PreGE2025 Tundu Lissu amegoma kesi yake kuendeshwa kwa njia ya Mtandao. Kesi yaendelea Mahakamani

PreGE2025 Tundu Lissu amegoma kesi yake kuendeshwa kwa njia ya Mtandao. Kesi yaendelea Mahakamani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Endelea kusubiri.....Lissu hafi leo wala kesho. Note my words
Mkuu mimi ni shabiki wa lissu mkuu, ila narrative ya kwamba sa100 atamuacha lissu, au lissu atamuacha sa100. Hii hakuna anajua nani anaondoka lini mkuu. Ni mambo ya ajabu kusema fulani ndo atawahi, wametangulia watu wema kibao, wametangulia watu wabaya kibao, wametangulia watu wenyw afya njema kibao, wametangulia wenyw afya zoofu kibao, wametangulia watoto kibao , wametangulia wazee kibao.

Au nasema uongo mkuu?🤣
 
Nyie watu mkoje. Unataka kusema kuangalia Mpira uwanjani na kuangalia kwenye TV ni sawa?

Mpira wa kuangalia kwenye TV anayedhibiti mtazamani aone nini ni muonyeshaji wakati uwanjani ni mtazamani ndiye anayeamua aangalie nini.

Ukisema "Visual Court" ni sawa na mahakama ya kawaida Sasa Kwa nini majina hayafanani?
Hivi ndugu unawezaje kuelimisha haya mazwazwa na vilaza wa CCM!!!??
Hayo hayana ubongo, ni empty empty empty!
 

Attachments

  • downloadfile-2.jpg
    downloadfile-2.jpg
    180 KB · Views: 13
  • downloadfile-18.jpg
    downloadfile-18.jpg
    216.9 KB · Views: 14
  • JamiiForums-1270582057.jpeg
    JamiiForums-1270582057.jpeg
    32.5 KB · Views: 13
Mkuu mimi ni shabiki wa lissu mkuu, ila narrative ya kwamba sa100 atamuacha lissu, au lissu atamuacha sa100. Hii hakuna anajua nani anaondoka lini mkuu. Ni mambo ya ajabu kusema fulani ndo atawahi, wametangulia watu wema kibao, wametangulia watu wabaya kibao, wametangulia watu wenyw afya njema kibao, wametangulia wenyw afya zoofu kibao, wametangulia watoto kibao , wametangulia wazee kibao.

Au nasema uongo mkuu?🤣
Hahahah......Lissu hafi leo wala kesho. Chukua huu ujumbe wangu acha ubishi
 
Marekani haijakosea kujenga GEREZA la GWANTINAMO ukiingia humo hutoki labda baada ya miaka 30.
 
Ndio siasa zenyewe, dawa ya kiburi ni ununda na maarifa zaidi! Iwe stunts au kingine utakavyodefine yote sawa!
Watunushiane tu, hainipunguzi ugali,. matter of fact nikale sembe langu mapema.

Indeed my definition and any ion is mine.
 
huenda mgeni wa technologia ndie pekee hajui changamoto za technolojia,
huenda pia hafatilii kesi za mahakama ya ICC na mambo mengine mathalani hata uapishao wa Trump nini kilitokea kuhusu technolojia,

hata hivyo,
kesi zoto nchini zinaendeshwa kwa technolojia na hii sio ya kwanza.
basi wacha tusubiri hizo siku 30 zijazo tutamsikiliza huko huko mahabusu,

na sasa arudishwe korokoroni:NoGodNo:
Kwani yeye amekwambia ana shida yeyote akikaa mahabusu.
 
Kwani anaficha nini?

Si yeye kutwa anapiga kelele kutaka uwazi
Hiyo kesi iendeshwe kwa uwazi ili kila mtu aone haki inatendeka sio baadaye aje na porojo zake kuwa majaji hawajui kingereza na hawakutenda haki sababu ni CCM

Ifanyike live dunia yote ione
Ndio, lakini lazima awe mahakamani live. Mitandao ya bungu ni magumashi matupu.
 
Tulifungua Mahakama za Wahujumu Uchumi kwa gharama na mbwembwe nyingi mpaka leo majengo yanaoza hayajawahi endesha kesi hata moja ikaisha😀😀
Ulifungua weye na nani?

Tuwekee picha, hivi unajua hata mtaa gani zilipo hizo mahakama.

