TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
MENEJA TANESCO

NAOMBA MSAADAAA NYUMBA YA MAMA IMEUNGUA KONGOWE YA MBAGALA HAPO
 
Itabidi rais afukuze watendaji wa Tanesco wengi aturudishie net solution ya South Africa ilijua kuisimamia Tanesco
 
0748550000 hii no ni TANESCO INAISHIWA CHAJI KWA SABABU UMEME UNAKATIK?
 
Tangia ile asubuhi hamna umeme na siku za deadline zimekaribia walipewa miezi 6 sasa miezi 5 tayari lakini haionyeshi matumaini kuwa wamebadirika

Shirika la kipuusi sana hili
 
Habari ndugu mteja ahsante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto, ombilako lenye namba 021023-0921 na jina AUREUS CHARLES NDIMBO, lipo hatua ya kuunganishwa na huduma wakati wowote kuanzia sasa watalamu wetu watakufikia na kukupatia huduma.^OK
Kwa nini mnaleta umeme mdogo hasa maeneo ya Dar, inafika hatua fridge guard hairuhusu umeme unakuwa mdogo hadi uunganishe direct, na vifaa kama feni vinakuwa havina nguvu.....au mna kampeni ya kutuharibia vifaa, ukichukulia hivi vifaa vinanunuliwa kwa bei ghali.

Toa ushauri, huu umeme mdogo ni salama kwa matumizi ya vifaa au tuzime tusije ingia hasara.​
 
Kwa nini mnaleta umeme mdogo hasa maeneo ya Dar, inafika hatua fridge guard hairuhusu umeme unakuwa mdogo hadi uunganishe direct, na vifaa kama feni vinakuwa havina nguvu.....au mna kampeni ya kutuharibia vifaa, ukichukulia hivi vifaa vinanunuliwa kwa bei ghali.

Toa ushauri, huu umeme mdogo ni salama kwa matumizi ya vifaa au tuzime tusije ingia hasara.​
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto hiyo, tunashauri endapo mkipata changamoto hiyo ni vyema mkazima vifaa vya umeme ili kuepusha uharibifu.^OK
 
Nimeenda mara mbili ofisi za TANESCO Yombo (Buza) kuliripoti tatizo la nguzo kuoza na kuinama hadi nyaya zinazoingia ndani kukaribia kugusa chini wananipa namba za simu za TANESCO nipige kuripoti hilo tatizo, wao watakuja kutengeneza baada ya kupewa taarifa hizo na TANESCO ninayoipigia simu.

Sasa ile ofisi pale inafanya kazi gani? Hizo namba nimepiga mara nne wanachukua maelezo tu hakuna kilichofanyika toka tarehe 9 Jan 2024 na mimi nakaa chini ya 1KM toka ofisi za TANESCO Yombo (Buza).

Haya ni maajabu, unaenda kuripoti tatizo ofisi za TANESCO unapewa namba za simu za TANESCO ili upige kuelezea tatizo lako na hakuna kitu kinafanyika
 
Yani kuna maeneo kila siku umeme shida,then unakuta mitaaa mingine hao hata hawajua hiyo shida, kuna maeneo ni kuonea watu, ni kama laini ya majaribio
 
Tanesco mmeniunguzia laptop yangu. Nawaambia mtanilipa siendi mahakamani sababu system sio rafiki lakini mtanilipa
 
Kutukatia umeme huku Nzuguni Dodoma wakati tunajitayarisha kuangalia mpira final ya AFCON maana yake nini jamani!!!! Mnaudhi kweli!!!
 
tanesco mkikata umeme kwa wengine ni fgursa..
ngoja nichangamkie hii fursa ya giza nitimize malengo yangu ya kujenga ghorofa kama la Mwijaku
 
Back
Top Bottom