Pre GE2025 Tundu Lissu atahadharisha uchaguzi ndani ya chama kuingiliwa na fedha za Rais Samia na mwanae Abdul

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wananunua madaraka nakuita wenzao wezi.

Mtoa rushwa anapo sahau kuwa rushwa nayo ni jinai na inaondoa integrity vile vile.
anapoona wagombea wanapesa za ajabu ajabu yawezekana yakawa ni mapandikizi ya ccm. Na ukajikuta uongozi mzima wa mkoa ccm tupu, baadae yanajifaragua na kusema narudi ccm, kumbe yalitoka hukohuko.
 
Haya Yameanza leo? Magu alidhibiti hili and soon mama atabana tena hizi pesa za wafadhili wenye agenda
Umenichanganya kwelikweli na andiko lako hili.
"...soon mama atabana tena hizi pesa za wafadhili wenye agenda"?
Sasa sijui kama huyo mama atabana vipi endapo yeye ndiye mwenye agenda!
 
Ningeungana nawe kutia mashaka kama ingekuwa ni wakati wa Magufuli. Hawa wawili wapo karibu sana na Mama; kama alivyo Mbowe.
Chunga sana namba.
Jamaa ameshindwa kuelewa kwamba viongozi wandamizi karibia wote wapo karibu sana na mama au yule jamaa mstaafu adui wao alikuwa mwendazake naona TAL ndiye kagoma kuelewa somo
Ningeungana nawe kutia mashaka kama ingekuwa ni wakati wa Magufuli. Hawa wawili wapo karibu sana na Mama; kama alivyo Mbowe.
Chunga sana namba.
 
Ni wagombea wanahonga? Inatakiwa Chadema iwe macho sana kwa sababu CCM wanaweza kupandikiza watu ili wakivuruge chama.
Ni vizuri kwamba hili limefahamika kungali mapema. CHADEMA wakishindwa kulidhibiti hili, itakuwa ni halali kwao kusambaratika. Hakuna wa kumlaumu tena, bali watajilaumu wenyewe.
 
Jamaa ameshindwa kuelewa kwamba viongozi wandamizi karibia wote wapo karibu sana na mama au yule jamaa mstaafu adui wao alikuwa mwendazake naona TAL ndiye kagoma kuelewa somo
Hili nilianza kulielewa kwa mara ya kwanza niliposikia hotuba ya Mbowe aliyoitoa kule ughaibuni akiwahutubia diaspora wa Marekani kuhusu uhusiano wake na mama kwenye wakati wa mazungumzo ya maridhiano. Toka wakati huo; na baadaye kidogo kufuatiya sarakasi zilizofanyika ndani ya chama kupoza msimamo waliokuwa wamufikia kama chama kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na ule uchaguzi mkuu.

Hitimisho langu baada ya hapo, nikajuwa CHADEMA ya Mbowe tayari wanajiandaa kuungana na CCM ya Samia kwenye chaguzi hizo na serikalini endapo kama Samia atapenya kwa njia yoyote atakayoitumia kuendelea madarakani.

Msimamo wangu huo, sasa unazidi kuimarika, mambo kama haya anayoyazungumzia Tundu Lissu kwenye mikutano hii.

Sasa sijui CHADEMA itakuwaje, na inawezekana pia tukaanza kuulizana swali kama hilo huko ndani ya CCM. Sijui.
 
Naangalia maandamano namuangalia Lissu nawaangalia wandamanaji ...kuna sauti ya Mungu inatembea!!!
 
Umenichanganya kwelikweli na andiko lako hili.
"...soon mama atabana tena hizi pesa za wafadhili wenye agenda"?
Sasa sijui kama huyo mama atabana vipi endapo yeye ndiye mwenye agenda!
Hana agenda unayotaka ionekane hivyo
 
AISEEE!.
Tulisha sema humu. Pesa ya Mwarabu itamwagika uchaguzi utakapowadia; lakini naona wameamua kuwahi mapema.
Pesa sasa hivi iko kila mahala mpaka kwenye halmashauri vijijini, ndani ya ccm,kwenye wilaya,vijiji vitongoji nk kwa kofia ya mikopo kwa vikundi,miradi na watu binafs.Na hii sasa naona ni mpaka kwenye Upinzani zimetua. Hii hatari Nyerere huko aliko anajuta.Madaraka kwa pesa.Jamani Rupia haijawahi kushindwa CDM ni tegemeo la wananchi msihongeke kirahisi hivyo ondoeni makapi yarudi huko. Shida ni Kanda ya Nyasa. watchout!
 
Hizi wanazozunguka Nchi nzima wamezitoa wapi?
 
Mnaparurana wenyewe kwa tamaa zenu halafu lawama mnapeleka kwingine.Kundi la maskini na kundi la kibosile tuone nani atashinda.
 
Serikali ndio inapaswa kulipa wafanyakazi hawa sio CCM
 
Dalili za kuweweseka, yaani hela za Samia inakuaje ziwepo huko Chadema?

Au mgombea wake maji ya shingo?
 
Dalili za kuweweseka, yaani hela za Samia inakuaje ziwepo huko Chadema?

Au mgombea wake maji ya shingo?

View: https://twitter.com/Sisimizi3/status/1786241828036985268?t=ftaN6u1Guu1cMwnRJrBe3w&s=19
 
Inahitaji akili kubwa kuelewa anapoona wagombea wanapesa za ajabu ajabu yawezekana yakawa ni mapandikizi ya ccm. Na ukajikuta uongozi mzima wa mkoa ccm tupu, baadae yanajifaragua na kusema narudi ccm, kumbe yalitoka hukohuko
Pesa za ajabu ajabu ndio pesa zipi? Sugu na Lisu au Msigwa nani ana pesa?

Umaskini ndio uweledi? Huu ni ujinga wa wajima,ni wapi huko pesa Huwa haitumiki kwenye chaguzi?
 
Pesa za ajabu ajabu ndio pesa zipi? Sugu na Lisu au Msigwa nani ana pesa?

Umaskini ndio uweledi? Huu ni ujinga wa wajima,ni wapi huko pesa Huwa haitumiki kwenye chaguzi?
Ndiyo maana nimekwambia akili kubwa ndiyo inang'amua pesa za ajabu ajabu ndizo ziliwanunua akina Joshua nasari na akina harima mdee sio rahisi wewe mwenye ubongo wa kuku kuelewa
 
Matokeo ya kupokea makapi kutoka CCM na kuwapa audience kubwa ndani ya chama.

Rushwa imeasisiwa na Chanzo Cha Matatizo na inarnea kwa kasi kubwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…