Utoke Bushi huko utajuaje, nimesahau.
 
punguza mihemko muerevu wacha kujipiga kifua with nonsense point,

unaogopa technolojia hali ya kua umeililia hadi kwenye chaguzi halafu tena ng'we ng'we ghafala hutaki tena technolojia,

kasongo bana, kweli mbona weo:pedroP:
20250424_104020.jpg

Hivyo vifungu visome usijifanye mjinga kwa kufuata mihemko ya kiccm. Kuna sheria zake zinaoztaka kesi zisikilizwe kwa njia ya mtandao nasio hayo maujinga yenu mnayomezeshana huko lumumba kisa buku 5 ya kununulia bando.
 
Mnaolalamika kuwa Tz hawawezi kustream, Mbona mzigo upo hewani na hata mada hii inasema hvy na hakuna tatizo la kimtandao, em tuache mazoea.
 
Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amegoma kusikiliza kesi ya Uhaini inayomkabili kwa njia ya mtandao hii ni kwa mujibu wa mawakili wake. Lissu alipaswa kufikishwa Mahakamani leo ili kufatilia mwenendo wa kesi hii.

Pia soma > LIVE - Kisutu: Kesi ya Tundu Lissu leo itaendeshwa kwa njia ya Mtandao. Kila Mtu huru kusikiliza

View attachment 3313918

Sasisho kesi ya Lissu kwa Mujibu wa Hilda Newton kutoka mtandao X

Kesi imeanza kusikilizwa Mbele ya Mh. Hakimu Mhini

Mawakili wa utetezi wamefika lakini waserikali na mtuhumiwa watakuwa kwa njia ya mtandao.

Muda huu anaonekana kwenye screen afisa wa magereza (sijui kama ni mkuu wa gereza) lakini Mh. Lissu haonekani. Kesi inaelekea kuanza hapa.

Mawakili wa serikali wanaulizwa wapo tayari nao hawaonekani kwa sasa. Maana wanaendesha kesi kwa njia ya mtandao.

Wakili Mpale Mpoki anasema upande wa utetezi tuko tayari na upande wa serikali walikuwa na taarifa ya kesi na wanajua tarehe ya kesi kwahiyo anasisitiza tuendeleeee

Upande wa Jamhuri tuko tayari, anasikiki Wakili wa Serikali anasema hivyo. Wanaulizwa Magereza mko tayari? Anajibu askari magereza huyu afisa anasema Mshitakiwa amegoma kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao.

Anasema nimemjulisha mtuhumiwa na amegoma kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao kwahiyo amegoma

Upande wa Jamhuri tupo, Job Mrema wakili wa serikali mwandamizi niko pamoja na

Nassoro Katuga PSA
Cathbert Mbiringi , Tuko tayari kuendelea na Shauri. Shauri lilikuja kwa maelezo ya awali. Ameambiwa atulie kwanza

Utetezi wanajitambulishaa anasema mzee Mpale Mpoki
Alute Mugwai
Ruge Nshala
Peter Kibatala
Jeremiah Mtobesya
Nashon Nkungu
Gaston Garubindi
Deus Singa
Eben Silayo
Deogratias Cosmas Mahinyila
Edson Kilatu
Fredrick Kihwelo
Michael Mwangasa
Catheters Rafael Mandiho
Dickson Matata
Emanuel Chengula
Paul Kisabo
Edward Heche
Jebra Kambole
Maria Mushi
Sisty Masawe
Ikoti Lissu
Fredrick Msaki
Jacob Mogendi
Fikiri Gabriel
Florian Francis
Hekima Mwasipu
Emmanuel Ukashu.

Wakili Mpale Mpoki Anamaliza kutambulisha jopo la Mawakili wa Utetezi.

Wakili wa Serikali Job Mrema anasema yuko tayari kuendelea na shauri ambalo liipangwa kwa ajili ya maelezo ya awali na upande wa jamhuri tuko tayari lakini mshitakiwa hayupo hapo.

Anasema tumewaserve utetezi maelezo ya awali leo asubuhi kupitia wakili Hekima Mwasipu.

Shauri hili lilokuja kwa maelezo hayo na mshitakiwa hayupo mbele ya Mahakama. Kutokana na hali hiyo tuliyoipata kutoka magereza. Kwa upande wa jamhuri tunaomba ahirisho la shauri hili kwa tarehe nyingine.

Ambapo tunaomba kwa upande wa jamhuri tupewe mwezi mmoja kutoka sasa. Watu wanaguna hapa mahakamani.

Anaendelea ili mawakili upande wa utetezi waongee namtuhumiwa ili akubali kuja kusomewa maelezo ya awali.

Hakimu anamuuliza umemaliza au bado?

