Mla Bata
JF-Expert Member
- Jan 24, 2013
- 8,461
- 19,779
- Thread starter
- #61
Sadly, Ni kweli Binti wa zamani JF imekuwa zaidi ya jukwaa la kubadilishana mawazo, kwa wengi wetu imekuwa sehemu ya kujenga urafiki na mahusiano ya kweli ambayo mengine yameendelea, na mengine yakapotea kadri muda ulivyosonga. Ni matumaini yetu kwamba wale wote tuliowahi kuwa karibu nao humu wako salama popote walipo. 🤝🏾❤️Very well put 💯
Mimi kuna watu kadhaa nilishakutana nao humu na tukatengeneza mahusiano mazuri japo wengi hatujawahi kuonana ana kwa ana.
Kuna mtu mmoja kutoka JF nilishawahi kuwa na ukaribu naye humu mpaka nisipoongea naye najisikia kama kuna kitu nimekikosa, hatukuwahi kuonana ila genuinely alinigusa. From time to time huwa namkumbuka, nina audio ya sauti yake aliacha kwenye voicemail huwa naisikiliza nikimkumbuka. Overtime mawasiliano yetu yalipungua na mpaka mwisho yakakata kabisa na sina namna ya kumpata tena. I hope all is well with them!