Tundu Lissu adai Hayati Magufuli ndiye aliyeagiza shambulio la kupigwa risasi dhidi yake Dodoma

Tundu Lissu adai Hayati Magufuli ndiye aliyeagiza shambulio la kupigwa risasi dhidi yake Dodoma

Kipi kipimo cha usaliti?

Unapimwaje? [emoji2369]

Je sheria ina-define vipi usaliti?

Ikithibitika adhabu yake ni nini?

Je sheria imesema auwawe ?

Kwanini asishitakiwe kwenye vyombo vya haki?

..halafu Deo Mwanyika mshirika wake kwenye "usaliti" akapewa ubunge wa CCM jimbo la Njombe

..halafu usd 191 tulizodai tumeibiwa, na Lissu akasema ni kanyaboya, na Magufuli akamuita msaliti, Prof.Kabudi amejitokeza na kuthibitisha ilikuwa ni madai ya uongo.
 
Kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 Lissu amesema aliyetoa mari, masaa mawili kabla hajapigwa risasi alisema kulikua na mtu anahutubia na kwenye hotuba yake alikuwa anapokea ripoti ya Bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite, moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba hiyo ni;

"Wale wanaopinga nchi wakati tupo kwenye vita ya kiuchumi nyie wanajeshi mnajua huwa wanafanywaje, hawastahili kuishi."

Ambapo masaa mawili baadae Lissu alishambuliwa Dodoma, akisema bayana kuwa anayemuongelea ni Hayati John Pombe Magufuli, ambapo hata baada ya tukio hilo Rais Magufuli hakuwahi kusema chochote juu ya shambulio hilo.

View attachment 2504783
Yule jamaa alikuwa na roho mbaya mno.
 
Ulikuwepo nchini wakati wa utawala wa dikteta Magufuli?

Yeye ndiye alikuwa nchi. Yeye ndiye alikuwa katiba. Yeye alikuwa bunge, yeye alikuwa mahakama.

Kwa hiyo kumpinga yeye ilikuwa unapinga nchi. Lisu alikuwa anampinga dikteta Magufuli kuzuia exports za concentrates bila ya kufuata sheria.
Hujui kitu wew
 
Alikuwa kinyume na maamuzi ya dikteta Magufuli.

Note:

Kwenye utawala wa kidikteta, dikteta hujiona yeye ndiyo nchi.

Lisu afutwe uwanachama wa chadema. Maana badala ya kueneza sera za chama kimekuja na nini kipya. Yeye analeta za akina Magufuli. Ambazo zimepitwa na wakati, na ambazo hazina tija kwa taifa.
 
Kwenye mahojiano na kipindi cha Clouds 360 Lissu amesema aliyetoa mari, masaa mawili kabla hajapigwa risasi alisema kulikua na mtu anahutubia na kwenye hotuba yake alikuwa anapokea ripoti ya Bunge ya madini ya Almasi na Tanzanite, moja ya mambo aliyoyasema kwenye hotuba hiyo ni;

"Wale wanaopinga nchi wakati tupo kwenye vita ya kiuchumi nyie wanajeshi mnajua huwa wanafanywaje, hawastahili kuishi."

Ambapo masaa mawili baadae Lissu alishambuliwa Dodoma, akisema bayana kuwa anayemuongelea ni Hayati John Pombe Magufuli, ambapo hata baada ya tukio hilo Rais Magufuli hakuwahi kusema chochote juu ya shambulio hilo.

View attachment 2504783
Oooohoooo!! Kumekucha sasa ngoja waje wafia legacy!! Ila Lisu hapindishi maneno 🤣🤣🤣
 
Rais wa JMT kimsingi ndiye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, kumkashifu au kumdhulia jambo Rais wa JMT ni kuidharau CCM.

Sera za CCM zinajulikana na ndizo zinazotekelezwa na Serikali.

Ni vema Tundu Lissu pamoja na Kituo kilichorusha Uzushi huo vikahojiwa na vyombo husika.

Mlale Unono!
 
Back
Top Bottom