Anasema Job Mrema Wakili wa serikali kuwa nimemaliza mheshimiwa.

Itaendelea post inayofuata!…..


Anaanza upande wa utetezi Wakili Mpale Mpoki

Anaongea kingereza Ila nitatafsiri hapa.😂

Hata kama Mtuhumiwa aangekuwepo (vituraly) leo, tusingeweza kuendelea kwasababu ingekuwa ni kinyume na sheria kwa sababu sheria inataka maelezo ya awali yafanyike mtuhumiwa akiwepo.

Jambo lingine upande wa utetezi tnajitaji kupata nafasi ya kuonana na mteja wetu. Tumenyimwa kabisa kuonana nae toka amekamatwa kwa ajili ya kumuandaa ili asomewe hoja za awali.

Na sababu za hili kushjndikana ni Magereza kupitia maafisa wake wametukataza mawakili tusionane na mteja wetu licha ya hatua mbalimbali tulizofanya kuonana na mteja wetu Tundu Lissu. Jan na juzi tumekaaa zaidi ya masaa saba na juzi pia tulikaaa masaa nane kuingia na baadae akaruhusiwa wakili mmoja tu kunuona mteja.

Wakili mmoja aliyeruhusiwa kumuona kwa dakika 15 tu na huyo aliruhusiwa kumuona kama ndugu. Hivyo basi nasisitiza hata angekuwepo tusingeleea kwasaabbu hatukuonana na mteja wetu.

Nawaalika Wakili Peter Kibatala na Wakili Jeremia Mtobesya.

Anaanza Kibatala sasa anashukuru. Na yeye anatema ung'eng'e hapa.

Kibatala anasema ataanza na sheria s. 192 ya mwenendo wa makosa ya jinai inasema wazi kuwa

1. Maelezo ya awali yatasomwa kwenye mahakama ya wazi. Yameandikwa kwa herufi kubwa kabisa

Hakimu anasema Kibatala naomba useme taratibu mimi naandika

Kibatala anasema sheria zinasema endapo maneno ya sheria yako wazi na yanaeleweka basi sheria inapaswa kufuatwa kama ilivyo. Kusiwe na janjajanja yoyote.

Na katika kanuni hiyo ya msingi hakuna (exception) ni lazima mtuhumiwa awepo wakati wa kusikiliza Ph

GN. No. 637/2021 inazungumzia kuhusu uendeshaji wa mashauri kwa mtandao. Na hakuna mahali kokote inasema PH isomwe kwa http://mtandao.au mtuhumiwa asiwepo.

Kwa vile tunayo sheria mahsusi CPA inayosema namna Prelkminary hearing (maelezo ya awali) kusomwa basi tutumie sheria hiyo kama ilivyo.

Ni kinyume na sheria na haikubali na ni kujiongoza vibaya sana. Kwa upande wa mahakama kusema Maelezo ya awali yatasomwa kwa mtandao.

Hoja nyingine ni kwamba PH inapaswa kusomwa mbele ya Mtuhumiwa na sio tu mbele yake inasema sheria iwe kwneye mahakama ya wazi.

Nimeanza kuelewa hapa anayosema Kibatala pengine Lissu amekataa kwasababu anajua alipaswa kuletwa mahakamani ndio maana amewagomea Magereza. Huu mpambano mtamu sana.

Kibatala anasema ili tuisaidie mAhakama kutafsiri vizr kifungu cha 192(1) tunaomba isome 192(3) inasema mwisho wa yote hayo baada ya hoja za awali kusomwa PH mtuhumiwa atapaswa kusign memorandum

Mawakili wake watasign na mawakili wa serikali watasign

Sasa hapo neno la msingi ni lazima Memorundum iwe signed. Sasa mtuhumiwa hayupo hiyo memorandum tutampatia bodadboda apeleke magereza halafu aturudishie hapa mahakamani

Hii inaelezea kuwa lazima mtuhumiwa awepo maana ipo nyaraka ambayo atatakiwa kuisign hapa mahakamani.

Hoja nyingine anaendelea Kibatala

Baada ya PH kukamilika. Kunawezekana kuwepo kwa kutolewa vielelezo. Sasa Kanuni ya 5(3) kanuni za kuendesha mtandao inasema kama shahidi anataka kutoa kidhibiti lazima awepo mwenyewe.

Sasa kama itahitajika kuna kidhibiti kitolewe wakati wahusika hawapo kwa kipindi hiki. Kwahiyo inathibitisha kuwa tukiendelea kufanya hapa chochote yatakuwa ni mambo ya hovyo na sheria haitaki hivyo.

