Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Polisi Nyamongo wameshambulia msafara wetu kwa mabomu ya machozi wakizuia njia kuelekea kwenye mkutano wetu wa kampeni

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Polisi Nyamongo wameshambulia msafara wetu kwa mabomu ya machozi wakizuia njia kuelekea kwenye mkutano wetu wa kampeni

..sidhani kama angetumia zaidi ya dakika 10 kuzungumza na kusalimiana na watu hapo barabarani.

..TL amepita maeneo mengi hapa nchini na hakukuwa na matatizo yoyote, tena hata majuzi alianza kuwasifia jeshi la polisi.

..sidhani kama kuna ulazima wa kupiga mabomu kampeni ya chama chochote kile. kwa ujumla wananchi wamekuwa watulivu, wameonyesha uchangamfu, furaha, na hamasa, sidhani kama ni busara kwa jeshi la Polisi kuwapiga mabomu wananchi walio katika hali hiyo.

Kwa aliyoyaongea yule bosi wa NEC, na hili la polisi, nahisi kuna shinikizo kutoka ofisi kuu.

Wameona wanapoteza baada ya kumpa Lissu fair ground, walimu underrate mwanzoni.

Sasa hivi ndo kampeni zimeanza sasa, tusubiri kuona mengi.
 
Robert Amsterdam ndie kiboko ya madikteta ya afrika ana file case directly the Hague, mbali na jiwe pia anamshughulikia dikteta Paul biya wa Cameroon.Jiwe ndo akome kumsikiliza kagame badala ya kuwasikiliza watz check alivyomuuza anachukiwa Kama mavi nchi nzima sasa

Jiwe ni vema ukaacha kampeni na kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha URAIS. Unachukiwa nchi nzima kwa udikteta. Nchi hii si ya kwako. ONDOKA.
 
Sasa kama Magu ni rais anapita kuomba kura za nini?
Polisi wanachofanya ni kuinua zaidi ari ya wapenda mabadiliko na wanampaisha zaidi Lissu kwa watz na dunia nzima kutaka kufuatilia kwa karibu.
Bado watawala wa Tanzania hawajajua bado kwamba tukio la kujaribu kumuua Lissu huko Dodoma ndio limemweka juu kabisa kileleni aliko sasa.
"Haki huinua taifa"
Haki ya nani hivi unaamini kabisa kanda ya Ziwa na kaskazini kwa ujumla Lissu atamshinda kura Magufuli, sehemu ngumu kwa CCM huko ni Kilimanjaro tu na miaka yote CCM wakifanya mikutano yao wana ujaza umati kushinda ya Lissu anayopata kanda ya Ziwa.

Unasoma sana sensationalised headline za bavicha humu kwenye post “Lissu sijui ashangaza dunia kwa mkutano wake” etc with nonsense unadhani CCM ni political amateurs.

Hizo headlines za kufurahishana tu wafuasi wa CHADEMA uhalisia Lissu awezi mshinda Magufuli uchaguzi fairly and squarely.
 
Kwa aliyoyaongea yule bosi wa NEC, na hili la polisi, nahisi kuna shinikizo kutoka ofisi kuu.

Wameona wanapoteza baada ya kumpa Lissu fair ground, walimu underrate mwanzoni.

Sasa hivi ndo kampeni zimeanza sasa, tusubiri kuona mengi.
Cha muhimu ni kuitisha wachunguzi zaidi wa haki za binadamu na pia ICC FBI Scotland Yard na vyombo vingine waongeze uchunguzi ili baada ya uchaguzi wahusika wote wafikishe mahakamani The Hague
 
Cha muhimu ni kuitisha wachunguzi zaidi wa haki za binadamu na pia ICC FBI Scotland Yard na vyombo vingine waongeze uchunguzi ili baada ya uchaguzi wahusika wote wafikishe mahakamani The Hague

Nani atawaitisha sasa wakati serikali hii bado iko madarakani?
 
Watanzania wenzangu na wanachadema wenzangu tusipo angalia vizuri huyu Tundu Lissu atatupeleka pabaya, tumeishi kwa amani na upendo kwa miaka mingi lkn sasa anataka kutuchonganisha sisi kwa sisi, hatutaki kabisaaa
Hakuna amani ambapo hakuna haki sisi CCM ni waonevu sana
 
Haki ya nani hivi unaamini kabisa kanda ya Ziwa na kaskazini kwa ujumla Lissu atamshinda kura Magufuli, sehemu ngumu kwa CCM huko ni Kilimanjaro tu na miaka yote CCM wakifanya mikutano yao wana ujaza umati kushinda ya Lissu anayopata kanda ya Ziwa...
Duh, haya bana.
Yaani kwenye media zote kuanzia tv, radio, magazeti nk zilitekwa nyara kumsifia Magu na kuimba nyimbo za kuabudu.

