Volodimiri Zelensiki
JF-Expert Member
- Jan 3, 2015
- 1,154
- 3,417
Mambo yanazidi kunoga.Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Rais Samia amemlipa stahiki zake kama mbunge ambazo ni kiinua mgongo, Serikali ya Rais Magufuli ilikuwa imekataa kumlipa...
Mimi sina pingamizi kuhusu hili. Penye Haki , umoja na mshikamano na utawala bora maendeleo yanakuwa ni swala la muda tu. Ni AUTOMATICHuu ni uthibitisho kuwa Rais Mama Samia ni mpenda haki, mtenda haki, atabarikiwa, nchi itabarikiwa na itaneemeka kisiasa, kiuchumi na kijami...
Mimi ni Mkristo wa Katoliki niliyebatizwa na kupata kipaimara.Waislamu wa bongo wanaroho nzuri sana kuliko wakristo sijui kwanini
Alipenda kusifiwa kuliko sifa yenyewe😁😁😁Angekuwa yule jamaa, tukio lingefanyikia Ikulu, vyombo vyote vya habari live...na masimango juu, kwa mlipwaji!
Kwani kuna mahali nimesema umoja party na ngongwe wanamstakabali mwema na taifa ?🤔Ila umoja party na ngongwe ndio Wana mustakabali mwema na taifa?
😅😅😅😅Angekuwa yule jamaa, tukio lingefanyikia Ikulu, vyombo vyote vya habari live...na masimango juu, kwa mlipwaji!
Usidhani kila anae kosoa Ni mtu wa vyama vyama au ni timu wagufuli unapaswa kufahamu hivyoIla umoja party na ngongwe ndio Wana mustakabali mwema na taifa?
Jitahada anazofanya Mama Samia Suluhu Hassani ni za kupongezwa na kila mpenda Mema.Kwamza wanajukwaa Nina wasalimu kwa jina la jamhuri ya Muungano wa Tanzania....
Sasa hivi yeye ndiye atadai sasa😅..mbona Ndugai alikuwa akisisitiza na kujiapiza kuwa Lissu hadai chochote?
Leo watalala na viatu tena.Kuna wana CCM hawatapenda hii kitu.
Tunashukuru kwa Hilo.Samia kusema kweli Ana utu,japo sio kwamba nampenda ila kwenye hili namsifu, ajira Sasa hivi nje nje tu
Inabidi uamkie shikamoo!! Na usiseme rais tu sama mama pia! Wakati mwingine wema ni fimbo nzuri sana!! Inajua kukata mzizi wa fitina!!Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Rais Samia amemlipa stahiki zake kama mbunge ambazo ni kiinua mgongo, Serikali ya Rais Magufuli ilikuwa imekataa kumlipa...
[emoji38][emoji38][emoji38]Nakumbuka hata Magufuli ulisema hivihivi kuhusu yeye
Kweli kabisa SS wote ni watanzania na CCM watambue kwamba hii nchi hawawez kuijenga peke yao. Ndio maana miaka 60 ya Uhuru maendeleo hayaendani na mda, tubadilike tuijenge nchi yetu.Mimi sina pingamizi kuhusu hili. Penye Haki , umoja na mshikamano na utawala bora maendeleo yanakuwa ni swala la muda tu. Ni AUTOMATIC
nimemwelewa Mh Tundu Lissu. Akirudi Tundu anakuwa msalaba kwa Rais Samia. Kama wanaelewa hili aisee wafanya jambo.Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Rais Samia amemlipa stahiki zake kama mbunge ambazo ni kiinua mgongo, Serikali ya Rais Magufuli ilikuwa imekataa kumlipa.
Pia Serikali ilimuambia aandike barua pamoja na kuambatanisha na nyaraka ili apewe fedha zake za matibabu ambazo Serikali ya Rais Magufuli pia ilikataa kumlipa.
Pia Tundu Lissu amesema wanachama wa Chadema ambao walifungwa ama kuwekwa mahabusu kipindi cha Magufuli wameachiwa kasoro kesi chache ambazo nazo zinashughulikiwa.
Tundu Lissu alikutana na Rais Samia alipotembele nchini Ubelgiji ambapo waliongea mambo kadhaa ikiwemo stahiki hizo.
Magufuri kwa huku bongo tulishafunga jarada lake,ajee na mengine tuu Kama unajuwaa kwa kuendeleza kusema vibaya ndio itafaa kwahapa tz amefeli,sisi letu liko moyoni tukutane 2025.Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Rais Samia amemlipa stahiki zake kama mbunge ambazo ni kiinua mgongo, Serikali ya Rais Magufuli ilikuwa imekataa kumlipa.
Pia Serikali ilimuambia aandike barua pamoja na kuambatanisha na nyaraka ili apewe fedha zake za matibabu ambazo Serikali ya Rais Magufuli pia ilikataa kumlipa.
Pia Tundu Lissu amesema wanachama wa Chadema ambao walifungwa ama kuwekwa mahabusu kipindi cha Magufuli wameachiwa kasoro kesi chache ambazo nazo zinashughulikiwa.
Tundu Lissu alikutana na Rais Samia alipotembele nchini Ubelgiji ambapo waliongea mambo kadhaa ikiwemo stahiki hizo.
Magufuli ndio Rais aliyekopa kuliko marais wote, sema nyie mazezeta aliwaambia fedha za ndani kwa kuwa hamjui lolote mkaitikia tuWatu wengi humu hawajui tofauti ya kiuongozi kati ya JPM na bi Hangaya.
Magu alikuwa na mkakati wa kuendesha nchi kwa kutumia pesa za ndani huku akikopa kidogo.
Samia yeye anaendesha nchi kwa
kukopa sana huku akiacha maingizo ya pesa za ndani zikiwa hazina msukumo wowote.
Kwani unaumia akisemwa vibaya?Magufuri kwa huku bongo tulishafunga jarada lake,ajee na mengine tuu Kama unajuwaa kwa kuendeleza kusema vibaya ndio itafaa kwahapa tz amefeli,sisi letu liko moyoni tukutane 2025.