Maombi yetu tutayatoa baadae.

Sura nyingine ya pingamizi letu ni kwamba mahakama hii Ni Functus Officio ilishaamua kuwa PH Itafanyika live na mtuhumiwa atakuwepo.

Wakili Kibatala : Sasa haya mambo ya leo kuwa mtuhumiwa hayupo yanatokea wapi, mahakama ilisema mtuhumiwa atakuwepo hapa na mambo haya yalisemwa hapa mahakamani.

Kwahiyo mahakama inalazimika kumfanya mtuhumiwa kuwepo ili mambo yaendelee kama yalivyo pangwa.

Sheria zote nilizotaja hapo zinapaswa kuendana na rule ya Functus Officio kwahiyo mwenendo wa shauri la leo ni kuvunja kanuni kwanuni rule 4 ya kuendesha shauri mtandaoni ilipaswa kuwepo amri ya mahakama kisheria. Na imetolewa kwa pande zote.

Na kama kungekuwa na ulazima wa kusikiliza kwa mtandao tulipaswa kuambiwa

Wakili Kibatala anaendelea kuongea-; Rule 10 No. GN 367 na Hekima Wakili atasema. Tulitumiwa message ya kawaida kuhusu kusikilizwa kwa kesi hii saa tatu usiku.

Sasa haya yote ni nini saa tatu usiku unatutumia message kuwa kesi itasikilizwa kwa mtandao. Je hatuvunji sheria hapo? Rule 10 niliyosema inasema Mahakama ilipaswa kutoa siku 7 kabla taarifa ya kesi kusikiliza kwa mtandao.

Sisi tumepewa taarifa saa tatu usiku jana. Sasa hapo hatuvunji sheria. Hakuna taarifa yoyote (notice) haipo. Uwepo wa notice ni fair hearing kama notice haipo maana yake fair hearing haipo.

Kwahiyo uendeshaji wa shauri hili hauwezi kuwa wa haki na wa maana kama taarifa za namna kesi itasikilizwa zinatolewa kama message za wapenzi kusalimiana na kutakiana usiku mwema. Haikubaliki.

Wakili Kibatala anaupiga mwingi sana mpaka Mawakili Serikali wamepotea hewani 😂

Wakili wa Serikali Wakili Job Mrema kumbe alikuwa hasikilizi anaongea na simu huko ofisini kwao. Tunamuona live kwenye screen kubwa hapa Mahakamani. Watu wanacheka sana😂😂😂

Hakimu anauliza mnafuatilia kweli Mawakili wa Serikali naona unaongea na simu tu hapo.

Wakili wa Serikali Job Mrema anachekesha sana ni kama anaelekezwa jambo kwenye simu, Mahakama imesimama hapa kwa muda. Mambo ya ajabu kabisa. Hawa watu hawa nidhamu kwakweli.

Mawakili wa utetezi wamekerwa sana na kitendo cha mawakili waserikali wanaongea tu na simu huko

Wakili Kibatala anaendeelea, hakimu kasema we endelea acha wasisikilize.

Kanuni ya 10 pia inasema pia hiyo notice ya siku 7 tuliyopaswa kupewa inapaswa kujunuisha mambo mengi ikiwemo ni muda gani kesi hiyo itasikilizwa na mambo mengine kama vile marejeo kadhaaa ya kisheria. Kwahiyo notice ni muhimu na inahitaji mambo mengi.

Wanasheria watapeanaje kesi za marejeo kama hawatakuwa wanaonana. Ndio maana notice inatakiwa siku 7.

Sasa leo mkuu wa gereza anatuambia kuwa Lissu mtuhumiwa kagoma. Wakilili Kibatala anauliza Tunamuaminije yeye? Yeye ni rafiki yake LISSU au ndgu yake? Hatuwezi kumsikiliza yeye hapa.

Amerudi wakili wa serikali anasema hapo mwisho hatujamsikia wakili kibatala arudie.

Watu wanacheka 😂😂😂

Kibatala anasema mimi na mawakili wenzangu tulienda Jela, Ukonga Prison. Niliruhusiwa mimi tu 22/04 na mtuhumiwa aliniambia yafuatayo.

Siwezi kushiriki kwenye mwenendo wowote kwa njia ya mtandao ambao utakuwa kinyume na sheria. Hayo maneno aliniambia lissu mwenyewe kama wakili wake.

