Tundu Lissu: Rais Samia amenilipa stahiki zangu nilizonyimwa na Magufuli

Tundu Lissu: Rais Samia amenilipa stahiki zangu nilizonyimwa na Magufuli

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Rais Samia amemlipa stahiki zake kama mbunge ambazo ni kiinua mgongo, Serikali ya Rais Magufuli ilikuwa imekataa kumlipa.

Pia Serikali ilimuambia aandike barua pamoja na kuambatanisha na nyaraka ili apewe fedha zake za matibabu ambazo Serikali ya Rais Magufuli pia ilikataa kumlipa.

Tundu Lissu alikutana na Rais Samia alipotembele nchini Ubelgiji ambapo waliongea mambo kadhaa ikiwemo stahiki hizo.


Kuhusu kurudi anamuwekea Rais Samia masharti yasiyo na maana.

Anyway Rais Samia ni mpango wa Mungu. Yule shetani aliharibu sana nchi yetu
 
2025 wapinzani wote wa mama watakuwa wanamuunga mkono..2025 anapita bila kupingwa

Siasa ni sayansi.
Naunga mkono kwa namna mama anavyoenda na wapinzani.

Huko kwenye ubunge ndiyo kutakuwa na kilio na kusaga meno.

Majimboni CCM wajipange sana, hakutakuwa na kubebana.
 
Umesema kweli, mimi ni mkiristo ila nakiri kuwa ndugu zetu waislamu wana utu sana.
Tatizo la watanzania wengi tuna low thinking capacity. Nadhani ni sababu ya lishe, makuzi, utamaduni na elimu. Mtanzania mwonyeshe tarakimu moja tu yeye tayari ameshatoa conclusion kama amefanya research ya miaka 50! Mtu kama wewe unaangukia kwenye hili kundi. Samia hajafanya lolote jipya bali amesema haki itendeke. Kwanza kitendo cha mambo madogo kama haya kutegemea utashi wa rais ni hatari kubwa. Na bado haoni ulazima wa kubadilisha mfumo na raia kama wewe pia hamuoni ulazima wa kubadili mfumo! Mnabaki kusifu kitu ambacho bado kinaweza kujirudia wakati wowote!
 
Job Ndugai hapo anataka kujinyonga!
Mgonjwa aghali zaidi duniani, aliishahakikishiwa na Shetani wa Burigi kuwa watatawala 'wanavyotaka' na kudumu milele
1654097985625.png
 
Siasa ni sayansi.
Naunga mkono kwa namna mama anavyoenda na wapinzani.

Huko kwenye ubunge ndiyo kutakuwa na kilio na kusaga meno.

Majimboni CCM wajipange sana, hakutakuwa na kubebana.
Na Kinana alisisitiza hilo
 
Waislamu wa bongo wanaroho nzuri sana kuliko wakristo sijui kwanini
Acha udini we Kafiri, mbona JPM alimtoa Babu Seya jela ambaye aling'ang'aniwa miaka na miaka na yule Muislamu lakini hukusema kuwa Wakristo wa Bongo wana roho nzuri sana kuliko Waislamu [emoji848][emoji19]

Ficha upumbavu wako [emoji34]
 
Serikali ya Rais Magufuli pia ilikataa kumlipa.

Kodi zetu tulizolipa mwendazake (revered) hayati (late) rais John Pombe Joseph Magufuli alizifanya kama pesa zake binafsi anazotoa mfukoni.


Kongole kwa awamu kutambua kuwa pesa zilizopo katika fuko kuu la serikali ni mali ya walipa kodi hivyo katiba, sheria, kanuni na taratibu hutakiwa kufuatwa na siyo ridhaa ya rais kufanya anayohisi
 
Kama amelipwa kinachomfanya aendelee kukaa kwa amsterdam ni nini , au ukuni

Acacia hawajatushitaki MIGA sasa
 
Rais wetu mwenye utu, mwenye upendo, mwenye kutaka Amani na watu wote. Yaani Mungu ulituona. Iwe CCM au Chama chochote kile Amani na utu ni msingi wa kila kitu. Nina Amani hata kama pesa sina. By the way Rais hajazi watu pesa mifukoni bali kupitia wataalam wake anajenga mazingira Safi ya kupata pesa. Hongera Sana Rais wangu wa Moyoni kabisa.
 
Wale wafuasi wa lile zimwi la Chato wanasaga meno kwa hasira,hii mijitu ina roho za kishetani sana
Yaani hapo walipo wanajiharishia hovyo tu. Hawaamini kinachotokea. Siasa siyo chuki hata kidogo. Pongezi nyingi to our Her Excellency SS Hassan.
 
So all is well ?

Aluta Discontinued ?

Ni Vema na Haki ila naona nguvu nyingi zinatumika kwa sasa kwa Samia this JPM that na tunasahau / wanasahau kutumia muda wa kuimonitor CCM
😂 😂Aluta discontinued
 
Ni jambo jema. Sijui Ndugai anajisikiaje na ule ujeuri wake
Yuko jikoni anaota Moto na kusogeza kuni jikoni. Yahudi yule. Imeandikwa ole wake amtegemeaye Mwanadamu Chattel.
 
Ni Mtanzania.Kwa nini asiungwe mkono kama anakataa uonevu na ujinga?Huwa kuna mambo tunakosea kuwaza.Kwani upinzani umetokea wapi?Ni kwa sababu ya kutoridhishwa na mienendo ya kisiasa tu.Kama mambo yanaenda uzuri,nani atakuwa mkinzani?Tafakari.
Kabisa Mkuu. Tunachotaka ni kiongozi Bora. MTU atampinga nini wakati hakuna cha kupinga. Mungu ampe uhai na afya mpaka 2030 ulingo mpya uanze. Tunakuombea Rais wetu.
 
Back
Top Bottom