Sasa unalalamikia habari za vijimedia vya kujitegemea kuandika habari za kweli kumhusu Lissu tena kwa mda huu mfupi tu wa kampeni.
Habari zoote zinazotolewa na vyombo vya habari nimejitahidi kuzisoma/tazama.

Najua kuchagua na kupambanua kati ya kweli na uongo, propaganda na uhalisia.
 
Mimi siyo mwanasheria lakini najua mgombea yoyote iwe wa urais, ubunge au udiwani akivuruga ratiba au utaratibu malalamiko yanapelekwa tume ya uchaguzi mara moja.

Hili halihitaji mgombea kuwaelimisha polisi halafu wanamruhusu aendelee na tukio.

Maendeleo hayana vyama!
Uwage unaona na aibu
 
Ari ya nani hivi unaamini kabisa kanda ya Ziwa na kaskazini kwa ujumla Lissu atamshinda kura Magufuli, sehemu ngumu kwa CCM huko ni Kilimanjaro tu na miaka yote CCM wakifanya mikutano yao wana ujaza umati kushinda ya Lissu anayopata kanda ya Ziwa...
CCM husomba watu na fuso kutoka wilaya zingine kujaza mikutano yenye wanafunzi wengi hakuna Mtanzania mwenye Akili timamu ataenda mwenyewe kwenye mkutano wa CCM, CCM bila wasanii wa bongo fleva haji mtu watu wanaenda kusikiliza mziki siyo sera mbovu za CCM, uchaguzi huru na haki CCM bye bye.
 
Anataka nayeye asimamishe magari barabarani kama Magufuli, kwenye kichwa chake yeye kama raia na raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania nyadhifa zao ni sawa.

Mwisho wa siku tutakuja kubaliana jamaa ‘mtambo’.
Puppets walikuwepo toka zamani kina chief mareare
 
Akili zako na huyo Lissu sawa sawa. Unataka aachiwe asimame katikati ya barabara kama raisi wa nchi? Tena ka audience chenyewe cha watu 200-300 kisa tu ku entertain his mental health issues yeye na raisi wa nchi ni watu sawa.

I think his honeymoon period should be brought to an end as days go Lissu is becoming a real pest.
Rais ni mtu tu lakini kama mimi na wewe
 
Jiwe ni vema ukaacha kampeni na kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha URAIS. Unachukiwa nchi nzima kwa udikteta. Nchi hii si ya kwako. ONDOKA.
Akirudi Tena kipindi cha pili atatubomolewa nyumba zetu.

Anga limemkataa, ndumba zikiexpire,Mungu kamnyima kibali anauwa kondoo badala ya kuwachunga, atukumchagua anapambane na Mbowe Bali shida zetu akajipa majukumu kufanya tusiyomtuma. Akubali kurudi Chato au aende the Hague
 
What a load of nonsense, kuendelea kumchekea Lissu ni ku entertain his fantasy; yaani azuie shughuli za watu wengine barabarani kisa tu kichwani kwake anajiona ni sawa na raisi.

This joke has gone too far.
usikute ulisoma mpaka chuo kikuu
 
Yeye anasikiliza porojo za Magu anapodai kasimamishwa njiani ni anadhani kweli. Wakati kiuhalisia kila kitu kinakuwa kimepengwa na ulinzi wa kutosha umesha tayarishwa.

Mahala ambapo ulinzi aujapangwa ata watokee maelfu barabarani Magufuli asimami.

Magufuli akicheza na yeye anacheza jukwaani the guy is obsessed na Magufuli anataka aige kila anachofanya.
Magufuli akiacha compaign nae anaacha
 
Hizo preveledge ni za raisi wa nchi hanazo.

..wananchi waliokusanyika hawajui kama hawatakiwi kumsalimia mtu asiyekuwa Raisi hapo barabarani.

..wananchi haohao ndio waliomchagua Raisi. Na wananchi haohao ndio kodi zao zimetumika kununua mabomu ya machozi.

..binafsi naamini Polisi hawakutumia busara.
 
IGP RPC OCD wote wanaoshiriki vitendo vya kuwaonea wapinzani kuhatarisha Amani watambue kuwa mara baada ya uchaguzi watafikishwa ICC The Hague kujibu tuhuma zao
Robert Amsterdam anafile kesi moja kwa moja the Hague,wamuulize Uhuru Kenyatta na mkuu wa polisi Kenya wawape dondoo za kule.Dunia haiwezi kaa kimya haki za watu zikivunjwa, hata hao mabeberu wamechoka kuhudumia wakimbizi wazalishwao na haya majitu yaliyokosa malezi Bora utotoni
 
Mkuu iweke kama Breaking News Dunia nzima inaangalia huu UCHAGUZI
Unadhani Dunia ni ndogo kama kijiji! Yaani watu wanapambana na hali zao huko, Covid-19, uchumi mbovu, uchaguzi wa US, North-South Korea tension etc. Wewe unawaza Dunia iwafikirie kisa mmefukizana moshi mitaani uko!
 
Back
Top Bottom