Na alisema hawezi kukubali shauri lake lisikilizwe kinyume na sheria. Kwahiyo msishangae leo kuwagomea huko magereza anasema fuateni sheria atakubali kusikiliza kesi yake. La sivyo hatakubali kabisa.

Kibatala anasema, Job Mrema anaomba ahirisho la siku 30 sasa hili ahirisho analoomba ni vituko. Haliko kisheria kabisa.

Anaendelea Kibatala-; Tusingeweza kuahirisha shauri kwa sababu zilizotolewa eti kwa siku 30 zote. Yani anaomba siku 30 tuahirishe kwasababu zipi? Kwanza ni mamlaka ya mahakama kujua kesi inaahirishwa kwa siku ngapi? Ameomba mambo hayapo kisheria. Na mahakama ikiamua lazima ahirisho liwe kwa kipindi kifupi sana.

Na sisi tuko tayari kuwepo kesho. Ahirisho hilo liwe hadi kesho. Tukutane hapa kesho. Na sio hizo siku 30 kama wanavoomba upande wa Jamhuri.

Wakili Kibata anaendelea

Anasema Job Mrema pia ameomba mambo ya kitoto sana hapa mahakamani. Sisi Mawakili tumezuiwa kumuona Mteja wetu kama Mawakili. Kwa mujibu wa sheria huko magereza ili tumuondae mteja wetu. Sasa leo Wakili wa serikali anadai eti mtupatie nafasi tukamshawishi mteja wetu akubali. Tunatumia njia gani? Mizimu au uchawi maana Magereza hawaturuhusu tunaenda kuongea nae vipi?

Katiba inasema mtuhumiwa achukuliwe hana hatia. Haya matendo yanayoffanyika hapa hayaeleweki kabisa. Akija Mzee Alute Lissu Wakili ataendelea eneo hilo.

Itoshe kusema kuwa ombi letu ni kwamba mahakama hii ina wajibu mtuhumiwaaliyepo Ukonga anapata haki yake ya kukutana na Mawakili Wake. Na tunaomba mahakama hii itoe amri kuwa waseme kwanini wametuzuia mawakili kumuona.

Mkuuu wa Jeshi la Magereza Dar es Salaam na Mkuu wa Gereza la Ukonga Wote waje waeleze Mahakamana kwanini wametuzuia mawakili tusiende kumuona.?

Pia tunaomba Mahakama itoe amri kwanini ndugu wa Lissu na mawakili wamefanyiwa matendo ya hovyo na Mapolisi. Wakiwa wanaingia hapa mahakamani.

Kwanini Mapolisi leo wapo wengi hapa Kisutu. Wanawazuia ndugu wa Lissu. Je mahakama iliambiwa kuwa wateja wa mahakama na ndugu wa Lissu watasumbuliwa leo. Je mahakama inafahamu hayo yakiyofanywa na Mapolisi.

Hakuna maombi yoyote (application) kwenye hii mahakama kuwa umma hautaruhusiwa kwenye mahakama hii. Kama ambavyo kifungu cha 186 cha CPA kinachosema umma unayo haki ya kuhudhuria mahakama ya wazi na kuangalia kesi.

Sasa hakuna order yoyote ya mahakama na sisi tunaiomba mahakama iwape haki yao ya msingi ndugu wa Lissu, marafiki wa Lissu, Mawakili wake na umma wote uhudhurie mahakamani kwa mujibu wa sheria ili haki si tu itandeke bali ionekane ikitendeka.

Anamalizia Wakili Kibatala kwa kusema Mahakama ya wazi ni haki ya msingi sana na mahakama iwe na wivu sana kulinda jambo hili kisha anamkaribisha JEREMIAH MTOBESYA.

Pia soma > KESI YA LISSU: Mtandao changamoto, hakimu aahirisha kwa muda
Watu wengi waelewa huwa wanawaambia CCM na serikali yake mara nyingi kuwa, CHADEMA imejaa wasomi haswaaaaa! CCM imejaa machawa na watu wakujipendekeza, hawana weredi kabisa.

Sasa kuongea na simu wakati wako live kwenye mtandao si aibu kubwa hiyo Kwa serikali. Alafu Kwa njia ya mtandao watu wote duniani wanaona, hivyo serikali haikuona hili. Yaani serikali inatakiwa kujitafakari Kwa kina juu ya suala hili, maana ni aibu kubwa sana kimataifa.

Nawapongeza sana wakili kibatala na wenzake, nawambia Kwa herufi kubwa "WAMEONGEZA CV ZAO NA HESHIMA KUBWA KIMATAIFA"
 
Back
Top Bottom