Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA

Uchaguzi 2020 Tume ya Uchaguzi yampitisha Tundu Lissu kuwania Urais kupitia CHADEMA

Leo ndio leo.....[emoji3][emoji3][emoji119][emoji119]
 
Tume kuchelewa kuamua hatima ya Lissu ni kuendelea kumpa umaarufu wa ziada pasipo sababu.

Huyu alipaswa asitumie hata dakika 5 hapo tume.
Siku zote, wamwisho huja kuwa wa kwanza. Lisu akiruka kiunzi hiki MUNGU anaachia Baraka zake.
 
Mhe. Tundu Lissu Kunguruma leo kwenye ofisi za Uchaguzi Dodoma akirejesha Form ya Kugombea Urais wa Tanzania

Updates
----
Tayari Mweshimiwa Tundu Lissu ambae ni mgombea urais na makamu wake Salum Mwalim wameshafika kwenye ofisi za tume ya Uchaguzi kwa urejeshaji wa Form

UPDATE:-
Tumehifadhiwa kwenye holding room ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi hapa Dodoma kusubiri kuitwa ndani kwa ajili ya uteuzi!

UPDATE:- 9:40
Mgombea wa CCM John Pombe Magufuli hakumali nusu saa kwenye Tume na fomu zake zimepokelewa, akateuliwa na kuondoka. Sisi wengine fomu zetu zinakaguliwa tangu saa sita mchana kwa utaratibu gani wa Sheria ya Uchaguzi na Kanuni za Uchaguzi wa Rais na Wabunge? Upendeleo huu wa nini?
10:13
Kwa ajili ya kusimamia utaratibu wa kisheria, fomu za mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CHADEMA mhe. Tundu Lissu hazikupita kwa Wasimamizi wa Majimbo ya uchaguzi kwa ajili ya zoezi la uhakiki. Zoezi la uhakiki ndio linaloendelea kwa sasa.
Wala hatuhitaji haya maelezo maana ni uzembe wakiwango cha reli ya SGR. Ina kuwa kama ni mara ya kwanza Chadema wana shiriki uchaguzi?? Ngoja wamalize uambiwe mgombea mwenza hayupo. Yatokee ya CCK au wamesahau risiti au picha zao.. Yaani Chadema mmekuja kuwa mwendo kasi kama kitoko.
 
I buy your reasoning.
CCM na vyombo vya baadhi ya viongozi wa vyombo vya dola hawaaminiki hata kidogo. Pengine wana "buy time" muda uende na jioni ifikike, watu walipuke kwa furaha na kufanya maandamano ili waovu wafanye vitu vyao. Yasije yakajirudia yale ya yule binti mdogo Acquilina.


Wanausalama wa CDM wawe makini mno nyakati za usiku. Dodoma hapaaminiki kwa usalama wa viongozi wa CDM. Pengine kuna magenge ya watu wasiojulikana wenye nia ovu wapo kazini kimkakati, kwa maelekezo maalum ya watu wenye hofu nyingi juu ya Lissu wanaojulikana.
 
Angalia ratiba NEC walimpangia saa 6:00 mpaka saa 6:15 akiwa mtu wa 10.
Cha ajabu CUF walikuwa ni wa 12 wamepitishwa.
Kajaza wadhamini maelfu tume haiwezi hakiki hao wadhamini maelfu ndani ya dakika kumi inataka muda
 
Tunamtaka Lissu.Lissu ni mtanzania mwenzetu na tunataka tumpigie kura.


Mie na familia yangu kura ni kwa Lissu.Watumishi wote kura ni kwa lissu
 
Back
Top Bottom