PostGE2025 Tume imetambua vifo 518 wakati wa maandamano ya Mo29. Wamekiri, watatokaje?

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Hii inabidi utamke kwa uangalifu sana.
Watu ambao hawajapatikana na walionekana wameuwawa mbele ya ndugu zao maiti zimepotelea wapi?
Goba jirani yetu tumezika nguo, alipigwa risasi ubongo ukamwagika mbele ya mdogo wake.
Kama hujui bora unyamaze.

Wewe unauthibitisho wa uwepo wa hilo kaburi?
 
Vifo ni vifo. Wapumzike kwa amani.

Mtu yeyote timamu alijua idadi ya 10k plus haikua na uhalisia na kaburi la halaiki ni story feki. Hii sio kumtetea Hangaya bali ndo uhalisia. Hatua ichukuliwe kwa hata kama mtu mmoja tu alipoteza maisha.
Hao wachache walizikwa wapi?
 
Anaweza kuwa sawa kwa mujibu wa takwimu walizopata, hizo takwimu nyingine ulizonazo mkuu ni za kwako sio walizopokea wao.
Yaani mauwaji wafanye wao na Tume yenye kila aina ya sources za taarifa na support ya serikali washindwe kujua data sahihi za vifo?, hivi huwa mnawaza kwa kutumia akili gani?, hiyo ni Tume iliyo chini ya Serikali kuu toka kwa rais kumbuka hilo na sio Tume ya mtu binafsi ambaye hawezi kupata nafasi ya kuingilia baadhi ya mifumo .
Tukubali tu hawawezi kuunda Chombo kitakachofunua ushenzi walioufanya, ni aibu
 
Sijui. Wewe unajua walipozikwa?
Kuna mtu anayejua basi?

Katika ripoti jambo hilo halikusemwa, bali wametajwa waliozikwa na ndugu zao tu na Polisi hawakutajwa katika mauaji ya holela.

Kwenye utekaji hakuna ilipotajwa Serikali kuhusika, bali ni kujiteka, kutekwa kwa fitina nk nk.

Ripoti yenye kuegemea upande ilikuwa ni ya kusafisha watawala.
 
Kuna list ya waliopotea ni maelfu kwa maelfu. Kama hujapoteza mtu wewe una bahati. List ni ndefu, wewe chawa haikuhusu.
 
Hayati mheshimiwa aliyekuwa wizara ya wanaoumwa alikuwa na idadi kamili na huenda taarifa alizokuwa nazo ndizo zilizomharakisha kwenda kuzimu.
Idadi ya mchongo. Alipenda sana kuwaita wanyonge na nyie mnakenua tu huku yeye anapiga pesa. Ila huyu ni kiboko kabisa. Anawapiga live huku anawachamba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…