawakati mwingine unaibonda only in Africa kuna mshikaji aliuwa gari na akauza kwa ujinga huu
Kuna Mmoja nilimpa karudi nayo imechubuka rangi mbele akaniambia dereva guta aliikwangua.
Nkaenda kupiga rangi kwa gharama zangu.
Kuna huyu mwingine anaondoka na gari gia kaweka namba Moja halafu anakanyaga mafuta mpaka mwisho Hadi gari inalalamika. Yaani uendeshaji wake hata simuelewielewi, watakuja kuniulia gari hawa
 
Hii tabia alikuwa nayo Babu yangu mmoja mkienda msikitini mkimaliza kuswali anakuja na nyie kwa Miguu anaiacha Gari na akiacha Gari mkiwa njiani anasema amesahau Gari anarudi kuichukua Ila lengo alikuwa hataki mtu apande hilo Gari.

Ni mwaka juzi lile Gari watoto wake wameshalipima .na Babu is no longer alive

So keep spread positive Energy nothing last.
 
Yaani urafiki wa kazini uishie kazini.
Watu tunahitaji kuwa na maisha mengine huku nje.
Hii wafanyakazi wengi Huwa inatupa ugumu.
Unakuta marafiki ni walewale wa kazini mnashindwa hata kujadili vitu vipya, mnashindwa mnaongelea mambo yaleyale
 
Mfumo wa ujamaa umewaharibi sana watu, wanageuza msaada kuwa haki,
Inabidi utambue Mali ya mtu mwingine huna haki nayo.
Lazima mtu ujifunze kujitegemea sio kusubiri hisani
 
Gari la kwanza ni sadaka ukija kununua la pili usiwakubalie.
 
Wapakie na waeleze kuhusu ratiba zako, hata kama kuna mahali unakwenda, nenda huko na park gari yako, washuke wakusubiri.
Kuhusu kuazima gari, wanyime.
Usiwe muoga kwenye kitu chako, unless nawe uwe uliishi maisha hayo kabla haujapata gari.
Mimi sikuwahi kuazima gari la mtu Wala kuomba lift.
Kwanza Huwa Sina mazoea sana na watu hapa kazini,zaidi ya wachache ambao utendaji wetu wa kazi unaingiliana.
Hawa wanaoniomba lift sikuwahi kuzoeana nao,wameanza mazoea baada ya kununua hii gari.
Kuna mwingine wiki iliyopita kaniazima gari limerudi mafuta yote kanitumia akaanza kujiongelesha kuwa posho za vikao zikitoka atanipoza.
Posho za vikao zimetoka kakaa kimya tu nami sijamkumbusha.
Ijumaa kanifata eti nimpe gari aende supermarket nikamwambia kuwa Nina ratiba ya kutoka muda sio mrefu
 
Hiyo ya pili inanikuta sana hiyo.
 
Mtu akikukuta unakula chakula no ukamkaribisha. Huwa unamuuliza kwanza hayo maswali? Au huko kwenu hata chakula na majirani hamkaribishani?
Mtaani kwako mtu akipata shida ya ghafla usiku na hana gari wala pesa utaweza kumsaida kweli wewe?
hyo ni shida muhimu dharura lazma kusaidia.
Ila lift kuomba ni aibu yan kila siku umekaza mshipa lift
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…