Pre GE2025 Tundu Lissu atahadharisha uchaguzi ndani ya chama kuingiliwa na fedha za Rais Samia na mwanae Abdul

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndiyo maana nimekwambia akili kubwa ndiyo inang'amua pesa za ajabu ajabu ndizo ziliwanunua akina Joshua nasari na akina harima mdee sio rahisi wewe mwenye ubongo wa kuku kuelewa
Pesa za ajabu ajabu ndio pesa gani? Akili kubwa ndio inakuaje?
 
Lissu: Ni pesa za Abdul na mamake.

Swali: Pesa hizo zimeingia kupitia mlango upi, au zimepitia dirishani?

Bado natafuta jibu.

Kwako Erythrocyte
Kutokana na hotuba hiyo ni dhahiri kuna kiongozi mkubwa ndani ya chama hicho anamwaga pesa kuandaa Viongozi watakao muunga mkono.

Hotuba ya Tundu Lissu inaonyesha hali ya mambo ndani ya chama hicho haiko sawa.
 
Kum. 16:19-20 Usipotoe maamuzi , wala usipendelee uso wa mtu , wala usitwae rushwa ; Kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili , na kugeuza daawa ya wenye haki . Yaliyo haki kabisa ndiyo utayoyafuata , ili upate kuishi na kuirithi nchi upewayo na Bwana , Mungu wako .
Abdul afanye sarakasi zake zote ila Mungu ataingilia kati na wenye haki ndio watairithi nchi ya Tanganyika.
 
Yeye mwenyewe Hana uhakika na hocho cheo Cha umakamu mwenyekiti kama atarudi .Anaogopa Wenye pesa kumpinga chini
 
Inaonekana mwalimu na mwanafunzi wanaplay checkers hii ni hatari kwa chama tawala
 
Natamani siku moja huko mbele hawa watu wawajibishwe wote bila ya kuoneana haya. Kila mtu kwa kipimo chake cha ushiriki katika kulinajisi taifa letu.
 
Katika hali halisi Chadema ni hatari mno kwa CCM, na hasa kwa mgombea wa ccm akibaki kuwa Hangaya, kwahiyo njia pekee ni kwa ccm kupenyeza watu wao, ndio maana Lissu kaanika mambo hadharani, Nakusanya Taarifa na nitaliweka hadharani hivi punde
Kweli ccm hawana presidential material kwa sasa
 
Ila amewaambia ukweli. Mbowe aisee anafanya maandamano nchi nzima kumbe hamna kitu
 
Maswali matatu kwa Lissu:
1. Ni wakina nani wanaotumia fedha nyingi za uchaguzi ndani ya Chadema? (Kwa maana wanaodaiwa kuhongwa). Atutajie tuwajue mfano, Lissu, Msigwa, Sugu, Mbowe, Heche au nani ili tumwamini.

2. Pili, atwambie ni shilingi ngapi?

3. Tunaomba vielelezo kwa anaowatuhumu kutoa fedha. Walizitoa lini, wapi na kwa njia ipi? Picha na vielelezo# Vingjnevyo ni story za kihuni kwenda kwa wahuni wa vijiweni tu.πŸ™πŸ™πŸ™
 
Wakati huu wa uchaguzi Chadema wanaogelea katika bahari ya hela, je ruzuku yetu iko salama? Hiki chama ndio huwananga CCM kila siku, kumbe ndani kimeoza, kinapendeza kwenye maneno ya ilani tu, ndani tayari kuna uvundo.

Wanahongana katika chaguzi na kule Njombe wapiga kura walizichapa ngumi kugombea rushwa
 
Cdm ni tofauti kabisa na ccm, viongozi wa ccm huwezi kuona wanakemea matumizi ya fedha chafu, cdm kiongozi mkubwa anajitokeza anakemea matumizi ya pesa chafu hadharani. Ingekuwa ni ccm wangenyamazia kimya, na kuishia kutoa story za upotoshaji.
 
Cdm ni tofauti kabisa ccm, viongozi wa ccm huwezi kuona wanakemea matumizi ya fedha chafu, cdm kiongozi mkubwa anajitokeza anakemea matumizi ya pesa chafu hadharani. Ingekuwa ni ccm wangenyamazia kimya, na kuishia kutoa story za upotoshaji.
Membe na Lowasa walikemewa
 
Cdm ni tofauti kabisa ccm, viongozi wa ccm huwezi kuona wanakemea matumizi ya fedha chafu, cdm kiongozi mkubwa anajitokeza anakemea matumizi ya pesa chafu hadharani. Ingekuwa ni ccm wangenyamazia kimya, na kuishia kutoa story za upotoshaji.
Bado hujasema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…